Wednesday 28 October 2020

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Kuanza Kupokea Matokeo ya Urais Leo Usiku

...


 Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dkt. Wilson Mahera amesema kuanzia leo usiku Jumatano Oktoba 28, 2020 tume hiyo itaanza kupokea matokeo ya kura za urais kutoka kwenye majimbo.

Dkt. Mahera ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na Mwananchi Digital kuhusu maandalizi ya kupokea, kujumlisha na kutangaza matokeo ya urais shughuli inayofanyika katika kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC).

“Tutaanza kupokea matokeo kuanzia leo na kuendelea kwa hiyo kesho tutakuwa tuko serious kupokea matokeo kutoka maeneo mbalimbali na kuyatangaza ila matokeo ya udiwani yatatangazwa kwenye kata” Mahera

“Matokeo ya Ubunge yatakuwa yanapokelewa na kutangazwa kwenye jimbo halafu wanatutumia sisi hapa(JNICC) tunayajumlisha na kuyatangaza tena kwamba jimbo fulani tayari matokeo yake yameshatangazwa ” Mahera


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger