Mkuu wa mkoa wa Kagera Fatma Mwassa(aliyeshikiwa maiki) Akimkabidhi Mwenge wa Uhuru mkuu wa wilaya ya muleba Dkt Abel Nyamahanga kwa ajili ya kuukimbiza Mwenge huo katika wilaya ya Muleba
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Fatuma Mwassa ( aliyeko upande wa Kulia ) akikabidhiwa Mwenge wa Uhuru na mkuu wa mkoa wa Geita .
Na Mariam Kaagenda
Jumla ya Miradi ya Maendeleo 58 yenye thamani ya shilingi bilioni 23.8 itazinduliwa , Kukaguliwa , kutembelewa na kuwekewa mawe ya msingi na Mwenge wa Uhuru katika mkoa wa Kagera ambao umeanza kukimbizwa leo Septemba 7 ambapo mapokezi ya Mwenge huo yamefanyika katika kata ya Nyakabango wilaya ya Muleba ukitokea mkoani Geita.Mkuu wa mkoa wa Kagera Hajjat Fatma Mwassa baada ya kukabidhiwa Mwenge wa Uhuru kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Geita Martine Shigela amesema kuwa kwa mwaka 2024 Mwenge wa Uhuru ulitembelea, kukagua,Kuzindua na kuweka mawe ya msingi kwenye Jumla ya miradi 55 yenye thamani ya shilingi bilioni 53.9Hajjat Mwassa amesema kuwa Mwenge wa Uhuru ukiwa mkoani Kagera utakimbizwa katika halmashauri zote 8 za mkoa huo kwa umbali wa kilometa elfu 1 na 40 na kuishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suruhu Hassan kwa kuwezesha fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo katika Sekta mbalimbali mkoani Kagera kwani miradi hiyo imefanikiwa kutokana na ushirikiano mzuri uliopo baina ya Serikali, Wananchi pamoja na wadau wa maendeleo .Ameongeza kuwa kwa kuzingatia Ujumbe wa mbio za mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2025 usemao Jitokeze kushiriki uchaguzi mkuu kwa amani na utulivu mkoa wa Kagera umetekeleza mikakati mbalimbali ya kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani na utulivu pia umeendelea kuweka utayali kwa kuhamasisha vyama vya siasa pamoja na wananchi wa makundi yote wakiwemo Vijana, Wazee na watu wenye mahitaji maalum kushiriki uchaguzi mkuu utakao fanyika October 2025 ili kutimiza haki yao ya kikatibaNaye kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2025 Ismail Ali Ussi wakati akizindua mradi wa Barabara ya Katembe _Mwaloni yenye urefu wa Kilometa 0.56 kwa kiwango cha Lami amesema kuwa utekelezaji wa miradi hiyo ni kutokana na dhamila na maono ya Rais Samia ya kuhakikisha maendeleo hayo yanafanyika ni kwasababu ya kuendelea kuienzi farsafa ya Mwenge wa Uhuru .Aidha ameongeza kuwa Tanzania inayo Tunu ya Taifa ambayo Mwananchi yoyote akiiona anajua kuwa mahali hapo Tunu inaenda kuweka matumaini , Upendo na heshima katika maeneo hayo kwani ipo miradi ambayo watu walidhani haiwezi kutekelezwa lakini Mwenge wa Uhuru umeizindua na kuweza kuwasaidia wananchi huku akiwaomba wananchi kuitunza miradi hiyo ikiwemo Barabara na kuendelea kuithamini kwa dhati .





.jpg)

0 comments:
Post a Comment