Tuesday 25 October 2016

HAYA HAPA MAJINA YOTE YA WANAFUNZI FIRST YEARS WALIOPATA MKOPO CHUO KIKUU UDSM 2016/2017

...
 Image result for UDSM.AC.TZ
TAARIFA KWA UMMA

Wizara ya Mikopo Chuo kikuu Dar es salaam inawatangazia wanafunzi wote na kuwapa mrejesho juu ya masuala ya mkopo kwa wanafunzi wanaoendelea na mwaka wa kwanza.


1. WANAOENDELEA NA MASOMO (CONTINOUS STUDENTS)
Kama ilivyokuwa katika taarifa yetu ya awali kwamba majina ya mgawanyo wa fedha kwenye chakula na malazi, ada na vitabu tutayabandika na tayari tumeyabandika tangu jana. Ikumbukwe ya kwamba huo ni mgawanyo wa fedha kwa mwaka mzima 2016/2017 .Lakini kuna majina ya mgawanyo huo hayajaletwa hasa kwa wanafunzi wenye SAPU pamoja na Mitihani maalumu (SPECIAL EXAMS) kwa sababu matokeo yao yalichelewa kufika Bodi ya Mikopo ila pia tunatambua kuwa kuna ambao hawana SAPU na majina yao bado hayajafika; hili tunalifanyia kazi kwa ukaribu sana na tunatarajia majina yao wiki ijayo.]

2. FEDHA ZA KUJIKIMU NA MALAZI 2016/2017 KWA WANAOENDELEA NA MASOMO (CONTINOUS STUDENTS)
Kwa wanafunzi wanaoendelea majina yao ya fedha za kujikimu na malazi (BOOM), tumeshaongea na Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo na tumeafikiana kwambakaratasi zitatufika leo na kama wizara tutalisimaia hili. Rai yetu kama Wizara tunawaomba wanafunzi wote wanaoendelea kufika katika mbao za
matangazo kuangalia majina yao hata kama katika majina ya mgawanyo wa fedha haukuwepo ni muhimu kufika uangalie jina lako.
Kama hautaona jina lako kwenye karatasi hizo za malipo ya chakula na malazi tunatarajia kupata majina hayo wiki ijayo. Kwa  watakaoona majina yao ambayo tunatarajia kuyapokea leo na kuyabandika kesho,
ZOEZI LA USAINISHAJI LITAANZA JUMATATU TAREHE 24/10/2016 saa 3:00 asubuhi mpaka saa 9:00 jioni.
3. MWAKA WA KWANZA
Wizara ya Mikopo na Serikali nzima ya DARUSO (WHITE DARUSO) tumekuwa tukipambana juu ya kuondolewa kwa suala la kukatwa kwa fedha yenu ya chakula na malazi ambayo kwa utaratibu tu inatakiwa iwe sh.8500/= kwa siku na kwa miezi miwili iwe 510,00/= badala ya 19,266 ambayo mlikuwa mmetengewa kwa miezi miwili. Hili lipo wazi na mnalifahamu tumelishughulikia na mchanganuo upo hivi÷
(i) Kiwango ambacho mnacho hivi sasa ni pungufu (deficit) hivyo basi, fedha zenu zitafanyiwa ongezeko (addition) ili kufikia kiwango cha 510,000/=  (laki tano na kumi) kwa miezi miwili na hili tutalisimamia na kupambana nalo kama ilivyokuwa hapo awali kama kauli ya Waziri wa Elimu ilivyosema jana TBC1 alipokutana na viongozi wa DARUSO.
Hivyo basi, karatasi za awali kama ambavyo mliziona majina (949) yalikuwa machache tumeomba leo hii tupate majina mengine ya wanafunzi ambao hawakuwepo kabisa yaani Ndaki za CoHU, UDBS, CoET, CoSF, CoSS, UDSoL,UDSoED, CoNAS na SJMC muda si mrefu tumewasiliana na Bodi ya Mikopo wamesema wanafanya haraka kutuwahishia majina takribani 680 jumla kufikia wanafunzi 1500 kama awamu ya kwanza. Hata hivyo, majina haya bado ni machache kwani hayajafikia lengo ambalo tunakusudia kwa kuzingatia vigezo vilivyopo kwenye muongozo wa Bodi ya Mikopo 2016/2017. Agizo letu kama wizara ni kwamba siku ya kesho zoezi la usainishaji litaendelea kuanzia saa 2:00 asubuh mpaka saa 7:00 mchana. Mnaombwa wote kwenda kuangalia majina yenu siku ya leo pale KAFTERIA "ONE"
MUHIMU
Wanafunzi wote mnatakiwa kusaini karatasi za malipo ya mafunzo kwa vitendo mkiwa na vitambulisho; vitambulisho vya zamani vinatumka ila kwa upande wa
fedha ya malazi na chakula mnatakiwa kutumia vitambulisho vipya.
Imetolewa na Wizara ya Mikopo kupitia Wizara ya Habari, Mawasiliano, Mambo ya Nje na Jumuiya za Wanafunzi.
Kasunzu Eliud A
0658202828
Mahmud Abdul N
0659366125
Makupa Erick C
0655191254


udbs_loans.pdf
Download File



udsm_cass.pdf
Download File



udsm_udsl.pdf
Download File



udsm_cohu.pdf
Download File



udsm_udse.pdf
Download File



coet_loans.pdf
Download File

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger