Wednesday 31 August 2022

ATUPWA JELA MIAKA 4 KWA KUMCHAPA VIBOKO KARANI WA SENSA

...



Amos Nyang'waji

Kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Amos Nyang'waji (25), mkazi wa Kijiji cha Matui wilayani Kiteto mkoani Manyara, amehukumiwa kwenda jela miaka minne kwa kosa la kumcharaza viboko Karani wa Sensa na kuharibu kishikwambi chake wakati akitekeleza majukumu yake.


Hukumu hiyo imetolewa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wilaya ya Kiteto, na Hakimu Mosi Sasy, ambapo awali akisoma mashtaka hayo, Mwendesha Mashtaka ya Polisi Joseph Kijo, amesema Agosti 25, 2022, katika Kijiji hicho cha Matui wilayani Kiteto mtuhumiwa Amosi Nyang'wali akiwa nyumbani kwa kaka yake alimpiga Karani wa Sensa aliyefahamika kwa jina la Cecilia Paulo.

Alipotakiwa kujitetea mtuhumiwa huyo alisema yeye ana tatizo la akili lililomfanya atende kosa hilo ambapo Hakimu Sasy alisema, kwa kawaida kosa la kwanza la shambulio la mwili anapaswa kwenda jela miaka mitano na kosa la pili la kuharibu mali ni jela miaka saba lakini baada ya kuiomba Mahakama impunguzie adhabu aliamriwa kwenda jela miaka 4 na faini laki 7 na fidia laki 5

Hakimu Sasy amesema adhabu hiyo iwe fundisho kwa wengine wenye tabia ya kukwamisha kazi za serikali na hata kuharibu mali ya serikali ambayo inatumia kodi ya wananchi kuwahudumia.

CHANZO - EATV
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger