Tuesday, 8 January 2019

WAJASILIAMALI 1317 BUKOBA DC WATAMBULIWA TAYARI KUPEWA VITAMBURISHO

Na Allawi Kaboyo- Bukoba. Katika kutekeleza Agizo la Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Wamezindua zoezi la kugawa Vitambulisho kwa wajasiliamali wadogo wadogo katika Halmasahauri yao, Zoezi ambalo limefanyika katika Ukumbi wa Halmashauri hiyo Januari 7, 2019. Akizungumza mara baada ya kugawa Vitambulisho hivyo Mh. Deogratius Muganyizi Kashasha (Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya Bukoba) Amewataka wajasiliamali hao kuwa mabalozi kwa wengine ambao hawajapata Vitambulisho hivyo ili wafanye Hima kujipatia Vitambulisho vitakavyowawezesha kufanya biashara zao bila usumbufu wowote, sambamba…

Source

Share:

Monday, 7 January 2019

MADAWATI YA NMB YAWANUSURU WANAFUNZI KUKAA CHINI TANDAHIMBA

Na Bakari Chijumba,Mtwara. Wakati shule zikiwa zimefunguliwa rasmi January 7 2019 kwa ajili ya kuanza kwa muhula mpya wa masomo kwa mwaka 2019, Benki ya NMB imetumia siku hiyo kutoa msaada wa madawati na vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya Tsh. Million 15, kwa shule tatu za sekondari zilizopo wilayani Tandahimba Mkoani Mtwara. Msaada huo uliotolewa na Nmb ni Madawati mia moja kwa shule mbili za Namikupa na Naputa na vifaa vya ujenzi ikiwemo bati zaidi ya mia tatu kwa shule ya sekondari Tandahimba, ambayo iliezuliwa paa kwa upepo mwaka…

Source

Share:

AJINYONGA KWA UGUMU WA MAISHA NA KUACHA UJUMBE MZITO.

Na Allawi Kaboyo – Bukoba. Mtu mmoja mkazi wa Kashai Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera, amekutwa amejinyonga kwa kamba ya katani hadi kufa Nyumbani Kwake kwa kile kinachodaiwa kuwa ni Kutokana na Hali ngumu ya Maisha baada ya kugundulika anaishi na Virusi vya Ukimwi. Marehemu huyo aliyetambulika kwa jina la SALVATORY RWEYEMAMU (47) amegundulika akiwa amefariki katika Chumba chake alichokuwa akiishi katika Nyumba ya Bi. TAUS ALLY (mwenye Nyumba), Mnamo tarehe 6 Januari,2019 Majira ya Saa tatu Asubuhi mara baada ya Kijana wa Kaka ake (jina halikupatikana) alipokwenda kumjulia hali.…

Source

Share:

LUGOLA AMPA SIKU 30 KAMISHA WA JESHI LA ZIMAMOTO NCHINI KUFANYA UKAGUZI TAASISI ZA UMMA KAMA ZINA VIFAA VYA ZIMAMOTO

Na Mwandishi wetu BIHARAMULO Waziri wa mambo ya ndani Kangi Lugola amempa siku 30 kamishna wa jeshi la zimamoto nchini kufanya ukaguzi taasisi mbalimbali za umma na binafsi kuwa na vifaa vya zimamoto hasa katika shule za msingi, sekondari vyuo, vituo vya kutolea huduma za Afya kuepukana na ajali zitokanazo na vyanzo vya moto Lugola ametoa agizo hilo hii leo wilayani Biharamulo mkoani kagera kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa mpira Biharamulo mjini na kwamba iwapo siku hizo zikiisha hajatekeleza atachukuliwa hatua za kisheria. Pia ameagiza wakurugenzi watendaji wa…

Source

Share:

MALINDI WAIPA KICHAPO YANGA...WAIONESHA MLANGO WA KUTOKEA

Mchezo wa kundi B wa kundi la Mapinduzi kati ya Yanga na Malindi umemalizika kwa Malindi kufanikiwa kushinda mabao 2-1 dhidi ya Yanga, katika Uwanja wa Amaan, Visiwan Zanzibar.

Matheo Anthony alikuwa wa kwanza kuandika bao la kuongoza kwa Yanga akiwa ndani ya18 kwa kumalizia kona kwa kisigino.


Dakika ya 41 Malindi walifanikiwa kusawazisha bao kupitia kwa Abdul Swamad Ali akiwa nje ya 18 kwa shuti kali lilomshinda mlinda mlango wa Yanga.

Dakika ya 62 Hamis Musa alimtengea pasi Juma Boluna akafanikiwa kuandika bao la pili la ushindi.

Mashabiki wa Yanga wamekaa jukwaa moja na wale wa Malindi kutokana na utamaduni wa visiwani Zanzibar tofauti na ilivyo Dar es Salaam.

Baada ya kupoteza mchezo wa leo wa kombe la Mapinduzi kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Malindi Yanga wanayaaga mashindano rasmi.

Yanga wanaishia hatua ya makundi ya kombe la Mapinduzi baada ya kupoteza michezo yao miwili kati ya mitatu waliyocheza paka leo baada ya kufungwa na Azam FC kwa mabao 3-0 na leo na Malindi SC kwa mabao 2-1.

Mchezo wao wa mwisho utakuwa dhidi ya Jamhuri ukiwa ni kwa ajili ya kukamilisha ratiba kisha watarejea nyumbani.

Kundi B ambalo wapo kwa sasa vinara ni Azam FC wakiwa sawa na Malindi SC wenye Pointi saba wakifuatiwa na Yanga wenye Pointi tatu huku KVS wakiwa na Pointi moja kwenye kundi B.
Share:

SPIKA NDUGAI AMTAKA CAG KUFIKA MBELE YA KAMATI YA MAADILI KWA HIARI LA SIVYO ATAPELEKWA KWA PINGU

Spika wa Bunge Job Ndugai amemtaka Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Prof. Mussa Assad kufika mbele ya kamati ya maadili ya Bunge Januari 21, 2019 kwa hiyari vinginevyo atapelekwa kwa pingu.


Kwa upande wa Mbunge wa Kawe Halima Mdee ametakiwa kuripoti kamati hiyo Januari 22. Viongozi hao wa umma wanatuhumiwa na Spika Ndugai kulichafua bunge.


Miongoni mwa tuhuma hizo ni ile iliyotolewa hivi karibuni na Profesa Assad alipokuwa akihojiwa na idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa.


Mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa, Arnold Kayanda, alimuuliza CAG kuwa ofisi yake imekuwa ikijitahidi kila mwaka kufanya ukaguzi na kutoa ripoti zenye kuonyesha kuna ubadhirifu lakini baada ya hapo wananchi hawaoni kinachoendelea.


CAG alijibu: "Hilo ni jambo ambalo kimsingi ni kazi ya Bunge. Kama tunatoa ripoti zinazoonyesha kuna ubadhirifu halafu hatua hazichukuliwi, huo kwangu ni udhaifu wa Bunge. Bunge linatakiwa kusimamia na kuhakikisha pale panapoonekana kuna matatizo basi hatua zinachukuliwa.


"Sisi kazi yetu ni kutoa ripoti. Na huu udhaifu nafikiri ni jambo lenye kusikitisha. Lakini ni jambo ambalo muda si mrefu huenda litarekebishika. Ni tatizo kubwa ambalo tunahisi Bunge linashindwa kufanya kazi yake kama inavyotakiwa."

Akiendelea kufafanua jibu lake, CAG Assad alisema: "Sitaki kuwa labda nasema hili kwa sababu linahusisha watu fulani, lakini ninachotaka kusema ni kuwa Bunge likifanya kazi yake vizuri, hata huu udhaifu unaoonekana utapungua."

Mwaka 2018 lilipoibuka suala la upotevu wa Sh1.5 trilioni kwenye hesabu za Serikali mwaka wa fedha 2016-2017, Assad aliulizwa kuhusu nini kifanyike, akataka Bunge liulizwe kwani ndilo lenye kutakiwa kuibana Serikali kuhusu kutoonekana kwa fedha hizo.
Share:

NYAMA YA DHAHABU YAMPONZA KIUNGO WA BAYERN MUNICH FRANK RIBERY

Share:

HATIMAYE TFF YAMREJESHA MWENYEKITI WA YANGA


Makao makuu ya klabu ya Yanga

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia kwa kamati yake ya Rufaa ya Uchaguzi chini ya Mwenyekiti wake, Kenneth Mwenda, imemrejesha mgombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Yono Kevela ambaye alikuwa ameenguliwa.

Hatua hiyo imekuja baada ya kamati hiyo kusikiliza rufaa aliyokata mgombea huyo akilalamikia maamuzi ya kuenguliwa jina lake kwenye majina ya wagombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti, kwa madai kuwa aliomba nafasi mbili, nyingine ya Uenyekiti.

Kevela sasa anaungana na Titus Eliakim Osoro na Salum Magege Chota kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti, wakati wagombea Uenyekiti ni Dk. Jonas Benedict Tiboroha, Mbaraka Hussein Igangula na Erick Ninga.

Wagombea 16 wa nafasi za Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ni Hamad Ally Islam, Benjamin Jackson Mwakasonda, Sylvestre Haule, Salim Seif, Shafil Amri, Said Kambi, Dominick Francis, Seko Jihadhari, Ally Omar Msigwa, Arafat Ally Hajji, Frank Kalokola, Ramadhani Said, Leonard Marango, Bernard Faustin Mabula, Christopher Kashiririka na Athanas Peter Kazige.

Viongozi waliojiuzulu ni aliyekuwa Mwenyekiti Yussuf Manji, Makamu Mwenyekiti, Clement Sanga na Wajumbe wanne, Omary Said Amir, Salum Mkemi, Ayoub Nyenzi na Hashim Abdallah hivyo nafasi zao zitazibwa katika uchaguzi huo wa Januari 13, 2019.
Share:

Picha : BASHIRU AMBEBESHA MAKAMU WA RAIS ZIGO LA MGOGORO WA MKUU WA MKOA NA KATIBU WA CCM SHINYANGA

Katibu mkuu wa CCM,Dkt. Bashiru Ally akizungumza leo Shinyanga - Picha na Kadama Malunde - Malunde1 blog
 **
Katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Dkt. Bashiru Ally amesema atamuomba Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT),Bi. Gaudensia Kabaka kusuluhisha mgogoro kati ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Bi. Zainab Telack na Katibu wa CCM mkoa wa Shinyanga, Bi. Haula Kachwamba.

Dkt. Bashiru amefikia maamuzi hayo leo Jumatatu Januari 7,2019 wakati akiongea na watendaji wa CCM ngazi ya kata,wilaya na mkoa kwenye Ukumbi wa CCM Shinyanga na kueleza kuwa kitendo cha kutunishiana misuli ya kimamlaka baina ya viongozi hao wa chama na serikali Mkoani ni tishio katika kasi ya ujenzi wa mkoa wa Shinyanga. 

Alisema mgogoro huo hauna nafasi katika kipindi hiki ambapo CCM ina mpango mkakati wa kujiimarisha ili kuondoa changamoto za maendeleo zinazowakabili wananchi. 

"Hapa nimeambiwa kuna ka mgogoro kati ya Mkuu wa mkoa na katibu wa CCM mkoa,nimesikitika sana, siyo kawaida,ingawaje watu wanasema wanawake hawapendani,lakini mimi nina ushahidi wanawake ni msingi wa umoja kokote,wanawake huvumilia sana,wanawake ndiyo mfano bora katika jamii...

"Sasa nimeambiwa jambo hilo mwenyekiti limeshamshinda…mwanaume!!…..nasikia hata Waziri Mkuu amekuja hapa limemshinda....mwanaume!!, nasikia hata Makamu wa pili wa rais ambaye ni Mlezi wa mkoa huu,Mjumbe wa kamati kuu ya siasa amesema limemshinda…mwanaume! Sasa mimi sitaki kuliingilia kwa sababu na mimi ni mwanaume ",alisema Dkt. Bashiru.

“Jambo hili namkabidhi Mjumbe wa Kamati kuu na makamu wa Rais mwanamke,na nitamuongezea nguvu,nitamwambia Mama Kabaka,Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake,wakae wajifungie,wanawake wanne,wawili waliotofautiana na wawili nitakaowaomba wawasuluhishe... 

…..mimi nitapokea taarifa na taarifa hiyo nitampelekea Mwanaume Mkuu wetu,Rais Wetu kwa sababu yeye ndiye aliyemteua mkuu wa mkoa,na yeye ndiye aliyeniteua mimi ninayemuajiri katibu wa mkoa,hivyo tutakaa sisi wanaume wawili kumaliza matatizo ya wanawake hawa wawili”,aliongeza Dkt. Bashiru. 

“Na ninaamini wanawake wawili nitakaowaomba na wanaume wawili tutakaolishughulikia kulimaliza,ngoma itakuwa sare sare,sisi hatuishiwi ubunifu kwa kuimarisha umoja na mshikamano katika chama chetu...

…bila mkuu wa mkoa wewe siyo lolote siyo chochote,bila katibu wa mkoa wewe siyo lolote siyo chochote,wewe unasimamia shughuli za serikali ya CCM,wewe unasimamia chama ambacho ndicho kinasimamia serikali ya CCM,mkianza kuyumba mtayumbisha mkoa mzima,nimeshayasikia ya kila upande na sijazungumza nao tangu nimefika,kila mara nilikuwa nakwepa nisimsikie huyu wala huyu.... 

“Kwa sababu ninazo taarifa za kutosha,taarifa hizo ntamkabidhi Makamu wetu wa Rais na Mjumbe wa kamati kuu Mama Kabaka,wakae wawasikilize halafu watatushauri na matarajio yangu ni kwamba jambo hilo litakwisha salama,sasa kwa sababu ni mchakato ninawaomba kuanzia leo,wafanye zoezi dogo tu,washikane mikono mbele yangu na nyie mkishuhudia,muwe mashahidi halafu habari ya ushauri wa hawa akina mama wawili itafuata baadae”,alisema Dkt. Bashiru. 

Katika hatua nyingine,Dkt. Bashiru alisema pia katika mkoa wa Mwanza kuna mgogoro akidai upo mvutano kati ya kundi la Anthony Diallo na Meck Sadick na kusisitiza kuwa hahitaji kuona vurugu bali umoja na mshikamano. 

Dkt. Bashiru aliwakemea viongozi wenye dhamana ya kuunganisha wanachama na wananchi kuhusishwa na upuuzi wa namna yoyote,akidai kuwa hata hisia tu kwa sababu wamebeba dhamana ya kujenga chama,taifa ya umma hivyo hawapaswi kuhusishwa kwa namna yoyote ile na mgogoro wa aina yoyote ile unaomhusu mtu yeyote. 

“Ikianza kuzoeleka tabia hiyo,mamlaka ya Urais na mwenyekiti wetu yatadhoofishwa,ofisi ya katibu mkuu wa chama itadharauliwa na huo utakuwa mwanzo wa kufaranganyika kwa uongozi wa chama na serikali,hizi ni dhamana nzito na sisi dhamana zetu,ni dhamana tulizozibeba kutokana na wananchi”,alisema. 

Na Kadama Malunde – Malunde1 blog
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Bi. Zainab Telack na Katibu wa CCM mkoa wa Shinyanga, Bi. Haula Kachwamba wakikumbatiana baada ya kutakiwa  Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally kushikana mikono ili kumaliza mgogoro wao.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Bi. Zainab Telack na Katibu wa CCM mkoa wa Shinyanga, Bi. Haula Kachwamba wakiendelea kukumbatiana kumaliza tofauti zao.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Bi. Zainab Telack (kushoto)  na Katibu wa CCM mkoa wa Shinyanga, Bi. Haula Kachwamba wakiangaliana baada ya kumaliza kukumbatiana walipotakiwa kushikana mikono.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Bi. Zainab Telack na Katibu wa CCM mkoa wa Shinyanga, Bi. Haula Kachwamba wakionesha hali ya furaha baada kutakiwa kushikana mikono kumaliza tofauti zao.

Wakuu wa wilaya na viongozi mbalimbali wa CCM wakiwa ukumbini.
Wakurugenzi wa halmashauri za wilaya na viongozi mbalimbali wa CCM wakiwa ukumbini.
Mkutano ukiendelea.
Wabunge wakiteta jambo. Wa kwanza kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini,Stephen Masele akifuatiwa na Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Shinyanga Lucy Mayenga,Mbunge wa jimbo la Msalala,Ezekiel Maige na Mbunge wa jimbo la Kahama Mjini,Jumanne Kishimba wa kwanza (kulia).
Mkutano unaendelea.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Bi. Zainab Telack akizungumza ukumbini.
 wa CCM mkoa wa Shinyanga, Bi. Haula Kachwamba akizungumza ukumbini.
Mkutano unaendelea.
Wanachama wa CCM wakiwa ukumbini.
Wanachama wa CCM wakiwa wamesimama wakati wa kufunga mkutano.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Share:

NJAA YAZITESA TIMU ZA LIGI KUU,MATOLA AIBUKA NA KUSEMA KWA MWENENDO HUU SIJUI TIMU GANI ITAFIKA

WAKATI kukiwa hakuna dalili yeyote ya kupatika mdhamini mkuu wa Ligi kuu soko ya Tanzania Bara ambayo inaelekea kumaliza mzunguko wake wa kwanza kocha  wa timu ya Lipuli, Seleman Matola,ameibuka na kutoa ya moyoni huku akionesha kukataa tamaa kwa ligi kuwa nzuri kwenye hatua ya  mzunguko wa pili.Matola ambaye ni mchezaji wa zamani wa wekundu wa msimbazi  amesema kuwa mwenendo wa mzunguko wa pili kwa timu nyingi zinazoshiriki Ligi Kuu zitakuwa na hali mbaya kutokana na ugumu wa uendeshaji wa timu. Matola ambaye alicheza timu ya Simba kwa mafanikio makubwa…

Source

Share:

‘YABAINIKA,MC PILI KUMBE DOMO ZEGE’

‛YABAINIKA, MC PILIPILI NI DOMO ZEGE’ Mchekeshaji maarufu na MC mwenye wasifu wake ulioshiba katika tasnia ya Burudani Tanzania Emmanuel Mathias almaarufu kama MC Pilipili alipiga hatua moja kuelekea kuuaga ukapera rasmi baada ya juzi kumvisha pete ya uchumba mpenzi wake ambaye ni mke mtarajiwa wa mchekeshaji huyo ambaye ameteka soko kwa sasa katika mtindo wake wa vichekesho vya jukwaani maarufu zaidi kama standup comedy. Mchekeshaji huyo ambaye kitaaluma ni mwalimu na aliyewahi kufanyia kazi kituo cha luninga cha Tv1 Tanzania alikamilisha zoezi hilo mbele ya umati wa watu ambao…

Source

Share:

FANYENI UTAFITI WA KUTOSHA ILI KUKOMBOA JIMBO LA IRINGA MJINI -MIZENGO PINDA

Na Francis Godwin Iringa Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa Mizengo Pinda amewataka viongozi CCM mkoa wa Iringa kuendelea kufanya utafiti wa kutosha utakaowezesha kumpata mgombea anayekubalika na wananchi ambae atalirejesha jimbo la Iringa CCM . Pinda ambae pia ni waziri mkuu mstaafu wa serikali ya awamu ya nne ameyasema hayo mkoani Iringa wakati akikutana na makundi tofauti tofauti ya wana CCM likiwemo kundi na wanafunzi wa vyuo vikuu vya Iringa ambao ni wana CCM ,kundi la wazee na viongozi wa CCM mkoa wa Iringa . Amesema…

Source

Share:

MAKOMBORA YA MBUNGE MDEE NA CAG ASSAD YAMVURUGA NDUGAI,

MAKOMBORA yaliotolewa na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Prof. Mussa Assad na Mbunge wa Kawe,Halima Mdee ni kama yamemtikisa Spika wa Bunge Job Ndugai ndivyo unaweza kusema baada ya kuibuka na kuagiza watu hao kufika mbele ya kamati ya maadili ya Bunge Januari 21, 2019 kwa hiyari vinginevyo atapelekwa kwa pingu. Kwa upande wa Mbunge wa Kawe Halima Mdee ametakiwa kuripoti kamati hiyo Januari 22. Viongozi hao wa umma wanatuhumiwa na Spika Ndugai kulichafua bunge. Hatua hiyo ya Spika Ndugai imetokana na tuhuma zilizotolewa hivi karibuni na Profesa…

Source

Share:

ALIYEKUWA MWENYEKITI WA CCM MKOA WA SHINYANGA ARUDI KWA KASI YA AJABU..AFUNGUKA MBELE YA BASHIRU

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Shinyanga Erasto Kwilasa ameanza kuitumikia CCM kwa ari mpya na nguvu mpya ili kukiimarisha chama hicho. 

Kwilasa ambaye hivi karibuni alirudishiwa uanachama baada ya kusimamishwa uanachama wa CCM na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC)akiwa mwenyekiti mkoa wa Shinyanga akidaiwa kukiuka misingi ya Katiba ya chama hicho mwaka 2017 ,amesema yupo tayari kutumwa kufanya jambo lolote kwa maslahi ya CCM. 

Kwilasa ameyasema hayo leo Jumatatu Januari 7,2018 wakati Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally akizungumza na Watendaji wa CCM ngazi ya kata,wilaya na mkoa kwenye Ukumbi wa CCM Shinyanga. 

“Ninawaomba kwa jambo lolote nitumieni na nitatumika kwa maslahi Chama na ninaahidi kwamba tutafanya kazi pamoja na wanachama ili kuleta maendelo ya mkoani Shinyanga”,alisema Kwilasa huku akishangiliwa na wafuasi wa CCM ukumbini. 

“Ninawaombea kwa mwenyezi awape afya njema ili muweze kuchapa kazi na kujenga chama chetu na mimi mbele yenu ninaahidi nitakuwa mwanachama mwaminifu na mwadilifu kwa maslahi ya chama chetu na kukijenga chama na kuimarisha umoja na mshikamano ndani ya chama chetu”,aliongeza. 

“Nawashukuru sana mwenyekiti wa CCM taifa Dkt. John Pombe Magufuli na katibu mkuu Dkt. Bashiru Ally kwa usimamizi wa chama chetu,chama hiki kimeonekana kuwalenga zaidi wanyonge kwani haki zinatendeka hakuna jambo lolote la uonevu linaweza kupita mbele yenu mkaliangalia tu”,alisema Kwilasa. 

Miongoni mwa wenyeviti wa mikoa ambao Machi, 2017 walifukuzwa uanachama kwa kudaiwa kukiuka katiba ya CCM ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu, Mwenyekiti wa Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida, Mwenyekiti wa Mkoa wa Shinyanga, Erasto Kwilasa na Mwenyekiti wa Mkoa wa Mara, Christopher Sanya.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Erasto Kwilasa akishikana mkono na Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally leo Januari 7,2019 katika Ukumbi wa CCM mkoa wa Shinyanga - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally akizungumza na Watendaji wa CCM ngazi ya kata,wilaya na mkoa kwenye ukumbi wa CCM Shinyanga. 
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Erasto Kwilasa akizungumza baada ya kukaribishwa atoe neno na Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally
Erasto Kwilasa akizungumza na kuahidi kuwa mwanachama mwaminifu na mwadilifu wa CCM.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Share:

SERIKALI YA GABON IMEZIMA JARIBIO LA KUPINDUA SERIKALI YA BONGO

Waziri wa mawasiliano nchini Gabon anasema wanajeshi waaminifu kwa serikali ya Rais Ali Bongo wamefanikiwa kuzima jaribio la mapinduzi ya serikali nchini humo.


Bw Guy-Bertrand Mapangou ameambia BBC kwamba wanajeshi wanne waliohusika katika jaribio hilo wamekamatwa na mwingine wa tano anasakwa.

"Hali ni tulivu. Polisi ambao huwa hapo wamerejea na kuchukua udhibiti wa eneo lote la makao makuu ya mashirika ya redio na runinga, kwa hivyo kila kitu kimerejea kawaida," amesema.

"Walikuwa watano. Wanne wamekamatwa na mmoja yupo mafichoni na atakamatwa saa chache zijazo."

Kundi la wanajeshi nchini Gabon lilikuwa limetangaza kwamba limetekeleza mapinduzi ya serikali katika taifa hilo la Afrika Magharibi na kutangaza amri ya kutotoka nje.

Chanzo:Bbc
Share:

DC.KATAMBI AAHIDI KUENDELEZA MAPAMBANO KWA WAVUNJAJI SHERIA DODOMA

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe. Patrobas Katambi, amesema yuko tayari usiku na mchana kupambana na kila aina ya uhalifu na ukiukwaji wa sheria Jijini Dodoma. “ Kwa Dodoma Wahalifu,  wazembe, wabadhirifu, wapiga deal, wala rushwa, wakwepa kodi, wachafuzi na waharibifu wa mazingira pamoja na wavunja haki za binadamu hasa kwa wanyonge hawana nafasi hapa na hatutawavumilia hata sekunde moja. “ Vyombo vyetu vipo imara kulinda mda wote haki za Raia, za Serikali, Taasisi na makundi yote,” amesema DC Katambi. Amesema ni muda wa kuchapa kazi na kujenga nchi kama…

Source

Share:

MGOMBEA UBUNGE UKAWA JIMBO LA KWIMBA AKABIDHI BUSARA TANO KWA KATIBU MKUU CCM

Mgombea ubunge jimbo la Kwimba mkoani Mwanza mwaka 2015 ,Ntiga Julius Otto kupitia Chama Cha Wananchi CUF (UKAWA) amejiunga na Chama Cha Mapinduzi CCM na kupokelewa na Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally.
Otto amejiunga CCM leo Jumatatu Januari 7,2019 wakati wa mkutano wa Katibu huyo wa CCM uliofanyika katika ukumbi wa CCM mkoa wa Shinyanga. 

Akizungumza wakati wa kukabidhi kadi ya CUF na busara tano za kustawisha Chama cha Mapunduzi,Otto alisema ameamua kujiunga CCM kwa sababu ni chama chenye mipango kazi inayotekelezwa kwa vitendo na uaminifu kama mwenye Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli alivyoahidi wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu 2015. 

“Nimeamua kujiunga CCM kwa sababu ya utashi nilionao wa kutumikia wananchi kupitia siasa na kuamini kwamba CCM ndiyo mahali pekee penye ndoto na dira ya utekelezaji wa sera ili kuwaletea maendeleo wananchi”,alisema Otto. 

“Mheshimiwa Katibu Mkuu,naomba kukukabidhi bango langu nililolitumia wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka 2015 nikiwania ubunge jimbo la Kwimba lakini pia naomba kukukabidhi karatasi hii yenye busara tano zinazolenga kukistawisha Chama Cha Mapinduzi”,aliongeza. 

Akiwa katika mkutano huo,Katibu Mkuu wa CCM ,Dkt. Bashiru Ally amepokea wanachama 126 wapya wakiwemo kutoka vyama vya upinzani.
Mgombea ubunge jimbo la Kwimba mkoani Mwanza mwaka 2015 ,Ntiga Julius Otto kupitia Chama Cha Wananchi CUF (UKAWA) akizungumza wakati wa kujiunga CCM leo -Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Katibu mkuu CCM ,Dkt. Bashiru Ally akiwa ameshikilia bango la Mgombea ubunge jimbo la Kwimba mkoani Mwanza mwaka 2015 ,Ntiga Julius Otto kupitia Chama Cha Wananchi CUF (UKAWA).Kulia ni Ntiga Julius Otto akiwa ameshikilia karatasi yenye busara tano za kustawisha Chama Cha Mapinduzi aliyoikabidhi kwa Dkt. Bashiru.
Mgombea ubunge jimbo la Kwimba mkoani Mwanza mwaka 2015 ,Ntiga Julius Otto kupitia Chama Cha Wananchi CUF (UKAWA) akishikana mkono na Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally akimkaribisha CCM.
Mgombea ubunge jimbo la Kwimba mkoani Mwanza mwaka 2015 ,Ntiga Julius Otto kupitia Chama Cha Wananchi CUF (UKAWA) akiwa amekaa na makada wenzake wa CCM katika ukumbi wa CCM mkoa wa Shinyanga.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger