CCM
MASWA YAWEKA MSIMAMO KWA WAJUMBE WAKE
KATIKA UTOAJI WA MAONI KATIBA MPYA
Wakati muda
wa Wajumbe wa Mabaraza ya katiba ngazi
ya Wilaya kuanza mchakato wa kutoa maoni kutoka Kata mbalimbali za Wilaya
ya Maswa Chama cha Mapinduzi katika Wilaya
ya Maswa tayari kimeweka msimamo kwa
Wajumbe wanachama wake ambao ni Wajumbe wa Baraza la katiba liloanza kikao chake jana
Wakiongea
kwa nyakati tofauti jana na Mwandishi wa
habari hizi juzi mara baada ya kikao
chao kilicho itishwa kwa lengo kuweka simamo wa chama kwa sharti ya kuto tajwa
majina yao katika vyombo vya habari kwa kuhofia kuchukuliwa hatua za kinidhamu
na Chama
Walisema kitendo cha viongozi wa Chama cha Mapinduzi ngazi ya Wilaya
ya Maswa kuwa wekea msimamo wa chama kwa
madai wasiukosoe ni kuwanyima haki ya
kutoa mawazo yao ya demokrasia ndani na
kuwambia kilichojadiliwa na uongozi wa juu hakuna mtu wa kuzungumza tofauti watakapo
hudhuria kikao cha Baraza la Katiba ngazi ya Wilaya
Kufuatia
hali hiyo Mjumbe mmoja ambaye ni Diwani kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi alisema pamoja na kuhudhuria kikao cha
chama kitendo cha kuwafunga midomo wajumbe katika kikao kwa kuwa lazimisha
wajadili kilicho letwa na chama ngazi Taifa siyo kitendo kizuri kwa kweli kina wanyima fursa watu wengine kutoa mawazo yao ambayo huenda yanaweza
kusaidia kupata Katiba bora
Hata hivyo
alipo uliziwa katibu Mwenezi wa Chama
cha Mapinduzi katika Wilaya Maswa ambaye ni Katibu Mwenezi wa Mkoa wa Simiyu
Jeremiah Mange[Makondeko]kuelezea tuhuma za kuwaziba midomo Wajumbe wa Kikao
cha Chama cha Mapinduzi [CCM]
Kwa upande
wake alikanusha uvumi huo na kudai kuwa kikkao kilendeshwa kwa uhuru na kila
mjumbe aliruhusiwa kutoa maoni yake bila woga ama vitisho”sikiliza
Mwandishi CCM ndiyo inayo ongoza
Serikali na mawazo ya kuandika katiba
mpya ni wazo la Mwenyekiti wetu wa Chama Taifa Jakaya Kikwete kwa nini tuwazuie
Wanachama wetu kuzungumza katika kikao hayo ni majungu”alisema Mange
Mkutano wa Baraza la kutoa maoni ya Rasimu ya
Katiba ya Tanzania umeanza jana kwa kuwa shirikisha Wajumbe Mbalimbali kutoka
katika Kata zas Wilaya ya Maswa
0 comments:
Post a Comment