Askofu Zakary Kakobe
Askofu Mkuu wa kanisa la Full Gospel Bible fellowship (FGBF), Zakary Kakobe, ameweka wazi kukoshwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli kwa kuweza kuingiza ndege nyingine ya Air Bus 220-300.
Askofu Kakobe ameyasema hayo leo katika mapokezi ya ndege ya sita zilizoingizwa nchini katika awamu ya uongozi wa Rais Magufuli.
Kakobe ametumia nafasi yake ya kuliombea taifa kutoa maneno hayo kwa Rais Magufuli, ambapo amesema kwamba, " Mimi ni mbishi sana. Ukiniona nimekanyaga mahali hapa ujue umenikosha sana".
Askofu Kakobe amemuomba Rais Magufuli atumie siku ya leo kwa kulala ikiwa ni sehemu ya kujipongeza kwa kufanikisha kuingiza ndege nyingine nchini ( kwa kuwa Rais Magufuli aliwahi kutamka hadharani kwamba kitanda chake kimejaa ma-file, kiasi cha kumnyima usingizi).
Mbali na hayo, kiongozi huyo wa dini amemsifu Rais Magufuli kuwa kama Rubani na kwamba Watanzania wanakusanya kodi na yeye amekuwa akizitumia kwa usahihi.