Friday, 21 March 2014

...

WAALIMU  BINZA SHULE YA MSINGI, WAKANA KUWAZOMEA WAALIMU WA SHULE YA MSINGI SHANWA KATIKA WILAYA YA MASWA

Waalimu wa shule ya Msingi katika Wilaya ya Maswa wamekanusha vikali juu kudaiwa kuwazomea  Waalimu wenzao wa shule ya Msingi Shanwa zote zikiwa katika Mji mdogo wa Maswa

Kwa mujibu wa Mwalimu mkuu msaidizi Shule ya msingi Binza Bibi Iviri Swai alisema kuwa Ofisi yake pamoja na Walimu wenzake wamesikitishwa mno na taarifa zilizo andikwa na gazeti la Tanzainia daima la Feburuari 12,2014 toleo Namba 3357 kuwa si za kweli hata kidogo jambo hilo halipo shuleni kwake

Mwalimu Swai katika maelezo yake kwa mwandishi habari hizi alisema kuwa anachofahamu ujio wa Afisa Elimu msingi kufika katika shuleni yake  alikuwa na ujumbe wa kuwaeleza Walimu wa Shule ya Binza na Shanwa juu ya ujio wa Rais Jakaya Kikwete katika Wilaya Maswa wala hapakuwa na maelekezo mengine

Aidha alipo ulizwa mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Shanwa Gilda Gogadi yeye kwa upande wake alisema amesikitishwa na taarifa hizo zilizo andikwa  na gazetii la Tanzania daima kuwa zilikuwa na lengo la kuwachonganisha kati uongozi wa shule ya msingi Binza na Shule yake ya Shanwa

“Inawezekana mwadishi huyu hana madili ya uandishi wa habari na si dhani kama ni Mwandishi wa habari anaye fahamu wajibu wake huyu ni mzushi na kama ameshindwa kazi ya uandishi wa habari atafute kazi ingine au akandikie magazeti ya udaku hayo ndiyo kazi yake umbeya na uzushi tu”alisema Mwalimu Gogadi

“Hata hivyo pamoja na kuandika habari za uongo na kumchafua Afisa Elimu wetu ambaye kimsingi bado ni mgeni katika Wilaya Maswa si kwamba ametuchafua sisi hiyo amewachafua Walimu wote wa Halimashauri ya Maswa na Jamii nzima”alisema Gogadi

Kwa upande wake Afisa Elimu katika Halimashauri ya Wilaya ya Maswa  Mabeyo Bujimu  aliyehamia kutoka Halimashauri ya Kibondo mkoani Kigoma alisema kuwa kazi yake ni kusimamia taaluma na Waalimu wote wa Shule za Msingi katika Halimashauri ya Wilaya ya Maswa na Si vingenevyo

Bujimu alibainisha zaidi kwamba kitendo cha kuandikwa na baadhi ya vyombo vya habari hususani gazeti la Tanzania Daima ni kitendo cha kutaka kumdalisha na kudalisha  taaluma ya elimu kwa ujumla “sisi Wataalamu[Walimu]hatuko katika majukwa ya kisiasa kazi yetu ni moja kuelimisha watoto basi”alisisitiza Bujimu

“ Hivi mwandishi kwa uelewa wako mimiDEO mzima] nitoe magizo kwa Walimu wa  Binza wakazomee Walimu wa Shanwa nimeanza jana kazi ya ualimu?huyu mwandishi  ana elimu ndogo yupo yupo tu nenda katika shule zote mbili Binza na Shanwa ukweli utaupata huko”alisema kwa kujiamini  Bujimu

Mwandishi wa habari hizi alipo hojiana na baadhi ya Waalimu kutoka Shule ya msingi Binza na Shanwa ambao  majina yao yame[ hifadhiwa] kwa kwa sasa kwa nyakati tofauti walisema wanatarajia kuitisha kikao kwa shule zote mbili [Shanwa na Binza] ili kutoa tamko lao hatua za kuchukua dhidi ya Mwandishi wa habari na na chombo anacho andikia.

                       
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger