Sunday, 25 October 2020

ASKOFU MABUSHI : WASHINDI UCHAGUZI MKUU WASHANGILIE BAADA YA KUTATUA KERO ZA WANANCHI

...

 

Askofu Mabushi akihubiri kanisani hapo

Waumini wa Kanisa la IEAGT Kambi ya Waebrania la Mjini   Shinyanga wakiimba na kumsifu Mungu wakati wa ibada ya Jumapili Oktoba 25, 2020


Na Shinyanga Press Club Blog
Wagombea wanaowania nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano Oktoba 28, 2020 wameaswa kutobweteka baada ya kushinda, bali furaha yao ya ushindi waionyeshe baada ya kutatua kero zinazowakabili Watanzania.

 Wito huo umetolewa na Askofu wa Kanisa la International Evangelical Assemblies of God (IEAGT) la mjini Shinyanga, David Mabushi wakati wa ibada ya kuhitimisha maombi maalum ya kuombea uchaguzi yaliyofanyika kanisa hapo kwa muda siku tatu.

Askofu Mabushi ameshauri kuwa wagombea ili wawe viongozi wa watanzania wanapaswa kutambua kuwa wana jukumu kubwa la kutatua kero za Watanzania kuliko kushangilia.

"Uchaguzi ni njia ya kupata watu wenye uwezo wa kusaidia wengine kumaliza kero zao kwani wanapatikana viongozi watakaokuwa na hatma ya kushughulikia kero za taifa hili.

"Ni vyema sana kwa washindi wa uchaguzi kutoshangilia baada ya matokeo bali wajue wana majukumu makubwa sana ya kusaidia Watanzania.....Mtu anayeshangilia ni kuwa hatambui nini maana ya kuwa kiongozi kwa Watanzania," amesema.

Askofu Mabushi amesisitiza kuwa hata matokeo yatakapo tangazwa kwa wale ambao hawajashinda ni vyema wawe na amani na furaha katika mioyo yao kwani walipaswa kubeba majukumu ya kero za Watanzania..
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger