Watu watatu wanaelezwa kujeruhiwa baada ya gari aina ya Hiace yenye namba za usajili T 836 DEB ikitokea Kishapu kwenda Shinyanga Mjini kumgonga mwendesha baiskeli na kutumbukia mtaroni wakati ikikwepa gari aina ya Toyota Harrier yenye namba za usajili T726 DFM.
Ajali hiyo imetokea majira ya saa 12 jioni leo Alhamis Januari 2,2019 katika eneo la Pepsi ‘Ushirika’ barabara ya Shinyanga – Mwanza.
Kwa Mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo wameiambia Malunde 1 blog kuwa dereva wa Hiace akitokea Kishapu alikuwa anajaribu kumkwepa dereva wa gari aina ya Toyota Harrier aliyeingia kwenye njia isiyo yake ndipo Hiace ikamgonga mwendesha baiskeli ambaye ni miongoni mwa waliojeruhiwa wakiwemo wale waliokuwa ndani ya Hiace na wamekimbizwa katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga.
Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga likiongozwa na Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Shinyanga (RTO) Anthony Gwandu wamefika eneo la tukio na tayari gari aina ya Harrier inashikiliwa katika kituo cha polisi.
Taarifa kamili tutawaletea hivi punde.
Gari aina ya Hiace yenye namba za usajili T 836 DEB ikiwa kwenye mtaro baada ya ajali - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Gari aina ya Hiace yenye namba za usajili T 836 DEB na baiskeli eneo la ajali
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blo
0 comments:
Post a Comment