Shule ya Msingi Little Treasures iliyopo Manispaa ya Shinyanga, imefanya mahafali ya kuwaaga wanafunzi wake waliomaliza elimu ya msingi darasa la saba mwaka 2025, pamoja na wanafunzi wa awali Pre Unit wanaotarajiwa kuanza darasa la kwanza mwaka 2026.
Mahafali hayo yamefanyika Septemba 20, 2025 katika viwanja vya shule hiyo na kuhudhuriwa na wazazi, walezi pamoja na wageni mbalimbali, ambapo burudani , maandamano na risala na hotuba zikihusisha pia pongezi kwa wahitimu kwa hatua waliyoifikia.
Aidha, wazazi na wageni wameipongeza Shule ya Little Treasures kwa kuendelea kufanya vizuri kwenye mitihani ya kitaifa, jambo ambalo limeifanya ijulikane kama miongoni mwa shule bora zinazolea wanafunzi katika maadili, maarifa na nidhamu.
Wamesema mafanikio hayo ni kielelezo cha juhudi kubwa zinazofanywa na walimu, uongozi wa shule na ushirikiano wa karibu kutoka kwa wazazi, hali inayowafanya wanafunzi wa shule hiyo kuwa na uhakika wa msingi imara wa kielimu wanapoendelea na safari ya masomo.


































































































0 comments:
Post a Comment