Friday 21 October 2016

TCU: OPENING OF THE FOURTH ROUND OF APPLICATIONS THROUGH CAS

...

Image

PUBLIC NOTICE

Tume ya vyuo Vikuu (TCU) inautangazia Umma kuwa baada ya kukamilisha mchakato wa maombi ya waombaji wa vyuo vikuu, vyuo Vikuu Vishiriki na Taasisi za elimu ya juu kwa awamu ya kwanza, ya Pili na ya tatu, na matokeo ya waombaji wote waliofanikiwa kupata nafasi vyuoni kukamilika, Tume ya vyuo Vikuu imebaini kuwa bado kuna waombaji takribani 5,301 ambao bado wako kwenye mfumo na hawajakamilisha maombi yao.


Tume imebaini pia kuwepo kwa idadi kubwa ya waombaji hasa wenye Stashahada ambao hawakuomba kabisa kutokana na matokeo yao ya mitihani kuchelewa kufika Baraza za Vyuo Ufundi (NACTE)

Awamu hii itawahusu:

       Waombaji ambao bado wako ndani ya mfumo ambao hawajapata nafasi

       Waombaji wapya ambao hawakuwahi kuomba awali; na
       Waombaji walio na sifa linganifu ambao hawakukamilisha taratibu za uombaji hapo awali

Kutokana na sababu tajwa hapo juu, tume inautangazia Umma kuwa itafungua Mfumo (CAS) kwa siku tatu tu, kuanzia Jumatatu tarehe 24 hadi Jumatano tarehe 26 Oktoba 2016 ili kuruhusu Makundi tajwa hapo juu kuingia kwenye mfumo kutuma maombi.

Waombaji wa awamu Nne wanasisitgizwa kuzingatia yafuatayo:

       Kuhakikisha wanaomba kozi walizo na sifa stahiki

       Kuhakikisha wanakamilisha maombi yao kiufasaha
       kuhakikisha wanajiridhisha na nafasi zilizopo kwa kuzingatia viwango vyao vya ufaulu.

Aidha Tume inapenda kuujujulisha Umma kwamba kozi zote zosizo onekana kwenye mfumo kwa sasa kuwa zimejaa.

Baada ya tarehe tajwa hapo juu tume itafunga rasmi zoezi la udahili kwa mwaka 2016/17 ili kuruhusu mchakato mingine ya Bodi ya Mikopo na Vyuo kuendelea.



Kaimu Katibu Mtendaji

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania 21/10/2016
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger