Na Ally Daud- Maelezo.
Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) imebakiza Tsh. Trilioni 2.363 ili kufikia lengo waliojiwekea la kukusanya mapato ya trilioni 12.363 katika mwaka wa fedha 2015/16, ambapo hadi sasa imekusanya kiasi cha Tsh. Trilioni 10.
Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) imebakiza Tsh. Trilioni 2.363 ili kufikia lengo waliojiwekea la kukusanya mapato ya trilioni 12.363 katika mwaka wa fedha 2015/16, ambapo hadi sasa imekusanya kiasi cha Tsh. Trilioni 10.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa awamu ya pili ya mpango wa mafunzo kwa wafanyakazi waliopo kwenye fursa ya ajira za taasisi hiyo Kamishina Mkuu wa TRA Bw. Alphayo Kidata alisema taasisi yake imefanikiwa kukusanya kiasi cha sh trilioni 10 katika muda waliojiwekea na kuahidi kumalizia kiasi cha shilingi trilioni 2.363 kabla ya mwaka mpya wa fedha wa Serikali unaoanza mwezi Julai mwaka huu.
“Tumejiwekea
malengo ya kukusanya kiasi cha fedha cha shilingi trilioni 12.363 kwa
mwaka huu wa fedha na tumefanikiwa kukusanya shilingi trilioni 10 mpaka
mda huu ila tunaendelea na kutimiza lengo letu hadi kufikia July mwaka
huu na tutajipanga upya mwaka ujao wa fedha kufikia malengo mapema” alisema Bw. Kidata.
Aidha
Bw. Kidata amesema kuwa kwa mpango huo wa mafunzo ulioanzishwa kwa
kushirikiana na Chuo cha Usimamizi wa Kodi (ITA) ni mafunzo ya mwaka
mmoja yanayoendana na usaili mpya kwa wahitimu ili kufanya Mamlaka hiyo
kuwa na wafanyakazi waadilifu na wachapa kazi ili kupaisha uchumi nchi.
Kwa
upande wake Mkuu wa chuo cha cha Usimamizi wa Kodi (ITA) Prof. Isaya
Jairo alisema kuwa wameamua kuanzisha mpango huo kwa kushirikiana na
Mamlaka ya mapato ili kufundisha wafanyakazi wa TRA maadili na nyenzo
za utendaji kazini pamoja na kuendesha mafunzo ya dini ili kuwafanya
wafanyakazi wawe wacha mungu katika kazi zao.
Aidha
Kaimu Mkurugenzi Rasilimali Watu na Utawala wa TRA Bw. Victor Kimaro
aliwataka wafanyakazi wote wanatakiwa wafanye kazi kwa maadili hususani
upande wa ukusanyaji kodi na Chuo hicho kimewafundisha wafanyakazi hao
kufanya kazi kwa ushindani katika maeneo ya kazi ili kuliletea taifa
maendeleo yaliyokusudiwa.
Kamishina
Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Alphayo Kidata (katikati)
akionesha kitabu cha mtaala mpya wa mafunzo kwa wafanyakazi (TRA)
watakaopata fursa za kusoma katika Chuo cha Usimamizi wa Kodi (ITA),
kulia ni Mkuu wa Chuo hicho Prof. Isaya Jairo na kushoto na kushoto ni
Kaimu Mkurugugenzi Rasilimali Watu na Utawala Bw. Victor Kimaro.
Baadhi
ya washiriki waliohudhuria katika uzinduzi wa awamu ya pili ya mpango
wa mafunzo ya kuhitimu kwa wafanyakazi waliopo kwenye fursa za ajira
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) uliofanyikia jijini Dar es salaam.
Baadhi
ya washiriki wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni Rasmi Kamishina
Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Alphayo Kidata
0 comments:
Post a Comment