Tukio hilo lililoacha simanzi katika kitongoji hicho, limehusisha
ndugu watano wa tumbo moja wakiwamo wanafunzi watatu, waliovamiwa usiku
wa manane na watu wasiojulikana na kuanza kucharangwa mapanga.
Baadhi ya wakazi wa kitongoji hicho wamesikitishwa na tukio hilo
ambalo limetokea majira ya saa tisa usiku wa kuamkia Mei 11, huku
wakiiomba serikali kuchukua hatua kali dhidi ya watu watakaobainika
kuhusika na mauaji hayo.
Inadaiwa kuwa watu wawili waliokuwa na mapanga walikwenda katika
nyumba ya wanafamilia hao na kuanza kuwashambulia huku wakianza na
marehemu Donald ambaye alipambana na wauaji hao lakini alizidiwa nguvu
kabla ya kuangushwa chini na kukatwa katwa mapanga, huku mama wa familia
hiyo ambaye naye ameuawa katika tukio hilo akijaribu kufungua mlango wa
chumba walicholala wajukuu na watoto wake, hali iliyowapa mwanya wauaji
hao kuingia ndani ya nyumba hiyo na kuanza kuwashambulia kwa mapanga.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella ambaye pia ni mwenyekiti wa
kamati ya ulinzi na usalama amefika katika eneo la tukio na kusema
kitendo kilichofanywa na wauaji hao hakiwezi kuvumiliwa.
Kwa mujibu wa diwani wa kata ya Sima Makoye Lugata watu waliouwa ni
pamoja na mama mwenye nyumba Augenia Kiwitega, Maria Philipo na Leonard
Thomas ambaye anasoma kidato cha nne katika shule ya sekondari Sima,
wengine ni Leornad Aloys mwanafunzi wa darasa la saba, Mkiwa Philipo wa
darasa la tano katika shule ya msingi Ijinga.
Marehemu wengine wamefahamika kwa jina moja la Samson na Donald
kutoka wilayani Ngara mkoani Kagera ambao walikuwa wanafanya kazi ya
kilimo kwenye familia hiyo.
Katika tukio hilo watoto wawili (majina yamehifadhiwa) wa familia
hiyo wamenusurika kuuawa baada ya kujificha chini ya uvungu wa kitanda.
0 comments:
Post a Comment