Wednesday 19 October 2016

MPYA:WANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA ST.FRANCIS IRAKARA WAANIKA "MADUDU" YA CHUO HICHO HADHARANI,

...
 Image
Habari zenu,leo wanafunzi wa chuo kikuu cha st.francis ifakara wameuandikia uongozi wa maswayetu blog barua,ili tuifikishe mahala husika,naamini kila siku waziri wa elimu lazima usome blog hii,natumaini utaliona hili na kulitolea maamuzi siku si nyingi.


Hii ndio barua yenyewe kuhusu madudu ya chuo hiki kutoka kwa wanafunzi wenyewe
 
 Kwako Maswayetu blog,

"Chuo chetu kwa muda mrefu sasa kimekuwa na matatizo kadhaa ambayo TCU inaonekana kushindwa (wakati fulani) kutolea maamuzi ya mwisho.

Mara baada ya wanafunzi wa mwaka wa tatu kurudishwa hivi karibuni,limezuka jambo lingine ambalo tuliliacha na kuamini kuwa litakuwa limekwisha kabla ya kwenda likizo tukiamini ni wazi kuwa walichotaka kukifanya HAKINA MASHIKO wala misingi ya kisheria.

Jambo lenyewe ni kupandisha ADA huku ikizingatiwa kuwa ST. FTANCIS (SFUCHAS) walifungiwa kutokuchukuwa wanafunzi wapya kwa mwaka 2016/17 kutokana na kukuosa SIFA stahiki na kupewa muda wa kurekebisha dosari hizo kabla ya kufunguliwa tena mlango wa kuweza kudahili na kusajili wanafunzi wapya...
Ada tunayoambiwa tulipe ni Mil. 4.1 (tuition fee),na taarifa ni kuwa mfumo mzima wa ulipaji ada (fee structure) umebadilika (kwa kuongezeka gharama zake).

Usajili kwa wanafunzi wanaendelea ulianza rasmi JUMAMOSI (15/10/2016),na ajabu ni kuwa HATUJASAJILI (wengi wetu-watoto wa hali duni) tukitamani kupewa ufafanuzi wa ni ipi gharama rasmi inayotakiwa katika usajili na hadi sasa uongozi wa juu umeshikilia maamuzi ya kushinikiza katika kusajili kwa ada mpya (ambayo si rasmi na haijapitishwa,wala hakuna  waraka wowote kutoka TCU unaotoa muongozo wa ulipaji wa gharama hizo mpya.

Tumepewa kesh (20/10/2016) na kesho kutwa (21/10/2016) tuwe tumejisajili kilazima (kwa gharama batili,isiyotambulika rasmi).

KWA NINI NIKUANDIKIE WEWE???
Umeonekana kujali maslahi ya jamii kiujumla bila kujali matabaka ya kimapato na kwa kuzingatia taratibu za uandishi (na hivyo blog yako kusomwa na watu wengi sana-nikiwemo mimi).

Lakini pia mimi sina wadhifa wowote katika uongizi wa chuo na wala sijawahi kuwa (na sitarajii kuwa kutokana na changamoto zinazokabili kila atakayekuwa kiongozi wa chuo hiki-hawataki usimamie haki,wanataka utekeleze matakwa yao).

Kwa sasa wamewatangazia na kuwatishia (waliokuwa) viongozi kwa mwaka 2015/16 na KUWAVUA MADARAKA kutokana na ile iliyokuwa hujuma ya kuwafukuza wanafunzi 25 akiwemo Rais wa chuo (jina namuhifadhi).

Waliporudishwa walivuliwa madaraka na kwa sasa chuo kinatajwa na hao 'wakubwa' kuwa HAKINA UONGOZI hivyo kufanya kila jitihada inayofanywa na wanafunzi juu ya sakata hili kuonekana inakwenda KINYUME NA SHERIA NDOGO ZA CHUO (Students' By-Laws).

Tusaidie wahanga sisi kuifikishia jamii na haswa walengwa wetu kakiwa WADAU wa elimu hususani WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI,TUME YA TAIFA YA VYUO VIKUU na wadau wengine wenye lengo zuri na wananchi wasomeshwao kwa kodi zao...TUSAIDIWE KABLA YA KUPIGWA 'PENALTY' ya SH. 100,000 ukishindwa kusajili ndani ya muda uliopangwa,lakini pia kabla hatujatafutiwa sababu za kufukuzwa chuo,ama namna nyingine ya adhabu kwa sababu tu tunajaribu kuitafuta haki.

IKIWA ADA HII MPYA INAYODAIWA,IMEPEWA 'BARAKA' na TCU,pia ombi letu kwa TCU ni kuwa...watusaidie,wapange viwango vipya (wanavyofikri kuvipanga-ikiwa wana mipango hiyo) vitakavyosaidia watanzania wenye hali duni wamudu gharama za masomo na VISIWAATHIRI WALE AMBAO TAYARI WALIINGIA MIKATABA KWA GHARAMA WALIZOAMINI KUWA WANAWEZA KUZIMUDU.

SINA KITU CHOCHOTE CHA KUKUPA 'MASWA YETU' LAIKINI jaribu kuwa sehemu kubwa ya msaada katika hili kama ambavyo umesaidia katika mengine."

TAARIFA ZIWAFIKIE WALENGWA,WATOE TAMKO,NA MAAMUZI YA MWISHO.
AKHSANTE.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger