SHIRIKA
la Taifa la Hifadhi za Jamii (NSSF) limetakiwa kuingia ubia na kampuni
za madini nchini ili kutengeneza ajira kwa vijana wa Kitanzania ambao
wengi wao wako vijiweni.
Kauli
hiyo ilitolewa juzi na Rais John Magufuli wakati akizindua majengo ya
mifuko ya pensheni ya NSSF na PPF yaliyogharimu zaidi ya Sh bilioni 60
yaliyojengwa jijini hapa.
Rais
Magufuli alisema wakati umefika kwa NSSF kujikita katika biashara ya
kupata faida kwa haraka kama vile ya madini ya tanzanite kwa kuanzisha
viwanda vya kukata madini hayo na kusanifu ili vijana wafundishwe na
hatimaye kuajiriwa katika viwanda hivyo.
Alisema
suala la Tanzania kuwa nchi ya tatu duniani kwa kuuza madini ya
tanzanite wakati madini hayo yanapatikana hapa hapa tu na kuziacha nchi
za India na Kenya zikiongoza, ni suala la kushangaza sana.
Alisema
NSSF sasa inapaswa kujipanga na kuingia katika biashara ya madini
hususan tanzanite kwa kuingia ubia na kampuni kama hiyo ya Signature
inayomilikiwa na mzawa Sailesh Pandit ili ifanye biashara na wanachama
wa mfuko huo wapate faida haraka haraka na kuachana na uwekezaji wa
majengo.
"Siku
nyingine hakuna ubaya hata NSSF mkawa ndio wawekezaji wakubwa wa
Tanzanite mkawa mnanunua Tanzanite kutoka kwa vijana hawa badala ya kuwa
inavushwa mpaka Kenya na kwenda Kenya, badala ya Tanzania kuwa ya
kwanza kuuza Tanzanite duniani inajitokeza India alafu inafata Kenya
"Unajua saa nyingine watu wanatuona Watanzania sijui tukoje, huyu shetani aliyetulaani sisi Watanzania kwanini asife? hata hatuhurumii kidogo? basi kama ni kuswali na kusali tusali sana ili tubadilike, tuthamini mali yetu kwa ajili ya vizazi vyetu." Alisema RAais Magufuli
"Unajua saa nyingine watu wanatuona Watanzania sijui tukoje, huyu shetani aliyetulaani sisi Watanzania kwanini asife? hata hatuhurumii kidogo? basi kama ni kuswali na kusali tusali sana ili tubadilike, tuthamini mali yetu kwa ajili ya vizazi vyetu." Alisema RAais Magufuli
Naye
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Profesa Godius Kahyarara alisema kampuni ya
madini ya Signature iliyopanga katika jengo la mfuko huo la Mafao House
imeajiri vijana zaidi ya 47 wa kuchonga tanzanite na watashirikiana
katika kuanza biashara hiyo.
Profesa
Kahyarara alisema kauli ya Rais ya shirika hilo kujikitaka katika
biashara ya tanzanite kwa kuanzisha viwanda vya kuchonga madini hayo
wataifanyia kazi haraka iwezekanavyo bila ya wasiwasi wowote.
Hata
hivyo, serikali ilishapiga marufuku usafirishaji wa madini ghafi nje ya
nchi na kutaka madini yote kuchongwa nchini na wazawa kuanzisha viwanda
vya kuchonga madini hayo.
0 comments:
Post a Comment