Mwanamume mkongwe wa miaka 92 anayeaminika kuwa mwanafunzi mzee zaidi nchini Uingereza kufanya mtihani wa GCSE amefaulu mtihani wake wa somo la hesabu darasa la tano – kwa alama ya juu zaidi.
Derek Skipper, kutoka Orwell huko Cambridgeshire, alifanya mtihani baada ya kusoma kupitia Zoom.
Mara ya mwisho alifanya mtihani wa hesabu mwaka wa 1946 alipotumia mfumo wa slaidi, lakini wakati huu alikuwa na kikokotoo na miwani ya kumwezesha kuona vizuri zaidi kwa sababu ya matatizo ya macho.
Alisema alifurahishwa na kupita mtihani huo.
Chanzo - BBC Swahili
0 comments:
Post a Comment