Tuesday 16 August 2022

RAILA ODINGA APINGA MATOKEO YA URAIS KENYA

...
Kiongozi wa Muungano wa Azimio nchini Kenya Raila Odinga amepinga matokeo ya uchaguzi uliomtangaza naibu wa rais William Ruto kuwa ndiye rais Mteule.


Raila amesema kwamba hakubaliani na matokeo hayo kwa sababu mwenyekiti wa tume hiyo alikiuka sheria ya tume hiyo kabla ya kumtangaza mshindi


Amesema kwamba makamishna wa tume hiyo hawakukubaliana kuhusu hesabu ya mwisho ya matokeo hayo yaliompatia ushindi William Ruto.


''Takwimu zilizotangazwa na Chebukati ni batili kwa maoni yetu, hakuna mshindi kisheria, aliyetangazwa kihalali wala rais mteule''.


Hata hivyo Raila amewasihi wafuasi wake kujizuia akiongezea kwamba atakwenda mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi huo.


''Jana, demokrasia yetu changa ilikumbwa na msukosuko mkubwa, kwa sababu hiyo, Kenya inakabiliwa na mgogoro mkubwa wa kisheria na kisiasa kutokana na matendo ya Wafula Chebukati''.


''Tunafuatilia njia za kisheria na za amani. Tuna hakika kwamba haki itatendeka. Tunaelewa kuwa ni Bw Chebukati pekee ndiye aliyepata kujumlisha kura za urais. Aliwanyima makamishna wote kupata taarifa hizo'', aliongeza Raila akizungumza na vyombo vya habari jijini Nairobi.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger