Monday, 16 May 2022

SPIKA WA BUNGE AWAKINGIA KIFUA WABUNGE 19 WALIOFUKUZWA CHADEMA..ASEMA 'JAMBO LAO LIPO MAHAKAMANI'


Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, Tulia Ackson
Wabunge 19 wa CHADEMA waliovuliwa Uanachama
**

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tulia Ackson amewakingia kifua wabunge 19 wa kuteuliwa kutoka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA ambao walivuliwa uanachama na Chama hicho Mei 12,2022 Jijini Dar es Salaam.


Akiongea Bungeni katika Bunge la 12 la Bajeti, Mkutano wa 7 kikao cha 23 amebainisha kama Spika amepokea barua kutoka kwa Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika ikimtaarifu juu ya maamuzi ya Kamati Kuu ya Chama hicho kuhusu kuwavua uanachama Wabunge 19 kutoka chama hicho.


Spika Tulia amesema Bunge haliwezi kuingilia jambo ambalo lipo Mahakamani na kwa mujibu wa Katiba ya nchi Mamlaka yenye kauli ya mwisho kwenye utoaji haki ni Mahakama, hivyo maamuzi ya Mahakama ndiyo yatakayotoa hatima ya Wabunge hao.


Spika Tulia amesisitiza kuwa maswali yeyote kuhusu jambo hilo mtu rasmi wa kuyajibia hayo ndani ya Bunge ni Spika wa Bunge na si mtu mwingine yeyote.


Hata hivyo baadhi ya wabunge kati ya 19 wa Viti Maalum waliofukuzwa uanachama na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wameingia bungeni kuendelea kushiriki vikao vya Bunge.

Aliyeingia wa kwanza kuingia bungeni leo Jumatatu Mei 16, 2022 ni Sophia Mwakagenda ambaye aliingia kwa kutumia mlango wa kawaida akiwa ameongozana na wabunge wengine wa CCM na moja kwa moja kaingia ukumbini.

Mwakagenda kaingia viwanja vya Bunge saa 2.44 asubuhi akitumia geti la kawaida ambalo hutumiwa na wabunge wote.

Dakika sita baadae waliingia Grace Tendega na Conchesta Rwamlaza ambao wao walitumia mlango wa geti linalotumiwa na watumishi wengine maarufu geti la Waziri Mkuu.


Wabunge hao waliingia moja kwa moja hadi ndani ya ukumbi na kuketi katika viti vyao.

Muda mfupi baada ya kuanza shughuli za bunge, waliingia Taunza Malapo na Cecilia Pareso na kama ilivyo kwa wenzao walikaa kwenye Viti vyao na kila mmoja alifungua kishikwambi chake kufuatilia shughuli za bunge ambazo hutumiwa kidigitali kwenye vishikwambi.


Kwenye kipindi cha maswali Grace Tendega alipewa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza kuhusu ukubwa wa Jimbo la Kilolo akihoji ni lini Jimbo hilo ligawanywa kiutawala kwani ni kubwa.


Swali hilo limejibiwa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi David Silinde akiomba wahusika wafuate taratibu zinazotakiwa na Serikali itakapojiridhisha italigawa Jimbo hilo.


Wengine walioingia bunge likiendelea ni Jeska Kishoa, Nusrat Hanje na Ester Matiko.


Ndani ya Bunge Jeska Kishoa alionekana akipita kwenye viti walivyokaa wenzake na kuwaonyesha simu yake kama kitu kilichokuwa kimeandikwa ili wasome.
Share:

WANANCHI HANANG WAMSHUKURU RAIS SAMIA KWA KUWAPATIA BILIONI 20 ZA MIRADI YA MAENDELEO NDANI YA MWAKA MMOJA


Katibu wa Itikadi na Uenezi Taifa Shaka Hamdu Shaka akielekeza jambo kwa Mkuu wa Wilaya ya Hanang Mhe. Janeth Mayanja alipokuwa akizungumza na Wananchi baada ya kupokea changamoto mbalimbali za Wanancnhi wa Kata ya Gitting,Hanang waliofika kumsikiliza

**

Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Manyara

WANANCHI wa Wilaya ya Hanang mkoani Manyara wamesema wanampongeza na kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na kazi kubwa na nzuri anayoifanya katika kuleta maendeleo na kwamba wilaya hiyo wamepokea Sh.bilioni 20 kwa ajili ya miradi ya maendeleo ndani ya mwaka mmoja tu.

Akitoa salamu kwa niaba ya wananchi hao, mbele ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Shaka Hamdu Shaka ambaye ni mlezi wa Mkoa huo, Mkuu wa Wilaya ya Hanang Janeth Mayanja amesema wilaya hiyo kupitia Rais Samia na Serikali anayoingoza wamepiga hatua kubwa kimaendeleo kutokana na utekelezaji mikubwa ya maendeleo katika nyanja mbalimbali.

“Kwa niaba ya wananchi wa Wilaya ya Hanang tunakuomba Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi utufkishie salamu zetu za shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa, huku kwetu tumepokea fedha nyingi za maendeleo.Ndani ya mwaka mmoja wa Rais Samia tumepokea Sh.bilioni 20 za kutekeleza miradi, huko nyuma hatukuwahi kupatiwa fedha nyingi kwa kiasi hiki , tunashukuru na wananchi wa Hanang tunampenda sana , tunamuunga mkono,”amesema Mayanja.

Kuhusu changamoto, Mkuu huyo wa Wilaya amemueleza Shaka kwamba, moja ya changamoto kubwa iliyokuwepo katika wilaya hiyo ilikuwa ni maji lakini tayari Serikali imetoa fedha kwa ajili ya kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama kwenye maeneo ambayo yamekuwa na changamoto hiyo akitolea mfano kata ya Gitin.

“Katika kata ya Gitin kuna changamoto ya maji lakini tunakumbuka wakati wa uchaguzi mkuu mwaka 2020, Mama Samia alifika kwenye Wilaya yetu na alikuja Kata ya Gitin alituahidi kuwa changamoto ya maji itapata ufumbuzi.

“Leo sote tunashuhudia mradi wa maji ukiendelea kutekelezwa na tayari tumeshaanza kupokea fedha Sh.bilioni 2.2 kati ya Sh.bilioni tatu ambazo zinahitajika.Tunaamini ndani ya miezi sita mradi utakuwa umekamilika na wananchi kwenye maeneo ambayo mradi huu umepita hawatakuwa na shida ya maji.Yoye hata yanafanyika chini ya Rais Samia,”amesema Mayanja.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Hanang Mathew Dareda amesema wananchi wa wilaya hiyo wameendelea kufurahishwa na namna ambavyo Rais Samia amekuwa akiwatumikia katika kuleta maendeleo na imani yao kuna siku atafanya ziara kwenye Wilaya hiyo na kwamba Rais Samia anaupiga mwingi kutokana na maendeleo aliyowapelekea.

Baada ya salamu hizo za viongozi wa Wilaya hiyo, Shaka alipata nafasi ya kuzungumza na wananchi wa Wilaya ya Hanang katika maeneo tofauti ambako alikwenda kukagua utekelezaji wa miradi likiwemo eneo la Gitin amesema kuwa Serikali inayoongozwa na Rais Samia imedhamiria kutatua changamoto za wananchi na kuboresha maisha yao.

“Kikubwa ndugu zangu wana Hanang, Manyara na Watanzania kwa ujumla tuendelee kumuunga mkono Rais Samia ambaye ana dhamira ya dhati kabisa ya kulitumikia taifa letu, amekuwa akifanya mambo makubwa ya kute maendeleo kila kona, katika kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wake amefanya makubwa yanayostahili kupongezwa.Niwahakikishie Rais Samia atatuvusha.

“Wakati nakuja huku nimewasiliana na Rais kwa njia simu, ameniambia maneno mawili tu kwanz anawapenda sana wananchi na pili anasema kazi iendelee na kubwa zaidi nchi yetu iko salama, imetulia.Niwaombe wananchi watoe ushirikiano kwa Serikali,”amesema Shaka.

Mbali ya kuzungumza na wananchi amepata nafasi ya kutembelea miradi ya maendeleo ndani ya wilaya hiyo ambapo amepongeza kazi nzuri inayofanywa na viongozi ngazi ya wilaya kwa kushirikiana na viongozi wa Mkoa.
Mkuu wa Wilaya ya Hanang Mhe Janeth Mayanja akitoa ufafanuzi wa baadhi ya changamoto zilizotolewa na Wananchi mbele ya Katibu wa Itikadi na Uenezi Taifa Shaka Hamdu Shaka ambaye pia ni mlezi wa CCM mkoa wa Manyara
Baadhi ya Wananchi waliofika kumsikiliza Katibu wa Itikadi na Uenezi Taifa Shaka Hamdu Shaka ambaye pia ni mlezi wa CCM mkoa wa Manyara.
Katibu wa Itikadi na Uenezi Taifa Shaka Hamdu Shaka ambaye pia ni mlezi wa CCM mkoa wa Manyara alipowasili kuzindua ofisi ya CCM tawi la Gehandu,Hanang mkoani Manyara na baadae alizungumza na Wanachama wakiwemo na baadhi ya Wananchi waliofika kushuhudia tukio hilo
Katibu wa Itikadi na Uenezi Taifa Shaka Hamdu Shaka ambaye pia ni mlezi wa CCM mkoa wa Manyara
Share:

SHULE YA SEKONDARI ILIYOSHIKA NAFASI YA TATU KITAIFA WAMSHUKURU RAIS SAMIA KUWABORESHA MIUNDOMBINU YA ELIMU, SHAKA ATIA NENO


Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Taifa Shaka Hamdu Shaka akifungua bomba la maji ndani ya moja ya chumba cha Maabara shule ya Sekondari ya Ayalagaya iliyopo mkoani Manyara jana Mei 15,2022.

Na Said Mwishehe, Michuzi TV

SHULE ya Sekondari ya Ayalagaya iliyopo mkoani Manyara ambayo imeshika nafasi ya tatu kitaifa matokeo ya kidato cha nne mwaka 2021 wameishukuru Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha miundombinu ya shule yao, hivyo kufanya shule kimasomo.


Wametoa salamu hizo za shukrani kwa Rais Samia na Serikali yake kupitia Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Shaka Hamdu Shaka ambaye alifanya ziara ya kuitembelea shule hiyo kwa lengo la kuwapongeza na kuwafikisha salamu za Rais Samia kuwa ataendelea kuboresha miundobinu ya sekta ya elimu nchini.

Mkuu wa Shule hiyo Stephene Naman amemueleza Shaka kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inastahili pongezi na shukrani kwa kuendelea kuboresha miundombinu ya shule hiyo , hivyo kwa kipekee wanamshukuru Rais Samia.

“Taaluma ya wanafunzi shuleni kwetu imekuwa ikimarika na kuridhisha mwaka hadi mwaka kwani mwaka 2021 shule ilikuwa na ufaulu wa daraja la kwanza hadi daraja la tatu tu katika matokeo ya mtihani wa taifa kidato cha nne mwaka jana.

“Katika matokeo ya mtihani jumla ya wanafunzi waliofanya mtihani walikuwa 95, waliopata daraja la kwanza ni wanafunzi 29,daraja la pili wanafunzi 54 na daraja la tatu walikuwa 12.Hakuna daraja la nne wala zero.

“Kwa matokeo hayo tumefanikiwa kuwapeleka wanafunzi 83 ngazi ya kidato cha tano na wanafunzi 12 vyuo vya kati.Mafanikio yetu yanatokana na jitihada za Serikali kuboresha miundombinu yetu hapa shuleni,”amesema.

Akifafanua zaidi, amesema shule yao imepata tuzo mbili kutoka Wizara ya TAMISEMI kwa kushika nafasi ya tatu kitaifa kwa shule za kata na nafasi ya kwanza kwa shule zilizoboresha ufaulu kwa kiwango cha juu kwa miaka mitatu mfululizo.

Kuhusu hali ya ujenzi wa maabara, madarasa , mabweni na bwalo , Naman amemwambia Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM kuwa ujenzi wa madarasa mawili umekamilika na mradi umegharimu Sh.46,576,140 .

Pia wamekamilisha mabweni mawili kwa ajili ya kidato cha tano na sita yaliyogharimu Sh.425,960,262.Aidha ujenzi wa maabara mbili na darasa moja yaliyogharimu Sh.189,294,600 pamoja na ujenzi wa bwalo ambalo limegharimu Sh.248,960,651.

Kwa upande wake Shaka pamoja na kupata taarifa kuhusu shule hiyo amepata fursa ya kukagua ujenzi wa miundombinu ambapo amewaleza wananchi kinachofanywa katika shule hiyo pamoja na shule nyingine ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya CCM.

Shaka amesema Ilani ya CCM inaelekeza kwa Serikali kuhusu kuboreshwa kwa miundimbinu ya elimu katika sekta ya elimu.Aidha amewapongeza walimu na wanafunzi kwa shule hiyo kuwa na ufaulu mzuri ambapo ametoa mwito kwa wanafunzi kuhakikisha wanajikita zaidi kwenye masomo kwani Serikali imetimiza wajibu wake.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Taifa Shaka Hamdu Shaka akifungua bomba la maji ndani ya moja ya chumba cha Maabara shule ya Sekondari ya Ayalagaya iliyopo mkoani Manyara jana Mei 15,2022.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Taifa Shaka Hamdu Shaka akipokea taarifa ya shule kutoka kwa Mkuu wa Shule hiyo ya Sekondari ya Ayalagaya, Stephene Naman

Muonekana wa madarasa mawili ambayo tayari yamekamilika

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Shaka Hamdu Shaka akimkabidhi tuzo Mkuu wa Shule hiyo ya Sekondari ya Ayalagaya, Stephene Naman kwa kufanya vizuri Kitaifa,tuzo hiyo imetolewa kwa niaba ya CCM mkoa wa Manyara

Baadhi ya Walimu wa Shule hiyo ya Sekondari ya Ayalagaya wakiwa katika picha ya pamoja na tuzo yao

Moja ya bweni ya  Shule hiyo ya Sekondari ya Ayalagaya ambayo tayari limekamilika.PICHA ZOTE NA MICHUZI JR-MMG

Share:

STAKEHOLDERS KEEN TO HALT THE SPREAD OF THE COVID-19 PANDEMIC

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU MEI 16,2022

Magazetini leo Jumatatu May 16,2022

Share:

Sunday, 15 May 2022

Video Mpya : MJUKUU WA MWANAMALONDE - RIZIKI


Malunde 1 blog inakualika kutazama video mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Maarufu Mjukuu wa Mwanamalonde inaitwa Riziki
Tazama Video hii hapa chini
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI MEI 15, 2022




Magazetini leo Jumapili May 15 2022...Mishahara juu



Share:

LIVERPOOL YATWAA KOMBE LA FA ENGLAND




TIMU ya Liverpool imefanikiwa kutwaa Kombe la FA England baada ya miaka 16 kufuatia ushindi wa penalti 6-5 timu hizo zikitoka kumaliza dakika 120 bila kufungana Uwanja wa Wembley Jijini London.


Waliofunga penalti za Liverpool ni James Milner, Thiago Alcântara, Roberto Firmino, Trent Alexander-Arnold, Diogo Jota na Konstantinos Tsimikas, huku Sadio Mane pekee akikosa mkwaju wake ukiokolewa na kipa Msenegal mwenzake, Édouard Mendy.

Upande wa Chelsea waliofunga ni Marcos Alonso, Reece James, Ross Barkley, Jorginho na Hakim Ziyech huku César Azpilicueta na Mason Mount wakikosa.
Share:

MWANAFUNZI AUAWA KWA KUPIGWA NA WANAFUNZI WENZAKE AKIDAIWA KUKASHFU DINI



Waandamanaji wakiwa nje ya kasri la Sultan wa Sokoto, Muhammadu Sa’ad Abubakar

Serikali ya Jimbo la Sokoto nchini Nigeria, imetangaza marufuku ya kutotoka nje kwa muda wa saa 24 kuanzia leo, ili kukabiliana na maandamano na fujo za waandamanaji wanaotaka kuachiwa kwa wanafunzi wanaoshikiliwa kwa tuhuma za kumuua mwanafunzi mwenzao, Deborah Samuel kwa madai ya kuikashifu dini yao.


Debora alipigwa na wanafunzi wenzake wa Chuo cha Shehu Shagari College of Education mpaka kuuawa kisha mwili wake kuchomwa moto kwa madai ya kuikashifu dini yao kwenye group la WhatsApp ambapo baada ya tukio hilo, polisi walianza kuwasaka waliohusika na mauaji hayo na kufanikiwa kuwakamata wanafunzi wawili huku wengine wakiendelea kusakwa.

Hata hivyo, baadhi ya wananchi hawakuridhishwa na hatua hiyo ya polisi wakidai kuwa marehemu alistahili kuuawa, wakaanzisha maandamano ya kutaka wote waliokamatwa kuachiwa ara moja.

Katika taarifa iliyotolewa leo na Gavana wa Sokoto, Aminu Waziri Tambuwal, watu wote wanatakiwa kukaa majumbani mwao kwa saa 24 ili kupisha vyombo vya ulinzi na usalama kurejesha amani hususan katika Mji wa Sokoto na maeneo jirani.
Share:

SIMBA YATINGA NUSU FAINALI YA ASFC...YAIFUATA KIBABE YANGA




Na Alex Sonna

SIMBA w wametinga Nusu Fainali ya Michuano ya Kombe la Azam Sport Federation (ASFC) na kuifuata Yanga kibabe baada ya kuichapa mabao 4-0 Timu ya Pamba FC kutoka Mwanza Mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Mabao ya Simba yamefungwa na Peter Banda dakika ya 45 kipindi cha kwanza baada ya kupokea pasi ya Rally Bwalya bao lililopelekea Simba kwenda mapumziko wakiwa wanaongoza bao moja.

Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko huku Simba ikinufaika zaidi na mabadiliko hayo.

Kibu Denis aliwanyanyua mashabiki wa Simba dakika ya 47 akifunga bao mara baada ya kupokea krosi ya Mohamed Hussein na mabaao mawili yamefungwa na Yusuph Mhilu dakika ya 52 na 88.

Kwa ushindi huo Simba watakutana na Yanga Nusu Fainali ya Michuano hiyo huku Azam FC watakutana na Coastal Union.
Share:

Saturday, 14 May 2022

Breaking News : HATIMAYE RAIS SAMIA ATANGAZA KUPANDISHA MISHAHARA KWA WATUMISHI WA UMMA

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Haasan ameridhia mapendekezo ya nyongeza ya mshahara ikiwemo kima cha chini kwa watumishi wa Umma kwa 23.3%

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger