Thursday 2 January 2020

Biteko Akamata Kiwanda Bubu Cha Uchenjuaji Dhahabu Shinyanga.

...
SALVATORY NTANDU
Licha ya serikali kuboresha sekta ya madini kwa wafanyabiashara wadogo wa madini wilayani Kahama mkoani Shinyanga imebainika kuwa wapo ambao wamekuwa wakifanya shughuli za uchenjuaji wa madini ya dhahabu ikiwemo kuanzisha viwanda bubu na kuikosesha  serikali mapato.

Hayo yalibainishwa Januari Mosi mwaka 2020 Waziri wa Madini Dotto Biteko katika ziara yake ya siku mmoja ya kushitukiza katika kijiji cha Bunango katika Halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga baada ya kubaini kiwanda bubu cha kuchenjua dhahabu kilichopo katikati ya makazi ya watu.

“Kiwanda hiki kipo hapa katika nyumba hii tangu mwezi julai mwaka 2019 huku kikiendelea kufanya kazi,serikali imepoteza mapato  mengi tutachukua hatua kali za kisheria kwa miliki wa mtambo huu na nyumba hii”alisema Biteko.

Sambamba na hilo  Biteko aliwaka viongozi wa vijiji na Mitaa wilayani humo kuhakikisha wanawafichua wafanyabiashara wanaojihusisha na biashara haramu ya madini ambazo zinafanyika katika makazi ya watu ambao hawana vibali wanaoikosesha serikali mapato.

“Niwaagize viongozi wa mkoa wa Shinyanga kuthibiti vitendo vya biashara haramu ya madini ambavyo vinaendelea kushamiri katika maeneo mbalimbali kwani mpaka sasa tumeshakamata viwanda bubu viwili vya uchenjuaji wa dhahabu ili kutokomeza vitendo hivyi alisema Biteko.

Hata hivyo  Biteko aliagiza kukamatwa na kuhojiwa kwa Ofisa mtendaji wa kijiji cha Bunango Kajanja Kajanja na Mke wa mwenye nyumba iliyobainika kuwa na mtambo wa kuchenjulia dhahabu aliyefahamika kwa jina mmoja la Shule kuhusiana na kuhusishwa na tukioa hilo.

Masoud Bakari Balozi wa kitongoji cha mnara wa voda alisema alishatoa taarifa kwa mamlaka za kisheria  kuhusiana na uwepo wa kiwanda hicho katika eneo lake lakini hakuona hatua zozote zikichukuliwa kwa wahusika.

“Kiwanda hiki kipo katika nyumba hii tangu julai mwaka jana kuna vijana wageni wanne ambao walikuwa wakifanyashughuli ya kuchenjua dhahabu hapa viongozi wote wa eneo hili wanajua tumelalamika sana kuhusiana kumwagwa ovyo kwa maji yenye kemikali kwenye makazi yetu”alisema Bakari.

Katika ziara hiyo mifuko zaidi ya 35 imekamatwa ikiwa na Cabon zinadhaniwa kuwa na madini ya dhahabu katika kiwanda hicho huku mashine hiyo yenye uwezo wa kubeba kilo 500 za Cabon ikiwa tayari imewekewa mzigo kwaajili ya kuanza kazi.

Mwisho.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger