Licha
ya baadhi ya viongozi wa ngazi za juu wa Chama cha Wananchi (CUF) na wa
Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kutamka kutomtambua Profesa Ibrahim
Lipumba kama mwenyekiti wa CUF, Lipumba ameendelea kufanya shughuli za
chama hicho ambapo jana ameteua wakurugenzi wapya kwa madai ya kujaza
nafasi za wakurugenzi alizotengua teuzi zao juzi.
Miongoni mwa Wakurugenzi aliodai Lipumba kuwateua ni pamoja na;
- Mkurugenzi wa Uchumi na Fedha -Thomas Malima
- Maftaha Nachuma - Mkurugenzi wa Mambo wa Nje CUF
- Zaynab Mndolwa -Mkurugenzi wa Haki za Binadamu
- Jaffari Mneke -Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi.
Hata
hivyo, Lipumba amedai kuwa, aliowateua watakaimu nyadhifa hizo hadi
watakapothibitishwa na Baraza Kuu la Uongozi Taifa la CUF.
Aidha, amedai kuwa Naibu Mkurugenzi wa Mambo ya Nje atamteua kutoka Zanzibar hapo baadae.
Sambamba
na hilo, alisema wakurugenzi na manaibu wakurugenzi aliowateua baada ya
mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika Juni, 21, 2014 wataendelea na
nyadhifa zao huku akitishia kuwa, ikimbidi kufanya mabadiliko ya
wakurugenzi hao hatosita kufanya hivyo.
Katika
hatua nyingine, Lipumba alitoa maagizo kwa Mkurugenzi wa Uchumi na
Fedha CUF ambaye ndiye Katibu wa Bodi ya Wadhamini kuitisha kikao cha
bodi hiyo Oktoba 4,2016 ili ipewe taarifa ya msimamo na ushauri wa
Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi kuhusu mgogoro wa
uongozi kitaifa wa CUF.
Lipumba
alisema kuwa, amefanya teuzi za wakurugenzi hao kwa mujibu wa katiba ya
CUF ya mwaka 1992 toleo la 2014 ibara ya 90 (1) (f) ambayo inasema kuwa
Mwwenyekiti Taifa atateua Wakurugenzi na Manaibu Wakurugenzi kutoka
miongoni mwa wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa au wanachama
jasiri wa chama.
0 comments:
Post a Comment