Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ameliagiza Baraza la Uuguzi na Ukunga kumsimamisha kazi muuguzi anayetuhumiwa kumbaka mama mjamzito katika kituo cha Afya Mamba kilichopo Kijiji cha Mamba Mkoani Katavi.
Waziri Ummy ameyasema hayo leo wakati akiongea na Wananchi katika viwanja vya shule ya msingi Majalila Wilaya ya Mpanda, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya na uboreshaji wa miundombinu ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi.
"Naliagiza baraza la wauguzi na ukunga kusimamisha leseni ya muuguzi huyu wakati uchunguzi unafanyika, "Amesema Waziri Ummy.
Aidha,amewataka watumishi wote wa afya nchini kufanya kazi kwa kuzingatia maadili, weledi na viapo vya kazi zao.
0 comments:
Post a Comment