WAALIMU BINZA SHULE YA MSINGI, WAKANA KUWAZOMEA WAALIMU
WA SHULE YA MSINGI SHANWA KATIKA WILAYA YA MASWA
Waalimu wa
shule ya Msingi katika Wilaya ya Maswa wamekanusha vikali juu kudaiwa kuwazomea Waalimu wenzao wa shule ya Msingi Shanwa zote
zikiwa katika Mji mdogo wa Maswa
Kwa mujibu
wa Mwalimu mkuu msaidizi Shule ya msingi Binza Bibi Iviri Swai alisema kuwa Ofisi
yake pamoja na Walimu wenzake wamesikitishwa mno na taarifa zilizo andikwa na gazeti
la Tanzainia daima la Feburuari 12,2014 toleo Namba 3357 kuwa si za kweli hata
kidogo jambo hilo halipo shuleni kwake
Mwalimu Swai
katika maelezo yake kwa mwandishi habari hizi alisema kuwa anachofahamu ujio wa
Afisa Elimu msingi kufika katika shuleni yake alikuwa na ujumbe wa kuwaeleza Walimu wa Shule
ya Binza na Shanwa juu ya ujio wa Rais Jakaya Kikwete katika Wilaya Maswa wala
hapakuwa na maelekezo mengine
Aidha alipo
ulizwa mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Shanwa Gilda Gogadi yeye kwa upande wake
alisema amesikitishwa na taarifa hizo zilizo andikwa na gazetii la Tanzania daima kuwa zilikuwa na
lengo la kuwachonganisha kati uongozi wa shule ya msingi Binza na Shule yake ya
Shanwa
“Inawezekana
mwadishi huyu hana madili ya uandishi wa habari na si dhani kama ni Mwandishi
wa habari anaye fahamu wajibu wake huyu ni mzushi na kama ameshindwa kazi ya
uandishi wa habari atafute kazi ingine au akandikie magazeti ya udaku hayo
ndiyo kazi yake umbeya na uzushi tu”alisema Mwalimu Gogadi
“Hata hivyo
pamoja na kuandika habari za uongo na kumchafua Afisa Elimu wetu ambaye
kimsingi bado ni mgeni katika Wilaya Maswa si kwamba ametuchafua sisi hiyo
amewachafua Walimu wote wa Halimashauri ya Maswa na Jamii nzima”alisema Gogadi
Kwa upande
wake Afisa Elimu katika Halimashauri ya Wilaya ya Maswa Mabeyo Bujimu
aliyehamia kutoka Halimashauri ya Kibondo mkoani Kigoma alisema kuwa
kazi yake ni kusimamia taaluma na Waalimu wote wa Shule za Msingi katika
Halimashauri ya Wilaya ya Maswa na Si vingenevyo
Bujimu
alibainisha zaidi kwamba kitendo cha kuandikwa na baadhi ya vyombo vya habari
hususani gazeti la Tanzania Daima ni kitendo cha kutaka kumdalisha na kudalisha
taaluma ya elimu kwa ujumla “sisi
Wataalamu[Walimu]hatuko katika majukwa ya kisiasa kazi yetu ni moja kuelimisha
watoto basi”alisisitiza Bujimu
“ Hivi
mwandishi kwa uelewa wako mimiDEO mzima] nitoe magizo kwa Walimu wa Binza wakazomee Walimu wa Shanwa nimeanza
jana kazi ya ualimu?huyu mwandishi ana
elimu ndogo yupo yupo tu nenda katika shule zote mbili Binza na Shanwa ukweli
utaupata huko”alisema kwa kujiamini Bujimu.
0 comments:
Post a Comment