Tuesday, 30 November 2021

DC KIBAHA AIPONGEZA TBS KUTOA MAFUNZO KWA WAJASIRIAMALI WA MAZIWA KATIKA MKOA WA PWANI

...
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mhe. Sara Msafiri akifungua mafunzo kwa wajasiriamali wasindikaji, wasambazaji na wauzaji wa maziwa na bidhaa za maziwa wilayani Kibaha Mkoani Pwani. 

Mkuu wa wilaya ya Kibaha Mhe Sara Msafiri (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo kwa wadau wa maziwa na bidhaa za maziwa. 

Baadhi ya washiriki wa mafunzo kwa wadau wa maziwa na bidhaa za maziwa wilayani kibaha wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo. 

*************** 

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wametoa mafunzo ya Udhibiti ubora kwa wajasiriamali ambao niwasindikaji, wasambazaji na wauzaji wa maziwa na bidhaa za maziwa mkoani Pwani. 

Akizungumza na washiriki wakati wa hafla ya ufunguzi wa mafunzo hayo Mkuu wa wilaya ya Kibaha Mhe. Sarah Msafiri alisema amefurahishwa sana na uamuzi wa TBS kuamua kutoa mafunzo kwa wadau wa maziwa na bidhaa za maziwa na kuichagua wilaya ya Kibaha kuwa sehemu ya kwanza kabisa kupokea mafunzo hayo na nimatarajio yake kuwa wadau hawa watatumia vizuri fursa hii ya mafunzo ambayo itapelekea kuwa na uzalishaji wa maziwa na bidhaa za maziwa zitakazokidhi matakwa ya viwango. 

Alisema anatambua nafasi walionayo wadau wa maziwa na bidhaa za maziwa katika kuchangia uchumi wa taifa hivyo basi kama watakuwa wasikivu katika mafunzo hayo mahususi kwa ajili yao ili kuwajengea uwezo na hatimaye kuwa bidhaa zitakazoweza kuuzwa ndani na nje ya nchi. 

Kwa upande wake Bw. Hamisi S. Mwanasala mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu (TBS) alisema kuwa mafunzo haya yanafanyika katika wilaya Kihaha na Bagamoyo ( Pwani) na Kilosa na Bagamoyo ( Morogoro) na yanatarajia kuwa endelevu kwa Tanzania nzima 

Alifafanua kuwa mafunzo haya yatawanufaisha washiriki kwa kutambua faida na matakwa ya viwango vya maziwa na bidhaa za maziwa, kanuni bora za usindikaji wa maziwa, kanuni bora za afya, teknolojia mbalimbali za usindikaji wa maziwa, utaratibu wa uthibitishaji ubora wa bidhaa, usajili wa majenngo ya kusindikia vyakula na kanuni bora za ufugaji. 

Bw. Mwanasala alisema mafuzo hayo yamejumuisha wakufunzi kutoka taasisi mbalimbali kama vile TBS, SIDO, Bodi ya Maziwa , Afisa Biashara, Afisa Afya na Afisa maendeleo ya jamii. 

Lengo la kutumia wakufunzi kutoka taasisi mbalimbali ni kuhakikisha kuwa mafunzo haya yanaleta tija kwa washiriki kwa kupata elimu juu ya taratibu na kanuni za uzalishaji bora wa maziwa na bidhaa za maziwa.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger