Wednesday 22 January 2020

Wafanyakazi wanne wa kampuni ya uwindaji ya Green Miles Wakamatwa na Polisi

...
Wafanyakazi wanne wa kampuni ya uwindaji ya Green Miles iliyoondolewa katika kitalu cha Lake Natron(east) wilayani Longido wanashikiliwa na polisi kwa madai ya kukaidi agizo la Serikali  kuondoka wa hiari katika kitalu hicho.

Wafanyakazi hao wamekamatwa na polisi leo Jumatano Januari 22, 2020 waliokuwa wameongozana na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Longodo mkoani Arusha.

Wanatuhumiwa kuendelea na kazi katika kitalu hicho licha ya kutakiwa kuondoka Januari 20, 2020.

Katibu tawala Wilaya ya Longido, Toba Nguvila amesema baada ya wafanyakazi hao kukamatwa, eneo hilo litakuwa chini ya usimamizi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (Tawa) kwa kushirikiana na polisi.

Ofisa wanyamapori wa kikosi cha kuzuia ujangili Mkoa wa Arusha, Emmanuel Pius amewataja wanaoshikiliwa kuwa ni kaimu meneja wa kambi ya Tandala, Lazaro Lembrise, Moses Sikange, Mohamed Bembe na  Hassan Mahonza.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger