Thursday, 6 March 2014

MKURUGENZI WILAYA YA MASWA ACHA UBABE

...

MKURUGEZI MTENDAJI WA HALIMASHAURI YA MASWA, AACHE UBABE KWA WANDISHI WA HABARI

Mkurugenzi Mtendaji wa Halimashuri ya Maswa bibi Hilda Lauwo anataka kuongoza Halimashuri ya Maswa kwa ubabe jambo ambalo halita msaidia kwa namna yoyote katika mustakabali wa Halimashauri hiyo iwapo ataendelea kujenga mazingira hasi kwa wandishi wa Habari

Katika hali isiyo ya kawida hivi karibuni alilibeza Gazeti moja linalo tolewa mara moja kwa wiki Jijini mwanza jina la gazeti hilo kwa sasa lina hifadhiwa akidai kuwa kazi yake kuandika umbeya tu na ni balaa

Akionesha kuwa anataka kufanya kazi kwa woga wa kuto kusogelewa na vyombo vya habari na Wandishi wa Habari amejikuta kila mara lugha yake ni ya kibabe na kejeli kana kwamba nafasi aliyo pewa ya Ukurugenzi ni mali binafsi na wala si dhamana ya Umma tena

Aidha baadhi ya matukio alio yaonesha katika siku za hivi karibuni tangu alipo hamia Halimashuri ya Maswa akitokea Halimashuri ya Ludewa MKoa Mpya Wa Njombe

 Ni wakati ilipo kosolewa baadhi ya miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halimashauri ya Maswa kutokana taarifa ya  Afisa Mipango wa Halimashauri ya Maswa Jeremia Kikonge kutokidhi sifa za ujenzi mradi wa maabara shule ya Sekondari ya Kata ya Masela

 Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu Bibi Mwamvua Jilumbi hakuridhishwa kabisa na maelezo ya taarifa hiyo na kuamua kumweleza mkurugenzi mtendaji kina ubaga asimamia kwa karibu miradi hiyo kwa kuwa Serikali na Wafadhili maendeleo wamekuwa wakitoa fedha nyingi za kugharimia miradi hiyo 

Bibi Mwamvua Jilumbi alifanya ziara ya kutembelea Halimashauri ya Maswa miezi mitatu iliopita[Juni,2013 kwa  lengo la kukagua shughuli za maendeleo akiwa ameongozana na Timu ya Wataalamu wa ngazi ya  Mkoa wa Simiyu  Mkurugenzi wa Halimashuri ya Wilaya Maswa akiwa na Wataalaamu wake

Wakati zoezi linaendelea la kukagua mradi wa Jengo la kisasa la upasuaji katika eneo la Hospitali ya Wilaya ya Maswa katika hali isiyo tarajiwa na kiongozi wa umma ambaye ni Mkurugenzi wa Halimashauri ya Maswa Bibi Hilda Lauwo

 Mkurugenzi Mtendaji wa Maswa aliamua kujifunika uso kwa mikono ili asipigwe picha na kamera ya mwandishi wa Habari hizi hiyo ilikuwa wakati akipewa maelezo mafupi na mzabuni juu ya maendeleo ya mradi na changamoto zinazokwamisha kukamilika kwa mradi mzima kwa wakati[ jina la mzabuni limehifadhiwa] kwa sasa

Mkurugenzi huyo akiwa hajiamini na utendaji wake alisikika akisema ninyi andikeni chochote tu hamuni babaishi na uandishi wenu kauli zake hizo inazo ashiria ubabe na kejeli  ni pale aliposikika kwa mara ingine wakati wa kikao cha Sekta ndogo ya zao la Pamba kilichofanyika Mjini Bariadi

 Akisema hawapendi Wandishi wa habari, hawapendi kwa nini? Huyu ni mtumishi wa Umma vyombo vya habari ni rafiki wa maendeleo ya kweli na si vinginevyo anaogopa nini kuumbuka?kuwa karibu nao.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger