Tuesday, 3 January 2023

ANAYEDAIWA KUWA MWIZI ANUSURIKA KUUAWA BAADA YA KUDAKWA NA BATA TAMBUKARELI SHINYANGA MJINI

Kijana aliyejulikana kwa jina Musa amenusurika kuuawa kwa kupigwa na wananchi wenye hasira kali katika eneo la Tambukateli kata ya Ndembezi Mjini Shinyanga baada ya kukamatwa na bata anayedaiwa kumuiba katika mtaa huo huku mwenyewe akikiri kufanya matukio ya wizi katika eneo hilo.


Tukio hilo limetokea majira ya sita mchana leo Jumanne Januari 2,2023 ambapo wananchi wenye hasira wamemshambulia kijana huyo kabla ya askari polisi kufika eneo la tukio na kumuokoa kijana huyo.

Wakati hayo yanajiri mkazi wa eneo hilo ambaye hatukufanikiwa kupata jina lake naye anaugulia maumivu baada ya kupewa kichapo wakati akizuiwa asimpige mtuhumiwa huyo wa wizi.


Mtuhumiwa wa wizi akiwa na bata pembeni


Share:

WABUNGE WA UPINZANI WATUPWA JELA KWA KUMPIGA MBUNGE MWENZAO


Wabunge wawili wa upinzani nchini Senegal, wamehukumiwa kifungo cha miezi sita jela na kulipa faini ya franc 100,000 za CFA (euro 150) kila mmoja sambamba na fidia ya faranga za CFA milioni tano (euro 7,625) kwa kumpiga mbunge mwenzao, Amy Ndiaye ndani ya Bunge.


Tukio hilo la ushambuliaji, lilifanyika Desemba mosi, 2022 baada ya Mbunge Massata Samb na Mamadou Niang kumshambulia Ndiaye kutokana na kauli alizotoa dhidi ya Kiongozi wa Muungano Mkuu wa Upinzani wa Party of Unity and Gathering, Moustapha Sy mwanariadha mwenye ushawishi mkubwa nchini Senegal.


Kufuatia shambulio hilo, Amy Ndiaye alilazwa Hospitali na yupo katika hatari ya kupoteza mtoto aliyembeba tumboni, huku wakili wake, Baboucar Cissé akisema wakati wa kesi licha ya kuruhusiwa kutoka hospitalini, lakini bado yupo katika hali ngumu.


Wabunge hao wawili, waliokuwa kizuizini tangu Desemba 15, 2022 walihukumiwa rasmi Desemba 19 na Mahakama ya flagrante delicto ya jijini Dakar na picha zilizozagaa mtandaoni zilionesha zinaonesha Samb na Niang wakimpiga makofi na kumpiga teke la tumbo Bi Ndiaye aliyekuwa mjamzito wakati wa kikao cha Bunge
Share:

MAMA ADAIWA KUWATEKA NA KUWAUA WATOTO WAKE BAFUNI MKESHA WA MWAKA MPYA


Mama wa watoto wawili waliouawa katika Kijiji cha Kerwa eneo la Kikuyu nchini Kenya usiku wa mkesha wa mwaka mpya, amekamatwa.

OCPD wa Kikuyu, Catherine Ringera alisema kuwa uchunguzi uliofanywa unamhusisha mama huyo na vifo vya watoto hao.

 "Kulingana na ile statement zimeandikwa na hata kulingana sisi vile tuliangalia, vidole zote zinaelekezwa kwa mama," alisema Ringera.

 Ringera alisema kuwa watatafuta maagizo ya korti kumzuia mama huyo zaidi ili kukamilisha uchunguzi wa mauaji hayo ya kutisha.

OCPD alisema walipata simu ya mwanamke huyo ambayo ilikuwa na skrini iliyovunjika na ujumbe ambao alimtaka mume wake amlipe madeni yake. 

Ringera aliongeza kuwa wamekusanya sampuli kutoka eneo la tukio ikiwa ni pamoja na vitabu vitakavyosaidia kuwakamata waliohusika katika mauaji hayo. 

Mwanamke huyo atafikishwa kortini leo, Jumanne, Januari 3 akisubiri uchunguzi zaidi wa polisi. 

Baba watoto anasemaje?

 Baba ya watoto hao Paul Gaitho, ambaye ni mchinjaji alisema alipata simu ya kutatanisha kwamba watoto wake wawili walikuwa wametekwa nyara na watu wasiojulikana. 

Alisema kwamba aliacha kazi yake akifuatana na marafiki zake na kukuta watoto wake tayari walikuwa wameuawa na kutupwa bafuni; mmoja akiwa amefungwa kamba ya kiatu, na mwingine ametupwa kwenye ndoo ya maji. 

"Niliambiwa watoto wamekuwa hijacked. Nilitoka na marafiki zangu tukaenda hadi kwa nyumba. Nilikuta kama watoto washauawa," alisema Gaitho.

Mama huyo anaripotiwa kuwa pekee yake na watoto ndani ya nyumba wakati shambulio hilo linalodaiwa kutokea. 

Alikimbia umbali wa kilomita mbili ambapo alimfahamisha jirani yake kwamba alishambuliwa na hakujua waliko watoto wake.

CHANZO - Tuko news
Share:

Monday, 2 January 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE JANUARI 3,2023





Share:

TAARIFA YA JESHI LA ZIMAMOTO NCHINI

Share:

SENYAMULE AONGOZA UPANDAJI MITI BONDE LA MZAKWE


***********************

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule ameongoza zoezi la upandaji miti katika eneo la chanzo cha maji cha bonde la Mzakwe zoezi ambalo ni muendelezo wa kampeni ya upandaji miti ngazi ya Mkoa iliyozinduliwa rasmi Desemba 31 kwa kupanda miti kwenye eneo la chanzo cha maji cha DUWASA kilichopo eneo la Ihumwa vijijini.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo Mhe. Senyamule amewataka wasimamizi wa Bonde la Wawi-Ruvu, wadau wa mazingira na wananchi kulipa bonde hilo usimamizi madhubutu bila kusukumwa kwani kila mmoja anapaswa kutambua wajibu wake juu ya kulilinda eneo hilo la hifadhi kutokana na umuhimu wake.

“Tuna imani kuwa utafiti wa kutosha ulikwishafanyika hapa hivyo tutaona miti itakayopandwa ikikua kwani hauwezi kupanda miti eneo ambalo halijafanyiwa utafiti wowote ni matumaini yangu kuwa kama utafiti ulifanyika kweli, basi tutaona miti ikikua vizuri na sio kufa” Amesema Mhe. Senyamule.

Ametoa msisitizo kwa wasimamizi wa eneo hilo kuhakikisha wanalitunza eneo la bonde la Mzakwe ili kupoteza historia mbaya iliyowahi kutokea miaka ya nyuma ya miti kutoota katika eneo hilo, miti kuungua moto na uvamizi wa wananchi kwa kuweka makazi katika vyanzo vya maji na kusababisha uharibifu wa mazingira.

“Tuna imani kubwa miti hii mtaitunza, itakua na kupoteza historia yote ambayo ilitokea katika bonde hili la Mzakwe. Ni wajibu wetu kutunza vyanzo vya maji kwa ajili ya matumizi ya maeneo mbalimbali. Sitatamani kuona uzembe wowote ambao utatokea wa kufanya miti hii isikue, nitoe onyo kwa wananchi ambao ni chanzo cha uharibifu wa miti hii kwa kuchoma moto na kuleta mifugo kwenye hifadhi kuwa ni kinyume cha kisheria na tutawachukulia hatua” Ameongeza Mhe. Senyamule.

Naye Bi. Feliciana Mpanda ambaye ni Afisa Kidaki cha Maji Wami-Ruvu, amesema chanzo hiki ni muhimu kwakuwa kinategemewa kuzalisha maji takribani lita Milioni131 yatakayotumiwa na Jiji la Dodoma licha ya changamoto zinazolikabili bonde hili. Amezitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na uingizaji wa mifugo na uchomaji moto unaofanywa na wananchi wanaozunguka bonde hilo na kutoa rai kwa jamii ukabililiana na changamoto hizi ili kulilinda bonde.

Vilevile, Afisa wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) Bw. Frank Chombo, ameainisha aina 4 ya miti inatakayopandwa katika eneo hilo kulingana na tafiti za udongo zilizofanyika kwenye eneo hili na kuhimiza wananchi kufika kwenye bustani za Wakala wa Misitu Tanzania kote nchini kuchukua miche kwakuwa inapatikana kwa wingi. Kwa wakazi wa Dodoma, amesema bustani zipo maili mbili na eneo la Ikowa katika Wilaya ya Chamwino, pia wana miche zaidi ya Million 1 inayogawiwa bure.

Takriban miti 5,300 imepandwa katika bonde la Mzakwe katika kipindi cha mwezi mmoja na kampeni hii ni endelevu na lengo ni kupanda miti 40,000 ndani ya miaka minne.
Share:

MSIMU MPYA KAMPENI YA NIVISHE KIATU CHA SAMIA SULUHU KUANZA TENA BARA, ZANZIBAR

 

Na Mwandishi Wetu 

MSIMU mpya wa Kampeni ya Samia Nivishe kiatu inayofanywa na Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao inatarajia kuanza kutekelezwa katika mikoa ya Lindi,Mtwara,Songea, Iringa pamoja na Visiwani Zanzibar.


Hadi sasa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao chini ya Uongozi mahiri wa Mwenyekiti wake Steven Mengele maarufu kwa jina la Steve Nyerere imeshawavisha wanafunzi wengi viatu kupitia Kampeni ya Samia Nivishe Kiatu 2022 na sasa msimu mpya wa kampeni utaendelea kwenye mikoa hiyo.


Akizungumza leo Jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao Steve Nyerere amesema kwamba  lengo la kampeni hiyo ni kuhakikisha kila mtoto mwanafunzi mwenye uhitaji anavaa Kiatu cha Samia Suluhu.


"Msimu mpya unaanza Samia nivishe kiatu  utafanyika katika Mkoa wa Lindi, Mtwara,Songea Iringa pamoja na Visiwani Zanzibari, kote huko tunataka wanafunzi wavae kiatu cha Samia Suluhu.


"Kiatu cha Samia Suluhu kitavaliwa katika shule mbalimbali nchini na tutapita kwenye shule na kuwakabidhi  watoto wenyewe viatu hivyo kwa ajili ya mazingira mazuri ya masomo kwa watoto,"amesema Stive Nyerere alipokuwa akielezea kuanza kwa msimu huo mpya.


Kwa mujibu wa Steve Nyerere Kampeni ya Nivishe Kiatu cha Samia Suluhu itafanyika nchini nzima na kwa sasa wameshipita katika mikoa kadhaa kwa kuanza na Wilaya ya Rufiji mkoani Pwani na baadae Mkoa wa Tabora.


Aidha ametumia nafasi hiyo kuelezea kubwa tangu kuanza kwa Kampeni hiyo wanashukuru kwa kuungwa mkono na wadau mbalimbali ambao kwa namna moja au nyingine wameifanya Kampeni hiyo kuwa rahisi kwao huku akisisitiza wataendelea nayo hadi wahakikishe wanafunzi wenye uhitaji wa viatu kote nchini wanafikiwa na kuvaa Kiatu cha Samia Suluhu.


Kampeni hiyo ulizinduliwa mwaka 2022 na Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao ambayo inaundwa na wasanii wa filamu na muziki Tanzania na kauli mbiu yake ni 'Samia Nivishe Kiatu 2022' huku dhumuni kuu likiwa kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan kwenye sekta ya elimu.

Share:

WANAFUNZI WAFARIKI BAADA YA MASHUA KUZAMA


Wanafunzi watatu kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya wamefariki dunia baada ya mashua waliyokuwa wameabiri kuzama eneo la Budalangi, kaunti ya Busia.

Wanafunzi hao watatu walikuwa sehemu ya kundi cha wanafunzi saba ambao walikuwa wamekwenda kufurahia safari ya mashua kabla ya mambo kwenda mrama. 

Kwa mujibu wa ripoti ya runinga ya Citizen, kamanda wa polisi wa kaunti ndogo ya Bunyala Isaiah Mose alisema wanafunzi wanne kati ya saba wameokolewa huku miili mitatu ya ikiwa bado haijaopolewa.

Shughuli za kutafuta mabaki yao zilisitishwa baada ya giza kuingia Jumamosi, Disemba 1, na zinatarajiwa kurejea leo .
Share:

AJALI YAUA WATU SITA WA FAMILIA MOJA BOXING DAY


Familia ya watu sita akiwemo baba, Khumbulani Togara, mama na watoto wao wanne, akiwemo kichanga, wamefariki dunia katika ajali ya kutisha iliyotokea siku ya Boxing Day, Desemba 26, 2022.

Ajali hiyo iliyozua gumzo kubwa na kuwasikitisha wengi, imetokea nchini Afrika Kusini katika eneo la Musina, wakati familia hiyo ikirejea nyumbani kwao, Zimbabwe baada ya kula Krismasi nchini Afrika Kusini.


Video iliyonaswa na kamera za CCTV, imenasa tukio hilo ambapo familia hiyo ikiwa ndani ya gari aina ya Mitsubishi ‘double cabin’, ilivaana uso kwa uso na lori lililokuwa kwenye spidi kubwa na kusababisha maafa hayo.
Ajali hiyo imetokea katika Barabara ya N1 kati ya Miji ya Baobab Tollgate na Musina.

Inaelezwa kuwa chanzo cha ajali hiyo, ni uchovu na mwendokasi.

Taarifa hiyo iliripotiwa pia na Ubalozi wa Zimbabwe nchini Afrika Kusini kupitia kwa Balozi Melody Chaurura


Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU JANUARI 02,2023



\\\







Share:

Sunday, 1 January 2023

WATU 9 WAFARIKI KWA KUKANYAGANA MKESHA WA MWAKA MPYA 2023

 

Watu 9 wamefariki na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya kukanyagana kwenye Msongamano ulitokea Freedom City Mall usiku wa kuamkia Mwaka Mpya 2023.

Akithibitisha tukio hilo Naibu msemaji wa polisi wa Metropolitan ya Kampala, Luke Owoyesigyire amesema kuwa waathiriwa walikandamizwa huku mamia ya watu wakijaribu kurejea ukumbini baada ya kutazama onyesho la fataki lililoanzisha mwaka mpya.

"Inadaiwa kuwa tukio hilo lilitokea usiku wa manane wakati MC wa hafla hiyo aliwahimiza waliohudhuria kutoka nje na kutazama maonyesho ya fataki. Baada ya onyesho kumalizika, mkanyagano ulitokea, na kusababisha vifo vya papo hapo vya watu watano na wengine kadhaa kujeruhiwa,” Owoyesigyire alisema.

Amesema sehemu ya duka hilo imefungwa ili kuruhusu uchunguzi wa tukio la jana usiku lililowaua tisa.

"Ni sehemu tu ambayo tukio la jana usiku limefungwa ili kuruhusu uchunguzi. Eneo hilohilo lilikuwa na tukio lingine lililopangwa kufanyika leo lakini haliwezi kutokea kwa kuwa uchunguzi bado unaendelea kwenye eneo la uhalifu,” Owoyesigyire aliambia Nile Post.

Hata hivyo alibainisha kuwa sehemu nyingine za maduka hayo ikiwa ni pamoja na maduka makubwa na vifaa vingine bado viko wazi na biashara bado inaendelea.

Ziara katika jumba hilo la maduka Jumapili alasiri inaonyesha kuwa baadhi ya washiriki wa sherehe hizo wakiwemo watoto waliokuwa wamefika kwenye bwawa la kuogelea wamerudishiwa pesa zao kwani mahali hapo bado ni eneo la uhalifu.

NILE POST UG
Share:

Video Mpya : NG'WANA SAMAKA - LAWAMA

Share:

MLETE MWANAO BECO PRE & PRIMARY SCHOOL APATE ELIMU BORA

Share:

MALUNDE 1 BLOG INAKUTAKIA HERI YA MWAKA MPYA 2023....Happy New Year!

 🛑 🧊 MALUNDE 1 BLOG inakutakia wewe na familia yako Heri ya Mwaka Mpya 2023


 🌐 Endelea kutembelea www.malunde.com kwa habari za ukweli na uhakika kwa wakati muda wote


📲 Tunapenda tukutumie habari moja kwa moja kwenye simu yako bure kabisa


📢📱 PAKUA APP YETU >HAPA<


⁉️ Una Habari/Taarifa/Tangazo?


⚪ Tupigie🥏 0757478553

Email : malundekadama@yahoo.com

Share:

Saturday, 31 December 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JANUARI 1,2023





Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger