WAKUU WA
SHULE ZA SEKONDARI MASWA” WAFUNDWA”NA AFISA ELIMU SEKONDORI –NTAGAYE
Waalimu wa
shule za Sekondari katika Halimashauri ya Wilaya ya Maswa wameagizwa
kuhakikisha na wanafuatilia kwa ukaribu ufundashaji wa Wanafunzi katika Shule
zao ili kuinua kiwango cha ufaulu Wanafunzi
Kauli hiyo
alitolewa hivi karibuni na Afisa Elimu Sekondari wa Halimashauri ya Wilaya ya
Maswa Paulina Ntagaye wakati alipokuta na
Waalimu Wakuu wa Shule za Sekondari
katika Ukumbi wa Halimashauri ya Maswa kwa lengo la kuwekeana mikakati ya
kuboresha elimu ya Sekondari kwa mwaka 2014
Ntagaye
pamoja na mambo mengine alisema kufuatia tamko la Serikali kuwa na mpango wa
matokeo makubwa sasa[BRN] ni wajibu wa Waalimu wakuu kwa kila shule kusimamia
kwa dhati kazi ya ufundishaji na kila Mwalimu wa Somo ahakikishe anawajibika
kadri anavyoweza ili tupate matokeo makubwa
Hata hivyo
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya kutwa ya Binza Focus Nchiyiki alisema kuwa ili
elimu yapatikane matokeo makubwa sasa ni wajibu wa Serikali kuhakikisha ina
sambaza vitabu vya kianda na ziada vya kutosheleza kwa Wanafunzi sambamba na ujenzi wa maabara kama ilivyo kwa
Shirika la Umeme[TANESCO]wanavyo sambaza umeme vijijini
“Tunaona
karibu kila siku maroli ya nguzo za Umeme na nyaya zinazambazwa katika vijiji
mbalimbali vilivyo pendekezwa kupata nishati ya Umeme lakini Wizara ya Elimu na
mafunzo Wanafunzi wana uhaba wa vitabu hakuna maabara za kutosha pia na Waalimu
ni nwachache katika baadhi ya shule za Sekondari”alisema
Afisa Elimu
wa Sekondari katika Halimashauri ya
Maswa Paulina Ntagaye alizipongeza shule kumi bora zilizo fanya vizuri katika
mtihani wa kidato cha Pili 2013 ambazo
ni Lalago Sekondari,Ipililo Sekondari,Kulimi Sekondari,Senani Sekondari,Mwabayanda
Sekondari, shule zingine ni Nyabubinza,Kadoto Sekondari,Ng’wanza Sekondari na
Salagi
Wakati huo huo Ntagaye hakusita kuwanyoshea
vidole Wakuu wa Shule kumi duni ambazo
matokea yake ni mabaya mtihani wa kidato cha pili kuwa Ofisi yake hata sita kuwa
chukulia hatua kali endepo shule hizo zitaendea kufanya vibaya katika mitihani
yake mbalimbali ya ndani na kitaifa alisema kwa msisitizo Afisa Elimu huyo
Shule ya
Sekondari ya Kata ya Ipililo imeshika na nafasi ya kwanza kwa shule za Serikali
kati ya shule 36 za Serikali ingawa
shule ya Sekondari ya Wazazi ya Lalago imeshika nafasi ya kwanza kati shule 38
za Serikali na binafsi wakati za binafsi ni Ng’wanza Sekondari na Lalago Sekondari
0 comments:
Post a Comment