Magugu maji
katika lambo la mwantonja Maswa
MAGUGU MAJI YAVAMIA LAMBO LA MWANTONJA MASWA
MAGUGU MAJI YAVAMIA LAMBO LA MWANTONJA MASWA
Na Isaack
Mbwaga Maswa Machi 11,2014
Mhariri Habari Mwananchi
Mimea aina
ya magugu maji yanatishia kufunika kabisa Lambo la maji la Mwantonja mini Maswa Lambo linalo hudumia
vitongoji 10 vinavyo zunguka lambo hilo maji yake yatumika kwa kiwango kikubwa wakati
wa kiangazi shughuli za kibinadmu kama vile umwagiliaji katika
bustania,kujengea na kunyweshea Mifugo
Wakiongea na
gazeti hili kwa nyakati tofauti lilipo tembelea eneo la Lambo la Mwantonja na
kujionea hali halisi jinsi mimea hiyo ilivyo stawi na kufunika karibu eneo lote
la Lambo kwa ktishia uhai wa Lambo
Mkazi wa
kitongoji cha Unyanyembe Njile Washa
alisema magugumaji hayo yamezidi kuongeka kadiri siku zinavyo songa mbele na
suala la kufurika kwa magugumaji katika
Lambo siyo geni viongozi wa vitongoji
karibu vyote vinavyo lizunguka Lambo wanayo taarifa na wanaona lakini hakuna
hatua zinazo chukuliwa kuyaondoa magugu hayo
Njile aliongeza
kusema kuwa endapo juhudi hazitafanyika kuanzia sasa kuyatoa huenda magugu hayo
yakanza kusafiri hadi mto simiyu ambayo maji yake yanasafiri hadi ziwa Victori
mkoani Mwanza
Naye
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Unyanyembe katika mji mdogo wa Maswa Nkuba Shimi
alipo ongea na gazeti hili alisema kuwa taarifa za kuwepo kwa magugu maji katika lambo la Mwantonja Ofisi ya Idara ya mifugo na Uvuvi wanazo
taarifa tatizo ni ukosefu wa nyenzo za kuvunia magugu hayo
Alizitaja
nyenzo hizo kuwa ni pamoja rasimali fedha kwa ajili ya kuajiri watu, mitumbwi
mitatu na visu vya kutosha ili watu watakao fanya kazi ya kuyaondoa magugumaji kazi iwe rahisi kwao na bila kuhatarisha
maisha yao ama kuzama endapo italetwa mitumbwi mibovu
Aidha
uchunguzi uliofanywa na gazeti hili
umebaini katika baadhi ya visima vya maiji na malambo kadhaa ya maji kuwepo kwa
mimea hiyo ambo inatishia uhai wa viumbe wengine kama vile samaki
Endapo
mamlaka hazita chukua hatua za haraka kulikabili na kuyaondosha magugumaji hayo
katika malambo na visima vilivyo vamiwa na mimea aina ya magugu maji iko hatari ya kukosa maji kabisa kiangazi kwa
ajili shughuli za kibinadamu kama vile Kilimo cha mbogamboga,kunyweshea Mifugo
na matumizi ya Binadamu
Tatizo la
kuoneka na kuota kwa magugu maji kwa mara ya kwanza lilianza kuijitokeza mwaka 1994 ambapo mimea hiyo ilikuwa
inasafishwa na wafanya biashara wa samaki kutoka Mwanza kuja kuuza katika Soko
kuu la Nyalikungu katika mji wa Maswa
Masalia ya
mimea ya magugu maji ambayo yalikuwa yanatumika kufunika Samaki kutoka ziwa Victoria baada ya kutua mzigo wa
Samaki majani ya magugu hayo yalikuwa
yanatupwa ovyo bila ungalizi karibu na Malambo ama visima vya maji wakati wana
fanya usafi wa vyombo vyao vilivyo kuwa vinatumika kusafirishia Samaki
Serikali ya
Halimashauri ya Wilaya ya Maswa [Idara ya Mifugo na Uvuvi] inao wajibu wa
kuhakikisha juhudi zinafanyika haraka za kuyavuna magugu hayo kabla hajasambaa
na kuenea maeneo mengi katika Halimashauri yote ya Wilaya ya Maswa na Wilaya
Jirani zinazo pitiwa na mto Simiyu
Kufutia
kuwepo kwa Mradi wa LIVEMP II kwa Halimashauri tano za
Itilima,Magu,Kwimba,Meatu na Maswa ambapo Halimashauri ya Maswa ina wahamasisha
Watu binafsi,Taasisi na Vikundi mbalimbali kuchimba mabwawa ya kufugia
Samaki kwa ajili ya matumizi ya nyumbani
na biashara
0 comments:
Post a Comment