Tuesday 31 May 2022

VIJANA 200 WAPATIWA MAFUNZO YA KILIMO KIDIJITALI

...

Wadau mbalimbali wa Westerwelle Startup Haus Arusha wakijadili jambo wiki iliyopita kwenye uzinduzi wa kituo hicho Jijini Arusha, (picha na Queen Lema).

Na Queen Lema, Arusha.

Westerwelle Foundation kutoka Ujerumani imeungana na Obuntu Hub kutoka Tanzania kufungua kituo kipya kwa ajili ya kuwainua vijana wajasiriamali (Innovation Hub).


Mbali na kufungua kituo hicho Jijini Arusha, pia mpaka sasa vijana zaidi ya 200 wameshanufaika na mafunzo kwenye kituo hicho.


Akiongea mwishoni mwa wiki na waandishi wa habari mara baada ya kufungua kituo hicho, Meneja mkuu wa Westerwelle Startup Haus Arusha Bw. Collins Kimaro amesema kuwa uwepo wa kituo hicho ni msaada mkubwa sana kwa vijana


Kimaro amesema kuwa vijana hao 200 walipatiwa ujuzi wa kidigitali kutoka katika sekta ya kilimo.


Kimaro amesema kuwa vijana hao kutoka Arusha na Iringa walipewa ujuzi wa kidigitali.


"Ni fursa kubwa sasa kwa vijana kunufaika na kituo hiki maana hata hao vijana 200 ambao tumewafikia toka mwezi Juni tayari matokeo yameshaonekana kwaiyo tuseme kuwa kila kijana mjasiriamali sasa atumie kituo hiki" ameongeza


Akiongea kituo hicho amesema kuwa ni muungano wa Obuntu Hub na Westerwelle Foundation,ambapo sasa kwa umoja huo wamefungua Westerwelle Startup Haus Arusha(WSHA) ambapo kituo hicho kitatoa nafasi za kisasa za kufanyia kazi yaani co working space,


Ameongeza kuwa programu ya mafunzo mbalimbali na kuwakutanisha wajasiriamali wa kitanzania na mtandao kimataifa.


Kimaro amebainisha kuwa anawashukuru wafadhili mbalimbali ambao wamejitolea kuwasaidia vijana ambapo mpaka sasa matunda yameshaonekana


Akahitimisha kwa kusema kuwa kwa sasa vijana wanakabiliwa na changamoto Kama vile ukosefu wa mitaji,na masoko lakini sasa wanatakiwa kujiunga na kituo hicho,lakini pia wanatakiwa kuchangamkia fursa pamoja na mashindano ya kimataifa ambayo yanatangazwa.


Naye mkurugenzi wa Westerwelle foundation Bw Oliver Reisner amesema kuwa wamefurahi sana kufika Tanzania na wameona muamko wa vijana na wataungana na jitiada za Serikali ya Tanzania kuchochea maendeleo kupitia ubunifu na ujasiriamali.


George Akilimali ni mmoja wa wanufaika, amesema kuwa umoja huo umekuwa msaada kwa vijana wengi sana hapa nchini ambapo kwa yeye aliweza kupata msaada mbalimbali ikiwemo elimu,na mtaji


Amedai kuwa hapo awali hakuwa na uwezo wa kupata masoko ya kimataifa ila kwa sasa amekutanishwa na wadau wa kimataifa hivyo vijana wanatakiwa kutumia kituo hicho.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger