Sunday 1 May 2022

TUCTA WATAKA KIMA CHA CHINI MISHAHARA IWE MILIONI MOJA NA ELFU 1O

...

Hery Mkunda, Katibu Mkuu TUCTA

Katibu Mkuu wa Shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Bw. Hery Mkunda amesema TUCTA imependekeza kiwango cha kima cha chini cha mshahara kwa mwezi kiwe shilingi milioni moja na elfu kumi.

Mkunda ameyasema hayo leo Mei Mosi, 2022 wakati wa hotuba yake kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye ni mgeni rasmi katika sherehe hizo za siku ya wafanyakazi ambayo yamefanyika kitaifa mkoni Dodoma katika uwanja wa Jamhuri.

Mkunda amesema licha ya Rais Samia Suluhu Hassan kuzitekeleza hoja mbalimbali za wafanyakazi ikiwemo punguzo la makato ya kodi, kupandisha madaraja, bado TUCTA inapendekeza kuongezewa mishahara walau shilingi milioni Moja na elfu kumi kama kima cha chini.

"Kauli yako ya 2021 ulisema 'Mimi ni Mama, na Mama ni mlezi', hivyo mama tuna imani na matarajio makubwa juu ya ile ahadi uliyotoa kuhusu kutupandishia mishahara wafanyakazi wote Tanzania, mishahara walau iwe shilingi milioni Moja na elfu kumi kama kima cha chini. TUCTA tunapendekeza, bila shaka hotuba yako leo itakuwa tiba sahihi"- Hery Mkunda, Katibu Mkuu - TUCTA.

CHANZO - EATV
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger