Serikali inakusudia Kuajili wafanyakazi wapya 71,456,
katika mwaka mpya wa fedha 2016/2017 kwa la kujaza nafasi zilizo wazi, huku
wilaya ya mbulu ikitengewa nafasi 466.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utumishi na utawala bora,
Angela Kairuki, aliliambia bunge jana kuwa, maombi ya nafasi za ajira kwa
kawaida hufanyika kwa uwazi kupitia bajeti ya seriksli, ambayo huidhinishwa na
bunge.
Angela alikuwa akijibu swali la Zacharia Isaya (Mbulu-CCM),
Aliyetaka kujua ni lini serikali itajaza nafasi za ajira zilizo wazi katika
maeneo mbalimbali nchini kwa ngazi za wizara, mikoa, wilaya na vijiji.
Alisema ajira hizo hufanywa na baada ya waajiri kuwasilisha
maombi yao serikalini na kidhinishwa kwa kuzingatia ukomo wa bajeti ya
mishahara serikalini.
Waziri alisema kwa halmashauri ya mbulu, katika mwaka wa
fedha unaomalizika, ilitengewa kuajiri watendaji wa vijiji (VEO) Kumi na
watendaji wa kata (WEO) sita.
Hata hivyo, Waziri alisisitiza kwamba pamoja na nafasi
hizo, serikali itajaza nafasi zilizo wazi kila mwaka, kutokana na bajeti
itakavyoruhusu na kuzingatia vipaumbele.
Aidha katika kuzingatia kupanda kwa gharama za maisha,
Waziri alisema serikali imekuwa ikipandisha kima cha chini cha mshahara kulingana
na uwezo wa bajeti, hususani mapato ya ndani.
Kutokana na hatua hiyo, Angela alisema Tanzania ni moja ya
nchi za afrika, ambazo kwa sasa hulipa kima cha chini cha mshahara sawa na
asilimia 80 ya kiwango cha gharama za maisha (Minimum Living Wage).
Waziri huyo alisema, serikali itaendelea kuboresha mishahara ya
watumishi wake wa umma kulingana na uwezo wa Kiuchumi.
Chanzo: Gazeti la Uhuru
0 comments:
Post a Comment