Moja ya ugonjwa hatari duniani na ambao huua watu wengi ni malaria.
Ugonjwa huu huenezwa na mbu. Ili
kujikinga na ugonjwa huu watu wanashauriwa wawe wakihakikisha
wanaharibu maeneo ambapo mbu huzaliana.
Wanashauri wa kufunika matangi ya maji
na beseni za kufulia nguo. Kuharibu vyombo vyote vya kutekea maji
ambavyo havina mifuniko.
Watu wanaelekezwa na wasiache maji
katika vyombo vya kuwekea maua kwani mbu wanaweza kutaga mayai katika
maji ya madimbwi hayo na kuzaliana kisha mbu hao kung’ata watu na kuugua
malaria.
Epuka kuwa nje wakati wadudu wengi wanapoanza kutokea, vyandarua na vitumike.
Epuka kuwa karibu na mifugo mara nyingi kwani unaweza kuambukizwa ugonjwa iwapo utaumwa na wadudu waliowauma mifugo hao.
Washiriki wote wa familia wanapaswa
kutumia vyandarua hasa vilivyotiwa dawa ya kuwafukuza wadudu, weka nyavu
madirishani na uzitengeneze zinapoharibika, ziba nyufa zilizo pembeni
mwa paa la nyumba ambapo wadudu wanaweza kuingia.
Njia hizo za kujikinga zinagharimu kiasi
fulani cha fedha, lakini unaweza kupoteza fedha nyingi sana ikiwa
utalazimika kumpeleka mtoto hospitalini au mtu anayetegemewa katika
familia pale anapougua.
Wazuie wadudu wasijifiche mahali popote
nyumbani mwako. Piga lipu ukutani na kwenye dari na uzibe nyufa na
mashimo. Ikiwa nyumba imeezekwa kwa nyasi funika dari kwa kitambaa cha
kuwazuia wadudu.
Ondoa vitu vilivyorundikana kama vile karatasi, nguo au picha nyingi zilizowekwa ukutani, kwani huko ndiko wadudu hujificha.
Usiwakaribishe kamwe panya na wadudu, tumia dawa za kuwafukuza na za kuwaua, lakini usisahau kufuata maagizo yaliyoonyeshwa.
Tumia mitego ya inzi na vifaa vya
kuwaua, uwe mbunifu; mwanamke mmoja alitumia kitambaa kutengeneza
mifuko, kisha akajaza mchanga katika mfuko huo na akauweka chini ya
mlango ili kuwazuia wadudu wasiingie ndani ya nyumba.
Kuna njia nyingi ya kujikinga na magonjwa mbalimbali hasa yale ya kuambukiza au kuambukizwa.

0 comments:
Post a Comment