Tuesday, 1 January 2019

MWALIMU ALIYEFUNGIA KABATINI MTOTO WA HOUSEGIRL ATEMBEZEWA KICHAPO

JESHI la Polisi limelazimika kumtia tena mbaroni Anitha Kimaro, ambaye anadaiwa kumfungia kabatini mtoto wa miezi sita.

Hatua hiyo imekuja baada ya wananchi wenye hasira kuvamia nyumbani kwake na kuanza kumtembezea kichapo huku wakipinga hatua ya polisi kumpa dhamana.

Anitha ambaye pia ni mwalimu wa Shule ya Msingi Chadulu mjini Dodoma, anatuhumiwa kumfanyia ukatili mfanyakazi wake wa ndani (jina linahifadhiwa), kwa kumpiga na kumjeruhi, huku akimfungia ndani ya kabati mtoto wake wa miezi sita Mtaa wa Makongoro, Kata ya Kiwanja cha Ndege.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto alisema waliamua kumkamata tena Anitha kutokana na usalama wake uraiani kuwa mdogo.

Alisema awali walimkamata mtuhumiwa huyo, lakini ilibidi wamwachie kwa dhamana ambayo ni haki yake ya msingi.

“Tulimwachia kwa dhamana, lakini jana (juzi) tulilazimika kumkamata tena kutokana na usalama wake kuwa mdogo baada ya wananchi wenye hasira kuvamia nyumbani kwake,” alisema.

Na Ramadhan Hassan  - Mtanzania
Share:

MSANII WA FILAMU AFARIKI DUNIA

Share:

BINTI ASIMULIA ALIVYOISHI MWANAE ALIVYOISHI KABATINI...


Licha ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto kudai kwamba madai ya mtoto wa miezi mitano kufungiwa kabatini sio ya kweli, mama mzazi wa kichanga hicho amesimulia jinsi alivyotumia mbinu kuokoa maisha ya mwanaye kabatini.

Katika tukio hilo ambalo linafanana na lile la mwaka 2014 la Mariamu Said wa Morogoro kumficha mtoto wa marehemu mdogo wake kwenye boksi kwa miaka minne, mama wa mtoto huyo amedai kuwa alikuwa akitakiwa kufanya hivyo na mwajiri wake ambaye ni mwalimu wa shule ya msingi jijini Dodoma.

Akizungumza na Mwananchi jana, mzazi huyo mwenye umri wa miaka 15 alisimulia jinsi alivyolazimika kuvunja sehemu ya nyuma ya kabati ili mwanaye aweze kupata hewa bila mwajiri wake kujua.

Binti huyo na mwanaye ambao wanapatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa Dodoma alisema alivunja mbao katika kabati hilo ili mwanaye apate hewa, wakati mwingine alikuwa akitumia upenyo huo kumnyonyesha kwa siri anapokuwa mwenyewe nyumbani hasa mchana.

“Hakujua kama nilivunja mbao nyepesi nyuma ya kabati lake lakini angejua sijui ingekuwaje maana asingekubali kilichofanyika,” alisema.

Binti huyo alidai kuwa ameishi kwa mwajiri wake zaidi ya mwaka mmoja na nusu baada ya kumchukua kutoka Kijiji cha Kigwe, Bahi. 

“Ila tangu aliponichukua hakuwahi kunilipa mshahara, alikuwa akinipa chakula tu,” alidai. “Mwanzoni aliniambia atakuwa akinilipa Sh30,000 kwa mwezi lakini sijawahi kupewa hata mia. Nilipata ujauzito nikiwa kwake na aliyenipa ni (anamtaja jina), ila tangu nimejifungua huyu mama amekuwa akinipiga.


“Asiponipiga yeye basi nitapigwa na mtoto wake wa kiume. Huyu mtoto wangu sijawahi kumnyonyesha mchana. Alikuwa akimuweka kwenye kabati lake la nguo lakini ikifika saa nane usiku ndipo ananipa nimnyonyeshe halafu asubuhi anamchukua tena.”

Polisi wakana kabati

Wakati mzazi huyo akisema hayo, Kamanda Muroto alisema wanamshikilia mwalimu huyo lakini amekanusha kukifungia kichanga hicho kabatini.


Na Habel Chidawali na Rachel Chibwete mwananchi
Share:

Monday, 31 December 2018

WANAOMILIKI BAABARA ZA AFYA BILA KUFUATA SHERIA KUANGUKIWA NA TAMISEMI

Wamiliki wa Maabara binafsi za Afya wametakiwa kufuata sheria na kanuni za kumiliki Maabara binafsi ikiwemo kulipa ada stahiki za uhakiki wa ubora wa huduma na ukaguzi za kila mwaka na yeyote atakeyekiuka hatua kali za kisheria dhidi yake zitachukuliwa. Akizungumza na waandishi wa Jijini Dar es salaam leo, Mkurugenzi wa Tiba WAMJW na ni Mwenyekiti Bodi ya usajili wa maabara binafsi za Afya (PHLB)Dkt Dorothy Gwajima amesema kuwa wasiofuata sheria na kutoa huduma bubu huku wakiwa karibu na ngazi za serikali za mitaa hivyo bodi itashirikiana na tamisemi kuhakikikisha…

Source

Share:

MWILI WA MWANASIASA MKONGWE NDEJEMBI KUZIKWA KESHO DODOMA

Mwili wa mwanasiasa mkongwe nchini Pancras Ndejembi unatarajia kuzikwa kesho Jumanne Januari Mosi, 2019 katika kitongoji cha Chizomoche kijiji cha Bihawana Jijini Dodoma.

Ndejembi (90) alifariki dunia Jumamosi Desemba 29, 2018 saa 2 asubuhi katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma.

Mweyekiti wa kamati ya mazishi, David Mzuri amesema leo Jumatatu Desemba 31, 2018 kuwa maandalizi yote yamekamilika ikiwemo watoto wa marehemu ambao walikuwa wanasubiriwa kutoka nje ya nchi.

Mzuri amesema mwili wa marehemu ulitarajia kuchukuliwa hospitali leo na kulala nyumbani kwake mtaa wa Uzunguni kata ya Kilimani.

“Kesho saa sita mchana tutapeleka mwili wa mpendwa wetu Kanisa la Mtakatifu Paul wa Msalaba na ibada itafanyika pale kisha msafara utaelekea Chizomoche kwa ajili ya mazishi,” amesema.

Baadhi ya viongozi waliofika nyumbani kwa marehemu ni mawaziri wakuu wastaafu Mizengo Pinda na John Malecela. Viongozi wengine wastaafu ni Balozi Job Lusinde, Joseph Butiku, William Kusila na Hezekia Chibulunje.
Share:

POLISI DODOMA WAKANUSHA MTOTO WA MTOTO KUFUNGIWA KABATINI

Wakati binti wa kazi akieleza jinsi mwanaye mwenye umri wa miezi mitano alivyofungiwa kabatini na mwajiri wake mkoani Dodoma kwa muda wa miezi sita, Jeshi la Polisi mkoani humo limekanusha madai ya mtoto huyo kufungiwa kabatini.

Binti huyo wa miaka 15, jana Desemba 30, 2018 akiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma alidai kufanyiwa ukatili kwa kupigwa na kufanyishwa kazi hadi usiku wa manane na bosi wake anayedaiwa kuwa ni mwalimu na kwamba amekuwa akimwambia amfungie hadi usiku mtoto wake na kila alipovunja masharti alikumbana na kipigo.

Leo Desemba 31, 2018 polisi mkoani Dodoma imekanusha madai ya mtoto huyo kufungiwa kabatini kama inavyodaiwa, lakini wamekiri binti huyo kushambuliwa na mwajiri wake.

Kamanda wa polisi mkoani humo, Gilles Muroto amesema polisi wamefanya upekuzi katika nyumba ya mwajiri wa binti huyo ambaye kitaaluma ni mwalimu, Anitha Kimako na kubaini hakuwa na kabati nyumbani kwake.

"Kesi ya shambulio ipo na ameshambuliwa kweli na ndiyo maana tunamshikilia. Anashikiliwa kutokana na usalama wake kwani kelele za watu ni nyingi, ila hili suala la kuwekwa mtoto kabatini halipo," amesema Muroto.

Amesema uchunguzi wa kina unafanyika na kwamba lazima mwalimu huyo wa Shule ya Msingi Medali afikishwe mahakamani.
Share:

SERIKALI YATOA MAAGIZO KWA WAMILIKI WA VITUO VYA AFYA NA MAABARA BINAFSI

Wamiliki wa maabara na vituo vya afya nchini wametakiwa kutimiza wajibu wao mara moja bila shurti kabla ya Januari 15 2019 kwa kuhakikisha wanakamilisha vigezo vyote vya umiliki maabara hizo kwa kuwa muda wa kutoa elimu umepita na sasa ni muda wa kazi tu.

Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Tiba wa Wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto na Mkurugenzi wa bodi ya usajili wa maabara Dkt. Dorothy Gwajima amesema kuwa hadi kufikia Septemba 2018 bodi ya usimamizi wa maabara binafsi ilitambua jumla ya maabara 641 zinazojitegemea na maabara 719 zilizoshikizwa kwenye vituo vya tiba vya watu binafsi vya ngazi mbalimbali.

Amesema kuwa kutokana na baadhi ya wamiliki wa maabara binafsi hasa zilizoshikizwa kutofuata maadili ya uwajibikaji kisheria kufikia Septemba 20, bodi kupitia ziara yake imebaini kuwa kati ya vituo vya tiba 1731vya watu binafsi vyenye maabara ndani ni maabara 1012 sawa na asilimia 58 pekee ndizo zilizotimiza wajibu wake wa kujiandikisha kwenye bodi ya usimamizi wa maabara binafsi na kutekeleza matakwa ya kisheria.

Amesema kuwa wamiliki ambao hawatatekeleza wajibu wao wa kumiliki maabara hizo watachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo kifungo pamoja na faini au vyote kwa pamoja.

Amewataka wamiliki hao kuhakikisha kuwa kila mmoja awe amekidhi vigezo vyote vya umiliki wa maabara ikiwa ni pamoja na kulipa ada zote stahiki zikiwemo malimbukizo ya nyuma na faini stahiki pamoja na kuwa na risiti halali za malipo hayo. Pia amewataka wamiliki wa maabara hizo kulipa tozo stahiki kila mwaka ili kuwezesha bodi kufanya uhakiki wa kudumu wa huduma zitolewazo katika maabara hizo.

Vilevile amesema kuwa katika kutekeleza hilo watatoa orodha za zahanati katika gazeti la Serikali na zahanati isiyokuwapo kwenye orodha hiyo haitatakiwa kutoa huduma yoyote na watakaokiuka watakutana na mkono wa dola. Gwajima ametoa mwito kwa serikali katika ngazi zote kushirikiana na kutoa taarifa dhidi ya wavunja sheria na kufanikisha kuipeleka mbele sekta hiyo.

Akieleza kuhusiana na faini zitakazotolewa Kaimu Afisa msajili wa bodi ya usimamizi ya maabara binafsi Neema Halliye amesema kuwa kwa mujibu wa sheria watakaokiuka sheria hiyo watapigwa faini ya kulipa kiasi cha shilingi laki mbili au kufungwa miaka miwili au vyote kwa pamoja na bado maboresho ya sheria hiyo yanafanyiwa kazi ili kuweza kutoa kibano zaidi.
Share:

HII NDIYO SABABU YA BASI LA MWENDOKASI KUUNGUA MOTO

Kampuni inayotoa huduma katika mradi wa mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam (UDA-RT) imeeleza chanzo cha ajali iliyoyokea mchana Desemba 25, mwaka huu eneo la Ubungo Maji ilitokana na hitilafu ya mfumo wa umeme.


Taarifa ya Mkurugenzi Mtendaji wa UDART, John Nguya kwa vyombo vya habari imeeleza kuwa basi hilo lenye uwezo wa kubeba abiria 155 ,lilikuwa likitokea Kimara kwenda Gerezani lilishika moto kwenye injini na kuwatia hofu abiria na wananchi wengine.


Alisema kuwa moto huo ulidhibitiwa kwa ushirikiano wa wananchi waliokuwa eneo hilo,Jeshi la Zima Moto na Uokoaji , Jeshi la Polisi na wafanyakazi wa UDART kwa kutumia vifaa vya kuzima moto vilivyomo kwenye magari hayo.


“Tungependa wananchi wafahamu kwamba usalama wa mabasi yote ya UDA -RT umedhibitiwa kwa asilimia 100 kuwa matengenezo take yanafanyika kwa umahiri ,viwango vya kimataifa kwa wasimamizi na watalaam kutoka kampuni ya Xiamen Golden Dragon ya China, Cummings ya Marekani ya kimataifa na Voith ya Ujerumani.


“Ndani ya mabasi hayo eneo la injini vipo vizimia koto vitatu vilivyotengenezwa humor na kuzima moto baada ya koto kuzidi na ndivyo ilivyokuwa wakati wa tukio na pia mabasi makubea kuna vizimia moto vinne vyenye ujazo wa kilogramu tatu katika kila mlango mikubwa ya pande zote mbili kwa akili ya dharura,” alisema Nguya.


Nguya alisema kuwa kwa mujibu wa sheria katika mabasi yote makubwa vipo vizimia moto vine vyenye ujazo wa kilogramu tatu kila kimoja na milango mikubwa pande zorte mbili kwa ajili ya dharura na matumizi ya kawaida.
Share:

AFGHANISTAN YAONGOZA VIFO WANATASNIA YA HABARI 16 WAUAWA 2018

Shirikisho la mashirika ya waandishi wa habari, IFJ imesema kuwa idadi ya waandishi wa habari na wafanyakazi wa tasnia ya habari waliouawa mwaka wa 2018 imepanda na kufika 94. Miongoni mwa hao 84 walikuwa waandishi wa habari, wapiga picha, mafundi mitambo na madereva. Kulingana na ripoti ya shirika hilo, nchi hatari zaidi kwa waandishi wa habari mwaka huu unaomalizika ilikuwa, Afghanistan ambako wafanyakazi 16 wa taaluma ya habari walipoteza maisha, ikifuatiwa na Mexico ambako 11 waliuawa. Nchi zingine ni Yemen, Syria, India, Somalia, Pakistan na Marekani.  

Source

Share:

CCM TABATA YAPIGA MARUFUKU KUTOA TAARIFA ZA CHAMA MITANDAONI

Na Heri Shaban CHAMA cha Mapinduzi CCM Tabata Mtambani kimetoa Elimu na kuwapiga msasa Jumuiya za Chama hicho kwa kuwapa elimu kila kiongozi afahamu majukumu yake. Semina hiyo iliandaliwa na CCM Tabata Mtambani ilifunguliwa Dar es salaam hii leo,na Katibu wa CCM Tabata Haruna Aliphonce ambapo katika ufunguzi alipiga marufuku taarifa za chama cha mapinduzi kujadiliwa mitandaoni badala yake aliwataka wana CCM masuala ya chama yasijadiliwe mitandaoni yafanyike katika vikao halali. Haruna aliwataka wana CCM kutumia vikao vyao vya kanuni na kufuata taratibu za chama cha Mapinduzi waachane na utandawazi…

Source

Share:

SIMBA YAONESHA UTII


Kocha wa Simba Patrick Aussems

Licha ya kukabiliwa na mechi ya klabu bingwa Afrika hatua ya makundi klabu ya Simba, imesema itasafiri siku ya Jumatano ya tarehe 2.01.2019, kuelekea visiwani Zanzibar kwa ajili ya kushiriki mashindano ya kombe la Mapinduzi yanayotarajiwa kuanza hivi karibuni.

Simba imeeleza kuwa inaondoka na kikosi kamili ili kufanya vizuri kwenye mashindano hayo, na pia kuipa mazoezi timu hiyo ambayo inajiwinda na mechi ya kwanza ya kundi D ligi ya Mabingwa barani Afrika dhidi ya JS Saoura ya Algeria.

Mechi dhidi ya JS Saoura inatarajiwa kupigwa Uwanja wa Taifa hapa Jijini Dar es salaam siku ya Jumamosi ya tarehe 12 Januari saa kumi alasiri.

''Iwapo tutafuzu kuingia nusu fainali ya Mapinduzi, kikosi cha pili kitabaki Zanzibar na baadhi ya wachezaji, huku wengine wakirejea Dar es Salaam kuwakabili JS Saoura'', imeeleza taarifa ya Simba.

Aidha Simba wameeleza kuwa kwa kuwa fainali ya Mapinduzi itafanyika Januari 13, na kama watafuzu kuna uwezekano mkubwa wa baadhi ya wachezaji wa kikosi cha kwanza kurejea Zanzibar kucheza fainali hiyo.

Kwenye kombe la Mapinduzi Simba ipo kundi A na timu za Chipukizi, Mlandege, KMKM na Simba.
Share:

Taharuki ! KABURI LAFUKULIWA..SANDA YACHOMWA MOTO


Taharuki katika kitongoji cha Kipondoda wilayani Manyoni mkoani Singida baada ya kaburi moja ambalo linadaiwa kuzikwa mtu siku tano zilizopita na kukutwa limefukuliwa huku sanda ikiwa imechomwa moto upande wa miguuni.

Mwajiri wa marehemu ambaye alishiriki maziko ya ndugu huyo, amesema marehemu Jamal Mkumbo alizikwa Desemba 25, mwaka 2018 kwa kufuata tararibu zote lakini ameshangazwa kukuta kaburi limefukuliwa na sanda kuchomwa moto kutokana nakudaiwa kuwa inawezekana ni imani za kishirikina.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kitongoji hicho bw. Jackson Job amekiri kutokea kwa tukio hilo na wamekemea tabia za aina hiyo.

Matukio ya makaburi kufukuliwa wilayani Manyoni yamekuwa yakitokea mara kwa mara na kudaiwa wanaofanya hivyo wamekuwa wakijihusisha na imani za kishirikina.
Share:

ANUSURIKA KIFO KWA KUCHOMWA MKUKI KISA UGOMVI WA SHAMBA

Na,Naomi Milton Serengeti Mwita Mtatiro(30) mkazi wa Kijiji cha Kwitete wilayani Serengeti amenusurika kufa baada ya kuchomwa mkuki na mtu aitwaye Nkori Mwita mkazi wa Kijiji cha Kwitete chanzo kikielezwa kuwa ni mgogoro uliopo baina yao kuhusu mpaka wa shamba Mtatiro aliyelazwa wodi ya wanaume kitanda namba 2 katika hospital Teule ya Nyerere Ddh anaugulia maumivu huku akiwa na jeraha eneo la kifuani na ubavuni wakati hali yake ikionekana kuwa sio nzuri kwani mpaka sasa hajaweza kuinuka wala kuzungumza Akisimulia chanzo cha tukio mmoja wa majirani aliyemfikisha Hospitalini hapo Chacha…

Source

Share:

UHURU MEDIA GROUP YAWAPA MOTISHA WAFANYAKAZI WAKE WOTE


Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Uhuru Media Group Faustine Sungura akimkabidhi mmoja wa wafanyakazi kutoka Idara ya Utawala,Banga Lucas kiasi cha fedha ikiwa ni sehemu ya motisha iliyotolewa kwa wafanyakazi wote wa kampuni hiyo ikiwa kama sehemu ya kuthamini mchango wao.Picha na Michuzi Jr-MMG.
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Uhuru Media Group ambayo inasimamia vyombo vya habari vya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Faustine Sungura akifafanua jambo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar kuhusu mambo mbalimbali ikiwemo kuwapa motisha wafanyakazi wote wa kampuni hiyo kama sehemu ya kuthamini mchango wao,aidha mbaliya kutoa motisha atatumia nafasi hiyo kufanya uhakiki wa wafanyakazi waliopo kwenye vyombo hivyo na iwapo kutakuwa na wafanyakazi hewa  atawabaini.
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Uhuru Media Group Faustine Sungura akielezea mbele ya Waandishi wa habari leo Ofisini kwake jijini Dar,namna kampuni hiyo inavyojipanga ,amesema kuanzia mwakani wataanza kufanya utafiti  utakaochukua muda wa miezi mitatu na lengo ni kufahamu wasomaji  wao,wasikilizaji wao na watazamaji wao wanataka nini."Pia Februari mwaka 
2019 tutafanya 'uzinduzi laini' wa vyombo vyetu na Aprili 2019 tutafanya uzinduzi rasmi,ambapo ndio tutazungumza malengo na mikakati yetu.",alifafanua Sungura.
***

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MKURUGENZI Mtendaji Mkuu wa Uhuru Media Group ambayo inasimamia vyombo vya habari vya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Faustine Sungura ameamua kuwapa motisha wafanyakazi wote wa kampuni hiyo kama sehemu ya kuthamini mchango wao.

Amesema motisha hiyo inakwenda sambamba na uhakiki wa wafanyakazi wote wa kampuni hiyo huku akielezea namna ambavyo amefurahishwa na utendaji kazi wa wafanyakazi wote na hasa katika kumuunga mkono Rais Dk.John Magufuli ambaye amefanya mambo makubwa kwa mwaka 2018.

Akizungumza leo ofisini kwake Sungura amesema Desemba 28 mwaka huu wa 2018 amekutana na wafanyakazi wote kwa kada mbalimbali na alitumia sehemu hiyo kuelezea mikakati ya kampuni hiyo ambayo imedhamiria kufanya mambo makubwa.

"Tulipokutana na wafanyakazi kuna mambo mengi ambayo tumeyazungumza.Pia nilitumia nafasi hiyo kuwashukuru kwa kumuunga mkono Rais Magufuli kwa kazi nzuri anayofanya. Rais wetu amefanya mambo makubwa kwa mwaka huu yakiwamo ya kuboresha sekta ya anga, miundombinu kwa upanuzi wa barabara na ujenzi wa madaraja, umeme wa mto Rufiji ,ununuzi wa korosho, elimu bure na mambo mengine mengi ambayo yamefanyika.Hivyo wafanyakazi hawa wamekuwa wakiunga mkono kwa vitendo jitihada za Rais,"amefafanua. 

Ameongeza wafanyakazi wa Uhuru Media Group kwa mwaka huu wa 2018 wamefanya kazi kwa bidii, hivyo ameamua kuwapongeza kwa kuwapa motisha kwani kesho ni Januari moja ni vema wakauanza mwaka vizuri."Kila mfanyakazi aliyeajiriwa na wasioajiriwa lakini wanafanya kazi kwenye vyombo vya habari vya chama tutawapa motisha hiyo.Tutafanya kwa walioko Dar es Salaam na wa mikoani," amesisitiza.

Aidha mbali ya kutoa motisha atatumia nafasi hiyo kufanya uhakiki wa wafanyakazi waliopo kwenye vyombo hivyo na iwapo kutakuwa na wafanyakazi hewa atawabaini."Nataka kumuona kila mfanyakazi uso kwa uso .Rais wetu aliamua kufanya uhakiki kwa watumishi wa Serikali ,nami namuunga mkono kwa kufanya uhakiki wa wafanyakazi wetu."amesema Sungura.

Amesema baada ya uhakiki wa majina ,hatua ya pili itakuwa ni uhakiki wa vyeti vyao vya kitaaluma na mwisho wa siku atatoa taarifa lakini ameeleza nia yake ni kuona wote ambao wanalipwa wawe ni wafanyakazi sahihi na wapo kwenye orodha yake.

Kuhusu mipango yao,amesema kuanzia mwakani wataanza kufanya utafiti utakaochukua muda wa miezi mitatu na lengo ni kufahamu wasomaji wao,wasikilizaji wao na watazamaji wao wanataka nini.Pia Februari mwaka 2019 watafanya 'uzinduzi laini' wa vyombo vyao na Aprili 2019 watafanya uzinduzi rasmi na hapo ndio watazungumza malengo na mikakati yao.

Amesema wanao mkakati wa kibiashara wa miaka minne na mkakati wa miaka 10 kwa ajili ya kulishika soko.Pia watajiimarisha kwenye mitandao ya kijamii ili kuhakikisha wanawafikia wasomaji wengi zaidi kwani utafiti unaonesha nusu ya watu wote duniani wanapata habari kutoka mtandaoni"Hivyo ili mambo yaende lazima mtandaoni nako tujiimarishe na mapema mwakani tutaweka nguvu kubwa katika eneo la mtandaoni kwa kuwa na timu maaluma," amesema.

Ametumia nafasi hiyo kuwatakia heri ya mwaka mpya wafanyakazi wote wa Uhuru Media Group huku akiwasisitiza waendelee kufanya kazi kwa bidii na kujituma kama ambavyo wamefanya mwaka 2018.
Share:

Good News : NJIA RAHISI KABISA YA KUPAKUA APP MPYA YA MALUNDE1 BLOG...


https://goo.gl/sKWDNS
Usikubali kupitwa na habari yoyote..Ili uwe wa kwanza kupata habari na matukio yanayojiri Tanzania na dunia kote tafadhali pakua/ Download App  mpya ya Malunde 1 blog  ili tukuhabarishe usiku na mchana.


App hii imeboreshwa kukupa vitu roho inapenda...Pia tutakuwa tunakutumia habari zote moja kwa moja kwenye simu yako.

 Ingia Play store kisha Andika Malunde 1 blog halafu bonyeza  Install



https://goo.gl/sKWDNS

Share:

STAND UNITED KUISHTAKI TFF, BIGIRIMANA KUSAJILIWA ALLIANCE FC


Dr. Ellyson Maeja

Uongozi wa klabu ya Stand United ya mkoani Shinyanga umepanga kulishtaki Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kutokana na hatua yake ya kumruhusu aliyekuwa mchezaji, Bigirimana Blaise, kusajiliwa na timu ya Alliance FC ya Mwanza.

Mwenyekiti wa Stand United, Dk. Ellyson Maeja, alisema klabu yake bado inatambua mchezaji huyo wana mkataba naye, hivyo hatua ya TFF kumwidhinisha Alliance wao wametafsiri kama uonevu.

“Tunasikitishwa na kitendo cha TFF kumruhusu Bigirimana kuitumikia Alliance wakati Stand United tayari imewasilisha malalamiko, nasisitiza kwamba sisi hatujampa barua ya kumruhusu kuondoka.

“Kwa kawaida na jinsi mfumo ulivyo mchezaji haruhusiwi kusajiliwa na timu nyingine, lazima kwanza aandikiwe barua na uongozi wa kule alikokuwa anachezea awali na wenye mamlaka ya kutoa barua ya ruhusa ni kiongozi wa TFF au kiongozi wa timu yake ya kwanza?” alihoji Dk. Maeja.

Bigirimana alikuwa sehemu ya kikosi cha Alliance ambacho kililazimishwa sare ya bao 1-1 na Stand United katika mchezo wa Ligi Kuu uliochezwa Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.

Katika mchezo huo uliopigwa Ijumaa iliyopita, Alliance FC ilikuwa ya kwanza kupata bao la kuongoza dakika ya 24 lililofungwa na Dickson Ambundo kabla ya Musa Hafidh kuisawazishia Stand United dakika ya 89.

Sam Bahari - Shinyanga
Share:

MANARA AWAINGIZA YANGA MTEGONI

Msemaji wa Mabingwa Watetezi, Klabu ya Simba, Haji Manara amehoji Mamlaka ya mapato Tanzania juu utaratibu wa watani zao wa jadi kuhusu kuchangisha kwa ajili ya klabu yao na kuuliza kama utaratibu huo ni sahihi.

Manara amehoji iwapo kama Klabu hiyo inayoongoza msimamo wa ligi kuu soka Tanzania bara kama inalipia kodi katika Mamlaka hiyo huku akisistiza kwamba hata kama ukweli ukiwa mchungu kiasi gani lazima usemwe.

"TRA nakumbuka mlienda katika kanisa la Mchungaji Kakobe kufuatilia ile michango na zile sadaka za waumini, Vipi kwa hawa wanaochangisha kila uchwao? wana mashine za EFD? wanalipia kodi za hizi Rambirambi za kujitakia?", ameandika Manara.

Katika kusisitiza kauli yake, Manara amesema "Nategemea 'soon' (mapema) wahusika watatoa maelekezo sahihi ya huu utamaduni unaotufedhehesha Watanzania na ambao ukiachwa unaweza kusababisha kizungumkuti cha kukokotoa hesabu".
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger