Wednesday, 12 March 2014

BWAWA LA MAGEREZA MASWA

...


Magugu maji katika lambo la mwantonja Maswa
MAGUGU MAJI YAVAMIA LAMBO LA MWANTONJA MASWA

Na Isaack Mbwaga  Maswa  Machi 11,2014   Mhariri Habari Mwananchi

Mimea aina ya magugu maji yanatishia kufunika kabisa Lambo la maji  la Mwantonja mini Maswa Lambo linalo hudumia vitongoji 10 vinavyo zunguka lambo hilo  maji yake yatumika kwa kiwango kikubwa wakati wa kiangazi shughuli za kibinadmu kama vile umwagiliaji katika bustania,kujengea na kunyweshea Mifugo

Wakiongea na gazeti hili kwa nyakati tofauti lilipo tembelea eneo la Lambo la Mwantonja na kujionea hali halisi jinsi mimea hiyo ilivyo stawi na kufunika karibu eneo lote la Lambo kwa ktishia uhai wa Lambo

Mkazi wa kitongoji cha Unyanyembe  Njile Washa alisema magugumaji hayo yamezidi kuongeka kadiri siku zinavyo songa mbele na suala la kufurika kwa magugumaji  katika Lambo siyo geni  viongozi wa vitongoji karibu vyote vinavyo lizunguka Lambo wanayo taarifa na wanaona lakini hakuna hatua zinazo chukuliwa kuyaondoa magugu hayo

Njile aliongeza kusema kuwa endapo juhudi hazitafanyika kuanzia sasa kuyatoa huenda magugu hayo yakanza kusafiri hadi mto simiyu ambayo maji yake yanasafiri hadi ziwa Victori mkoani Mwanza

Naye Mwenyekiti wa Kitongoji cha Unyanyembe katika mji mdogo wa Maswa Nkuba Shimi alipo ongea na gazeti hili alisema kuwa taarifa za kuwepo kwa magugu maji   katika lambo la Mwantonja  Ofisi ya Idara ya mifugo na Uvuvi wanazo taarifa tatizo ni ukosefu wa nyenzo za kuvunia magugu hayo

Alizitaja nyenzo hizo kuwa ni pamoja rasimali fedha kwa ajili ya kuajiri watu, mitumbwi mitatu na visu vya kutosha ili watu watakao fanya kazi ya kuyaondoa magugumaji  kazi iwe rahisi kwao na bila kuhatarisha maisha yao ama kuzama endapo italetwa mitumbwi mibovu

Aidha uchunguzi  uliofanywa na gazeti hili umebaini katika baadhi ya visima vya maiji na malambo kadhaa ya maji kuwepo kwa mimea hiyo ambo inatishia uhai wa viumbe wengine kama vile samaki

Endapo mamlaka hazita chukua hatua za haraka kulikabili na kuyaondosha magugumaji hayo katika malambo na visima vilivyo vamiwa na mimea aina ya magugu maji  iko hatari ya kukosa maji kabisa kiangazi kwa ajili shughuli za kibinadamu kama vile Kilimo cha mbogamboga,kunyweshea Mifugo na matumizi ya Binadamu

Tatizo la kuoneka na kuota kwa magugu maji kwa mara ya kwanza lilianza kuijitokeza  mwaka 1994 ambapo mimea hiyo ilikuwa inasafishwa na wafanya biashara wa samaki kutoka Mwanza kuja kuuza katika Soko kuu la Nyalikungu katika mji wa Maswa

Masalia ya mimea ya magugu maji ambayo yalikuwa yanatumika kufunika Samaki  kutoka ziwa Victoria baada ya kutua mzigo wa Samaki majani ya magugu hayo  yalikuwa yanatupwa ovyo bila ungalizi karibu na Malambo ama visima vya maji wakati wana fanya usafi wa vyombo vyao vilivyo kuwa vinatumika kusafirishia Samaki

Serikali ya Halimashauri ya Wilaya ya Maswa [Idara ya Mifugo na Uvuvi] inao wajibu wa kuhakikisha juhudi zinafanyika haraka za kuyavuna magugu hayo kabla hajasambaa na kuenea maeneo mengi katika Halimashauri yote ya Wilaya ya Maswa na Wilaya Jirani zinazo pitiwa na mto Simiyu

Kufutia kuwepo kwa Mradi wa LIVEMP II kwa Halimashauri tano za Itilima,Magu,Kwimba,Meatu na Maswa ambapo Halimashauri ya Maswa ina wahamasisha Watu binafsi,Taasisi na Vikundi mbalimbali kuchimba mabwawa ya kufugia Samaki  kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na biashara


 
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger