Monday, 22 August 2022

ODINGA ATUA MAHAKAMA KUU KUPINGA URAIS WA RUTO

...
Mahakama Kuu ya nchini Kenya
Raila Odinga
**

RAILA Odinga aliyekuwa mgombea katika nafasi ya Urais Kenya ameahidi leo saa nane kupeleka mapingamizi ya kushinda kwa mpinzani wake Rais Mteule wa Kenya William Ruto katika kura zilizopigwa Agosti 19, 2022.


Odinga, mgombea mwenza wake Martha Karua, na kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka jana walisalia na msimamo wakisisitiza kwamba adhma yao katika Mahakama ya upeo itaonyesha ulimwengu jinsi ushindi wao “uliibiwa”.

Wakenya wanasubiri kuona maamuzi yatakayo tolewa na mahakama kuu kama yatafanana na maamuzi ya uchaguzi uliopita, katika hali hiyo Mahakama inatarajia kuweka historia nyingine ya kutoa maamuzi.



Hadi sasa Tume huru ya Uchaguzi nchini Kenya imemtangaza William Samoei Ruto kama Rais Mteule wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Kenya
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger