Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (kushoto) akimkabidhi mizinga ya nyuki Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania ya Wilaya ya Misungwi, Bahati Makala (kulia) kwa ajili ya mradi wa ufugaji nyuki alipofanya ziara leo. Wengine ni Katibu wa CCM Wilaya ya Misungwi, Cholage Mohamed (katikati), Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Misungwi, Benson Mihayo (wa tatu kutoka kulia), Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Rahma Emmanuel (wa tatu kutoka kushoto) na viongozi wengine wa UWT Misungwi.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (kushoto) akikabidhi mizinga ya nyuki kwa wanajumuiya ya UWT Misungwi kwa ajili ya kuendeleza mradi wa ufugaji nyuki alipofanya ziara katika Ofisi za UWT Misungwi
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (kushoto) akifurahia baada ya kukabidhi mizinga ya nyuki 50 kwa wanajumuiya ya UWT Misungwi kwa ajili ya kuendeleza mradi wa ufugaji nyuki alipofanya ziara katika Ofisi za UWT Misungwi leo. Wengine ni viongozi wa UWT Misungwi, CCM Misungwi na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (kushoto) akizungumza na wanajumuiya ya UWT Misungwi (hawapo pichani) kuhusu umuhimu wa mradi wa ufugaji nyuki alipofanya ziara katika Ofisi za UWT Misungwi
Baadhi ya wanajumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania wa Wilaya ya Misungwi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (hayupo pichani) akizungumza na wanajumuiya ya UWT Misungwi (hawapo pichani) kuhusu umuhimu wa mradi wa ufugaji nyuki alipofanya ziara katika Ofisi za UWT Misungwi
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Misungwi , Cholage Mohamed Cholage akitoa neno la shukrani baada ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (kulia kwake) kukabidhi mizinga ya nyuki 50 kwa Jumuiya ya Wanawake Tanzania ya Wilaya ya Misungwi katika Ofisi za UWT Misungwi.
………………………………………..
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Mary Masanja amekabidhi mizinga ya nyuki 50 kwa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) ya Wilaya ya Misungwi kwa ajili ya kuendeleza mradi wa ufugaji nyuki.
Akizungumza leo katika Ofisi za UWT Misungwi Mhe. Masanja amesema mizinga hiyo imegharimu kiasi cha shilingi milioni tano.
“Naahidi kuongeza mizinga mingine endapo itaendelea kuleta faida kwa jumuiya” Mhe. Masanja amesisitiza.
Amefafanua kuwa mradi huo wa ufugaji nyuki utasaidia mapato ya jumuiya kutokana na mazao ya nyuki ambayo ni asali, nta na sumu ya nyuki ambayo soko lake ni la uhakika.
Mhe. Masanja amefafanua kuwa kupitia mapato yanayotokana na miradi ya jumuiya, itaiwezesha kujisimamia yenyewe hasa katika kukidhi mahitaji muhimu ya wanajumuiya.
Aidha, amewapongeza viongozi wa UWT Misungwi kwa kusimamia vizuri miradi ambapo wameweza kuzalisha lita 40 za nyuki zenye thamani ya shilingi laki nne kutokana na mizinga ya nyuki mitano ya awali.
Pia, Mhe. Masanja ameahidi kuipatia jumuiya hiyo pikipiki nyingine kwa ajili ya kuendeleza mradi wa pikipiki.
Naye, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Misungwi , Cholage Mohamed Cholage amewataka viongozi wa UWT Misungwi kuwa waaminifu kwenye kusimamia miradi ya jumuiya ili ilete manufaa yalikosudiwa.
Pia, amempongeza na kumshukuru Naibu Waziri Masanja kwa kuwa na moyo wa kuijitolea mizinga 50 kwa jumuiya ya UWT Misungwi.
Naibu Waziri Masanja anaendelea na ziara katika Kanda ya Ziwa ikiwa ni utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku
0 comments:
Post a Comment