Thursday, 15 April 2021

MAWAZIRI WA WIZARA ZA VIWANDA NA BIASHARA, NA WIZARA YA UWEKEZAJI WAKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA MAREKANI NCHINI

 

Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo akizungumza na wanahabari mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo na Balozi wa Marekani Bw. Donald Wright ambapo wamefanya mazungumzo kuhusu fulsa za uwekezaji hapa nchini.

Waziri wa Uwekezaji Mhe. Geoffrey Mwambe akizungumza na wanahabari mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo na Balozi wa Marekani Bw. Donald Wright ambapo wamefanya mazungumzo kuhusu fulsa za uwekezaji hapa nchini.

Balozi wa Marekani Bw. Donald Wright akizungumza wakati wa kikao na Mawawiri wawili wa Wizara mbili Viwanda na Biashara, na Uwekezaji walipokutana kujadili fulsa za uwekezaji hapa nchini.

Mawaziri na Naibu Waziri wakiwa katika mazungumzo na Balozi wa Marekani Bw Donald Wright walipokuwa wakizungumzia fursa za uwekezaji hapa nchini.

Balozi wa Marekani Bw Donald Wright akimkabidhi kitabu Waziri wa Uwekezaji kinachoonesha fursa mbalimbali zinazohitajika kuwekeza, mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo yao yaliyofanyika jana April 14,2021 jijini Dodoma,kulia ni Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Prof.Kitila Mkumbo akionyesha kitabu hicho.

Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo na Waziri wa Uwekezaji Geoffrey Mwambe wakipitia kitabu chenye fulsa za uwekezaji walivyokabidhiwa na Balozi wa Marekani Bw Donald Wright mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo.

Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo watatu kutoka kulia akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Uwekezaji Geoffrey Mwambe, na Balozi wa Marekani Bw. Donald Wright wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo kuhusu fulsa za uwekezaji.


Na.Alex Sonna,Dodoma

Mawaziri wawili wa Wizara za Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo na Wizara ya Uwekezaji Geoffrey Mwambe wamekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Marekani hapa nchini Bw. Donald Wright kwa lengo la kujenga ushirikiano na kushirikishana fursa za uwekezaji zinazopatikana hapa nchini.

Akizungumza na waandishi wa Habari mara baada ya mazungumzo hayo Waziri ya Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo amesema katika mazungumzo yao wamelenga kukuza biashara na uwekezaji baina ya nchi mbili za Tanzania na Marekani.

“Leo tumekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Marekani hapa nchini Bw. Donald Wright, kuona namna ya kukuza ushirikiano wetu uliopo baina ya nchi hizi mbili, bado tunafursa nyingi na kubwa za wafanyabiashara wetu kutumia fursa hiyo” amesema Prof. Mkumbo.

Amesema katika mazungumzo hayo wamekubaliana kuweka jitihada za kuhakikisha nchi hizo mbili zinazidi kushirikiana katika nyanja za kiuwekezaji na kuleta manufaa na kuwawezesha wafanyabiashara kuwanya biashara kukuza uchumi wa nchi na mtu mmoja moja.

Amesema katika mazungumzo hayo pia wamezungumzia kuhusu mazao ya kimkakati hasa katika kuchakata na sio kuuza malighafi, na hatimaye mazao hayo yachakatwe hapa nchini na kuuza bidhaa badala ya kuuza malighafi, na sekta ya matunda ambayo yanapatikana kwa wingi hapa nchini.

Nae Waziri wa Uwekezaji Mhe. Geoffrey Mwambe amesema katika mazungumzo hayo pia wamezungumza kuhusu uwekezaji katika sekta mbalimbali ikiwamo ya afya hapa nchini, na wameonekana kuridhika na hatua mbalimbali zilizochukuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan katika uwekezaji.

Amesema wawekezaji kutoka Marekani wameonyesha wapo tayari kuja kuwekeza hapa nchini ambapo tayari kuna kampuni imeonyesha nia ya kuja kuwekeza katika sekta ya mawasiliano kwa kuwekeza katika kampuni ya simu, na kampuni ya utalii kutoka Arusha imeonyesha nia ya kutaka kuongeza zaidi uwekezaji.

Ameongeza kuwa “Tumeongelea uchakataji wa mazao na ukiangalia Marekani ananunua korosho nchi flani, na ukiangalia sisi tunauza korosho ghafi na hizo nchi zinachakata na kuuza marekani, na sisi sasa tunaweza kuzichakata hapa nchini na kuuza Marekani” amesema Waziri Mwambe.

Amesema pia yapo mazao mengine ya kumkakati kama Kahawa na Pamba ambayo yatachakatwa na kuuzwa nje ya nchi hatimaye kama nchi kupata mapato kupitia kodi na kukuza ajira kwa wananchi ambao watapata ajira katika viwanda hivyo vitakavyoanzishwa.

Amesema katika mazungumzo hayo wamekubaliana kufanya majadiliano mara kwa mara ili kuuisha makubaliano yao ambapo watakuwa wakifanya tathmini kuona makubaliano hayo yanavyofanya kazi katika kuimarisha ushirikiano uliopo kwa miaka sitini sasa baina ya haya mataifa mawili.

Kwa upande wake Balozi wa marekani nchini Tanzania Mhe. Donald J. Wright amefurahishwa na ushirikiano wa kudumu wa Zaidi ya miaka 70 uliopo kati ya Tanzania na Marekani na

Mhe.Wright ameahidi kuwa Serikali ya Marekani itashirikiana kwa dhati na kwa karibu na Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha wawekezaji kutoka marekani wanakuja kuwekeza nchini Tanzania kwani nchi hii ina fursa nyingi za uwekezaji pamoja na hali nzuri ya ulinzi na usalama. Balozi Mhe. Wright amesema kuwa Marekani imetengeneza historia kubwa katika kusaidia maendeleo ya Tanzania katika miradi ya kupambana na magonjwa, Ulinzi, elimu, miundombinu n.k ambapo hiyo imepelekea uhusiano kati ya Marekani na Tanzania kuimarika zaidi.

Share:

ENVIRONMENTAL OFFICER II at TANESCO

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

POST ENVIRONMENTAL OFFICER II – 1 POST POST CATEGORY(S) RESEARCH,SCIENCE AND BIOTECH EMPLOYER TANZANIA ELECTRIC SUPPLY COMPANY LIMITED (TANESCO) APPLICATION TIMELINE: 2021-04-14 2021-04-27 JOB SUMMARY NA DUTIES AND RESPONSIBILITIES i. To assist in developing environmental policy, guidelines, action plans and programs as far as environmental Management is concerned; ii. To assist in preparing action plans […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

ELECTRICAL TECHNICIAN – 6 POST at TANESCO

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

POST ELECTRICAL TECHNICIAN – 6 POST POST CATEGORY(S) ENGINEERING AND CONSTRUCTION EMPLOYER TANZANIA ELECTRIC SUPPLY COMPANY LIMITED (TANESCO) APPLICATION TIMELINE: 2021-04-14 2021-04-27 JOB SUMMARY NA DUTIES AND RESPONSIBILITIES i. To be responsible for operating, controlling, maintaining, testing, troubleshooting, installing and repairing electrical control systems and equipments in hydroelectric power generating operations; ii. To perform minor […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

TECHNICIAN –(SURVEY) at TANESCO

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

POST TECHNICIAN –(SURVEY) – 1 POST POST CATEGORY(S) LAND MANAGEMENT EMPLOYER TANZANIA ELECTRIC SUPPLY COMPANY LIMITED (TANESCO) APPLICATION TIMELINE: 2021-04-14 2021-04-27 JOB SUMMARY NA DUTIES AND RESPONSIBILITIES i. To assist in preparing drawings, plans, and topographic maps; ii. To prepare Survey instruments such as Total stations, Differential GPS and level machine prior to execution of […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

MAWAZIRI WAKETI KUWEKA MAMBO SAWA KUHUSU MAAGIZO YA RAIS YA ONLINE TV


Na Faraja Mpina, WMTH, Dodoma
***
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Faustine Ndugulile na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wamefanya kikao cha pamoja na Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu pamoja na wataalamu kujadili hoja mbalimbali zinazohusu utekelezaji wa majukumu ya Sekta ya Mawasiliano na Utangazaji nchini hasa wakiangazia suala la Online TV katika vipengele vya usajili, kanuni, sheria, miongozo pamoja na tozo.

Kikao hicho kimefanyika tarehe 14.04.2021 Jijini Dodoma kikiwa ni utekelezaji wa maelekezo yaliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika hotuba yake wakati akiwaapisha Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu na Wakuu wa Taasisi kuhusu kufanya marekebisho ya kanuni na sheria zinazosimamia vyombo vya habari nchini hususani Televisheni Mtandao (Online TV).

Miongoni mwa maazimio yaliyoafikiwa na pande zote mbili ni pamoja na kuangaliwa upya muundo mzima wa uwajibikaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa Wizara zote mbili pasipo kuathiri utekelezaji wa majukumu ya mamlaka hiyo katika Sekta ya Mawasiliano na Utangazaji nchini.

Aidha, mawaziri hao walikubaliana kuzipitia upya kanuni, sheria na miongozo mbalimbali kuhusu Online TV ikiwa ni pamoja na kuweka mifumo rafiki ya usajili na malipo kuangalia uwezekano wa kupunguza tozo na kufanya uchambuzi yakinifu wa nani anatakiwa kulipia kuendana na matumizi husika.

Katika hatua nyingine TCRA ilipewa maelekezo ya kuongeza utoaji wa elimu kwa umma kuhusu usajili, kanuni, sheria na taratibu zote za Online TV ili ziwe wazi kwa wananchi na elimu hiyo iambatane na elimu ya matumizi sahihi ya mtandao kwa lengo la kuongeza uwazi na uwajibikaji wa pamoja.

Pamoja na mambo mengine mawaziri hao walipitia hoja mbalimbali zinazotakiwa kufanyiwa mapitio na maboresho ikiwa ni pamoja na chaneli za runinga zinazotakiwa kuonekana katika visimbuzi bila malipo (FTA), kanuni za maudhui na utoaji wa adhabu kwa vituo vya redio na runinga uwekewe ukomo kwa mujibu wa kanuni na adhabu ziwe zenye lengo la kulea na si vinginevyo.

Mawaziri hao kwa pamoja na watendaji wao wakuu wamejipanga kuhakikisha Sekta wanazozisimamia hasa katika maeneo ambayo yana muingiliano katika utendaji wao yanafanyiwa maboresho makubwa kuendana na hali halisi ya sasa ya kukua kwa teknolojia ya habari na mawasiliano na kuhakikisha malalamiko ya wananchi yanafanyiwa kazi na wao kama watendaji wanazungumza lugha moja kwa manufaa ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

Wajumbe waliohudhuria kikao hicho ni pamoja na Naibu Waziri wa Wizara ya Mawasiliano na Tekbnolojia ya Habari Mhe. Mhandisi Kundo Mathew, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Zainab Chaula na Naibu wake Dkt. Jim Yonazi, Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Hasaan Abbas.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari
Share:

MH. LUHAGA MPINA AIBUA SAKATA LA TEMBO KUVAMIA WANANCHI, ATAKA WAFUGAJI WALIOSHINDA KESI MAHAKAMANI KUTENDEWA HAKI



MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina amesema Jimbo la Kisesa linachangamoto nyingi sana ikiwemo uvamizi wa tembo ambao wamekuwa wa muda mrefu bila kupata suluhisho kutoka serikalini.


Amesema wananchi wanavamiwa na tembo mazao yao yanaliwa yakiwa shambani na hata yakiwa nyumbani chakula kinaliwa mashamba yote yanakanyagwa watu wamepoteza maisha wengine wamepata ukilema wa kudumu.

Mhe. Spika tumelalamika sana na tumeomba sana serikalini kulitatua hili tatizo lakini leo miaka mitatu sasa wananchi hao bado wanaendelea kwenye dhiki kubwa sana ya uvamizi wa tembo lakini uvamizi huu uko kwenye maeneo mengine pia

Mhe. Waziri Mkuu kwa sababu ni muda mrefu sana na tumekuwa tukipeleka malalamiko haya serikalini na hayajatatuliwa mpaka sasa hivi ambapo imepeleka umasikini mkubwa kwa wananchi tunaomba tatizo hili lifike mwisho.

Mhe. Spika tunajua Serikali hii tuliyonayo ya awamu ya tano na hii ya sita imetatua mambo mengi yaliyokuwa yameshindikana lakini imeweza kuyatatua mambo makubwa imeweza kuyatatua haiwezi kushindwa kuwazuia tembo.


Mhe. Spika tumeweza kumaliza mambo ya rushwa na ufisadi, tumeweza kumaliza madawa ya kulevya tumeweza kumaliza ujambazi na ujangili, tumeweza kumaliza uvuvi haramu tuje tushindwe na tembo”?

Mhe. Spika hapa kuna mtu mmoja hajawajibika sawasawa tunataka safari hii wananchi waishi kwa amani katika maeneo yao na tatizo hili la Tembo Mhe. Waziri Mkuu agiza likomeshwe mara moja.

Mhe. Spika tunalo tatizo pia kubwa sana la wafugaji ambao walikuwa wanafuga wakakamatwa na wahifadhi kwamba wanachungia ndani ya hifadhi na baada ya hapo wakaenda kushinda kesi mahakamani wakakatiwa rufaa wakaenda kushinda kesi mahakamani zaidi ya wafugaji 30 wenye ng’ombe wasiopungua 5,000 ng’ombe wao mpaka sasa hivi wanashikiliwa na Serikali licha ya kushinda kesi mahakamani.

Na wamefuatilia serikalini kurudishiwa mifugo yao kwa sababu wameshapewa haki hiyo na Mahakama warudishiwe mifugo yao lakini mpaka sasa hivi tunavyozungumza Mhe Spika ng’ombe hao hawajarudishwa na sababu za kutorudishwa hazijulikani mtu ameshinda kesi mahakamani kwanini uendelee kuzuia mifugo yake?.

Mhe. Spika kwa Jimbo la Kisesa peke yake ni zaidi ya ng’ombe 1,000 wanashikiliwa licha ya wananchi hao kushinda kesi mahakamani wananchi akina Malimi Sendama na wenzake, Ndaturu Malolo, Kwandu Malaba, Masunga Mhamali, Subi Maduhu na wengine Mhe. Waziri Mkuu tunataka kuambiwa huko Serikalini aliyekataa ng’ombe hizi zisitolewe ni nani kama mahakama imesha grant haki hao wafugaji aliyekataa huko serikalini ni nani?.

Mhe. Spika namuomba sana Mh. Waziri Mkuu aliingilie kati hili suala tukatende haki kwa hao wananchi wanyonge ambao mifugo yao imeshikiliwa na Serikali licha ya wao kushinda kesi mahakamani na tukitoka kwenye hili bunge niende na hizo ngombe za wananchi hawa
Share:

MPANGO WA TAIFA WA KUPAMBANA NA UCHAFUZI WA MAZINGIRA YA BAHARI UMEKUJA WAKATI MUAFAKA-RC SHIGELLA

 

MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza wakati akifungua warsha ya pili ya wadau wa Mpango wa Taifa wa kujiandaa na umwagikaji wa mafuta kwenye bahari na maziwa inayofanyika kwa wiku tatu mkoani Tanga kushoto ni Mkurugenzi Idara ya Udhibiti uchumi Tasac Nahson Sigalla akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Tasac
Mkurugenzi Idara ya Udhibiti uchumi Tasac Nahson Sigalla akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Tasac akizungumza wakati wa warsha hiyo kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella
MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella  akiwa ameshikilia kitabu chenye  Mpango wa Taifa wa kujiandaa na umwagikaji wa mafuta kwenye bahari na maziwa mara baada ya kufunga warsha ya wadau wa mpango huo wa Taifa Jijini Tanga kushoto ni Mkurugenzi Idara ya Udhibiti uchumi Tasac Nahson SigallaMkurugenzi Idara ya Udhibiti uchumi Tasac Nahson Sigalla kushoto akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kitabu chenye mpango wa wa Taifa wa kujiandaa na umwagikaji wa mafuta kwenye bahari na maziwaMKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella  kulia akiteta jambo na Mkurugenzi Idara ya Udhibiti uchumi Tasac Nahson Sigalla wakati wa warsha hiyo
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye warsha hiyo
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye warsha hiyo

MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella amefungua warsha ya pili ya wadau wa Mpango wa Taifa wa kujiandaa na umwagikaji wa mafuta kwenye bahari na maziwa inayofanyika kwa wiku tatu mkoani Tanga
 
Akizungumza wakati akifungua warsha hiyo,RC Shigella alisema Serikali kupitia Shirika la uwakala wa meli Tanzania (Tasac) imekuja na mpango wa Taifa wa kupambana na uchafuzi wa mazingira baharini unaotakana na umwagikaji wa mafuta kwa lengo la kuzifanya bahari na maziwa nchini ziweze kukabiliana na umwagikaji wa mafuta kutoka nchi jirani.
 
Alisema mpango huo umekuja wakati muafaka kutokana na kuongezeka kwa shughuli nyingi kwenye bahari na hivyo kupelekea uchafuzi na hatimaye kuhatarisha matumizi ya bahari kwa watumiaji. 

Alisema mpango huo utasaidia sana hasa wakati huu ambapo kumekuwa na matumizi mengi ya baharini na hivyo kuna uwezekano kukatokea uchafuzi wa mazingira. 

"Serikali imeona ipo haja ya kuja namkakati wa mpango huu wa kujiandaa na umwagikaji wa mafuta baharini na kwenye maziwa tumeona shughuli za baharini zinavyozidi kuongezeka na namna ambavyo shughuli za mafuta zinavyozidi kuwa nyingi…….., alisema RC Shigela na kuongeza kuwa

Kama tunavyofahamu Tanzania ina maziwa mengi sana na Tanzania ina bahari ya hindi ina zaidi ya kiliomota zaidi ya 1000 za bahari,  ni eneo kubwa ambalo linaweza kupata uchafuzi wa baharini na uchafuzi wa baharini unaweza ukatokana na meli zinazoleta mafuta lakini pia unaweza kutokea sehemu ya nchi nyingine sababu sisi tupo majirani na upande wa Mombasa na Mozambique uchafuzi unapotokea huko upo uwezekano wa kuja upande wa kwetu wa Tanzania. 

Alisema endapo patatokea tatizo la kumwagika mafuta nchi jirani upo uwezekano mkubwa wa madhara yake kufika mpaka nchini mwetu na ndio maana serikali imeona ipo haja ya kuja na mpango utakaotumika kwajili ya kukabiliana na uchafuzi huo. 

Shigela alisema mpango huo hauhusu eneo la baharini pekee bali unahusisha mpaka maziwa ya Tanganyika,  Victoria na Nyasa kutokana na kuwepo kwa muingiliano mkubwa wa shughuli za kibinadamu katika maziwa hayo. 

Hata hivyo Shigela alisema mpango huo umekuja wakati muafaka ambapo serikali ina dhamira ya dhati ya kuboresha mazingira ya shughuli za baharini kwa kupanua meli zetu kwa kujenga misingi na gati nzuri ambazo zitatumia meli kubwa lakini pia kwa kushuhudia wakati wowote ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda kuja bandari ya Tanga unaanza kutekelezwa. 

Kwa upande wake Mkurugenzi Idara ya Udhibiti uchumi Tasac Nahson Sigalla akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Tasac,  alisema kuwa majukumu ya Tasac ni kusimamia ulinzi na usalama wa usafiri majini na kuzuia uchafuzi wa mazingira unaotokana na shughuli za usafiri wa majini ambapo katika jukumu hilo shirika husimamia utekelezaji wa mikataba ya kimataifa ya shirika la bahari duniani (IMO)  iliyoridhiwa na jamuhuri ya muungano wa Tanzania. 

Mkurugenzi huyo alisema kutokana na majukumu ya Tasac ni kazi ya msingi ya shirika kuzuia uchafuzi wa mazingira unaotokana na umwagikaji wa mafuta kutoka kwenye vyombo vya usafiri majini kwasababu hiyo shirika kwa kushirikiana na taasisi nyingine za serikali liliandaa mpango wa Taifa wa kujiandaa na umwagikaji wa mafuta kwenye bahari na maziwa mwaka 2016.

Mpango huo ulifanyiwa mabadiliko mwaka 2020 na kuidhinishwa na waziri wa ujenzi na uchukuzi kama nchi walibaini umuhimu wa mpango na kuuandaa kwasababu unakidhi matakwa ya mikataba ya kimataifa ambayo Tanzania imeridhia.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI APRILI 15,2021















 

Share:

Wednesday, 14 April 2021

Mbunge Chikota ataka utekelezaji Mchuchuma na Liganga kuanza


Mbunge wa Nanyamba (CCM), Abdallah Chikota, ameiomba serikali kuanza kutekeleza mradi wa makaa ya mawe wa Mchuchuma na Liganga ili Bandari ya Mtwara ifanye kazi kwa ufanisi.

Akichangia leo bungeni bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka 2021/22, Chikota amehimiza matumizi ya bandari hiyo kutokana na serikali kufanya uwekezaji mkubwa uliogharimu zaidi ya Sh.Bilioni 57.

“Bandari ya Mtwara ina uwezo wa kupokea tani milioni moja naomba ule mradi sasa wa kujenga reli kutoka Mtwara hadi Mbambabay na mradi wa Mchuchuma na liganga sasa uanze ili utumike ipasavyo,”amesema.

Kuhusu zao la korosho, Chikota ameomba Wizara ya Kilimo kurekebisha dosari zilizopo katika mfumo wa stakabadhi ghalani kwa kuwa umeleta mafanikio makubwa sana kwenye sekta ya korosho.

Pia, ameitaka serikali ijipange kutumia maji kutoka mto Ruvuma kupeleka Mtwara ili kuondoa tatizo la maji.




Share:

Basata Watoa Onyo Kwa Wasani Kudhalilishana

 Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limeingilia kati sakata la kusambazwa kwa video zisizo na maadili kwa msanii Harmonize kwa kutoa taarifa inayosema imesikitishwa na kitendo hicho kinachoendelea kwenye mitandao ya kijamii.

Aidha BASATA wametoa onyo na kukemea  vikali vitendo hivyo na kuwataka wahusika kuacha tabia hiyo na hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa msanii atakayebainika kuendelea kutenda vitu hivyo.

"Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) limesikitishwa na matukio na mienendo ya wasanii wa Tanzania kwenye mitandao ya kijamii kwa kushamiri vitendo vya matumizi ya lugha zisizo na staha, malumbano, kukashifiana na usambazaji wa taarifa na video zenye mwelekezo wa kudhalilishana, vitendo hivi ni kinyume na kanuni ya Baraza"

Aidha ripoti ya taarifa hiyo imeendelea kueleza kuwa "Baraza linatoa onyo na kukemea vikali mienendo na vitendo hivi na kuwataka wahusika wote kuacha mara moja tabia hiyo, Baraza litachukua hatua kali kwa msanii yeyote atakayebainika kuendelea kutenda vitendo ambavyo ni kinyume na sheria na kanuni zinazosimamia sekta ya sanaa"




Share:

BASATA YATOA TAMKO SAKATA LA VIDEO ZA HOVYO ZINAZODAIWA KUWA ZA MSANII HARMONIZE


Picha ya msanii Harmonize

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limeingilia kati sakata la kusambazwa kwa video zisizo na maadili kwa msanii Harmonize kwa kutoa taarifa inayosema imesikitishwa na kitendo hicho kinachoendelea kwenye mitandao ya kijamii.

Aidha BASATA wametoa onyo na kukemea kwa vikali vitendo hivyo na kuwataka wahusika kuacha tabia hiyo na hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa msanii atakayebainika kuendelea kutenda vitu hivyo.

"Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) limesikitishwa na matukio na mienendo ya wasanii wa Tanzania kwenye mitandao ya kijamii kwa kushamiri vitendo vya matumizi ya lugha zisizo na staha, malumbano, kukashifiana na usambazaji wa taarifa na video zenye mwelekezo wa kudhalilishana, vitendo hivi ni kinyume na kanuni ya Baraza"

Aidha ripoti ya taarifa hiyo imeendelea kueleza kuwa "Baraza linatoa onyo na kukemea vikali mienendo na vitendo hivi na kuwataka wahusika wote kuacha mara moja tabia hiyo, Baraza litachukua hatua kali kwa msanii yeyote atakayebainika kuendelea kutenda vitendo ambavyo ni kinyume na sheria na kanuni zinazosimamia sekta ya sanaa"
Share:

Tangazo la Kazi : JAMBO GROUP OF COMPANIES INAHITAJI GRAPHIC DESIGNER


Share:

SERIKALI YAZINDUA BUCHA YA KUUZA NYAMA ZA WANYAMAPORI KATAVI


Na Israel Mwaisaka, TimesMajira,Online Katavi

SERIKALI ya Mkoa wa Katavi,leo imezindua rasmi bucha ya kuuza nyama ya wanyama pori ambapo imetangaza kuwa kilo mmoja ya nyama hiyo itakuwa ikiuzwa kwa bei ya sh. 8,000.

Mkuu wa Mkoa huo, Juma Homera amesema hatua hiyo imefanyika ikiwa pia ni kumuenzi Hayati Rais John Magufuli ambaye aliagiza kuanzishwa kwa bucha hizo hapa nchini ili kuwapa wananchi fursa ya kupata kitoweo hicho, sambamba na kupunguza vitendo vya ujangili.

Akizindua bucha hiyo, Homera amesema Hayati Magufuli alipokuwa mkoani Katavi ndipo alipotoa agizo la kuanzishwa kwa bucha hizo katika mikoa yenye hifadhi za taifa za wanyamapori, pamoja na mapori ya akiba kitendo kitakacho sababisha watu waliokuwa wakiingia ndani ya hifadhi na kufanya ujangili kupata kitoweo kuacha vitendo hivyo.

Aidha mkuu huyo wa Mkoa ametoa wito kwa wananchi wengine wenye nia ya kuanzisha bucha hizo kufuata utaratibu ili waweze kupata vibali vya kuanzisha bucha hizo ili wananchi wawe wanapata nyama za wanyama pori kirahisi na kuepuka kufanya ujangili.

Mkuu huyo wa Mkoa amesema kuwa katika kipindi hiki cha masika nyama katika bucha hiyo itakuwa ikipatikana mara tatu kwa wiki, lakini kipindi cha kiangazi itakuwepo kila siku kwani uwindaji utakuwa ukifanyika mara kwa mara.

Baada ya kuzindua bucha hiyo Serikali ya mkoa huo ilitumia fursa hiyo kuwafuturisha nyama hiyo ya pori baadhi ya wazee wa dini ya kiislaamu ambapo waliishukuru Serikali na kusema kuwa haijawahi kutokea katika mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani kufuturishwa kwa nyama za pori hii imekuwa ni mara ya kwanza kwao.

Kwa upande wake Meneja wa Pori la Akiba Rukwa (TAWA) Baraka Balagaye ametoa wito kwa yoyote ambaye anataka kufungua bucha ya nyama pori wao kama wasimamizi wa mapori ya akiba wapo tayari kutoa ushirikiano wa kutosha kufanikisha kufunguliwa mabucha ya kuuza nyama ya pori.



Share:

KUOTA NDOTO MBALIMBALI USIKU SIYO JAMBO ZURI NIMEGUNDUA LEO

 Asante Kiwangadoctors kwa huduma yenu nzuri huduma ambayo mlinipatia imeweza kubadilisha maisha yangu yote na kupata furaha ya usingizi ambayo nilikosa kwa miaka 10 iliyopita.

Najua wengi watanishangaa sana haswa nikigusia suala la usingizi, maana wengi kusema kuwa kitendo cha kulala ni sehemu moja wapo ya umaskini.

 Kweli ukilala sana ukapitiliza kamwe huwezi kufanikiwa ila kitendo cha kukosa usingizi usiku ni jambo ambalo ni baya sana katika afya zetu. 

Kitendo cha kukosa usingizi kinasababishwa na mambo mengi haswa unapolala kwa ajili ya kupumzisha ubongo na kujiandaa kwa ajili ya kesho yake.

Mimi naitwa Paul mkazi wa Mtwara hapa Tanzania,nimekutana na shida ya kukosa usingizi na kuota ndoto za kutisha usiku kwa miaka 10 iliyopita.

Kuna siku nilikuwa naota ndoto ambazo mimi mwenyewe nikishtuka kwa usingizi najaa hofu kubwa sana na mara nyingi kitu ambacho naota haipiti siku kama 3 hicho kitu nakiona kwa macho yangu.

 Jambo ambalo lilinisumbua sana ni pale ninapoamka asubuhi na kuhisi nimechoka mwili mzima jambo ambalo lilisababishwa nishindwe kabisa kufanya kazi yangu vizuri.

Nilikonda kiasi kwamba watu wengi walidhani kuwa nina ugonjwa ambao unanisumbua,kumbe ni ugonjwa wa ndoto ambazo zinasababisha mimi nisilale usiku kucha hali ya kuwa wenzangu wamelala.

Hiyo hali ilinifanya nianze kutafuta usaidizi kwa ajili ya kuepuka ndoto za kutisha muda mwingine kuota mtu anakufa na baada ya siku kadhaa hilo jambo kinatokea. 

Siku moja nikiwa Mtandaoni kwenye internet ndipo nilikutana na website ya Kiwangadoctors ambayo ni www.kiwangadoctors.com, niliweza tembelea website hiyo kwa makini zaidi nipo nikakutana na maelezo kuhusu kazi yao.

Nilipobonyeza kwa Upande wa spells nikagundua wanatatua shida mbalimbali na miongoni mwao kutatua shida za watu ambao wanakumbana na shida kama yangu.

Ndipo nilichukua namba ya Dr. Kiwanga ambayo ni hii +254 769404965.Niliongea na Dr. Kiwanga na kutoa shida ninazokumbana nazo usiku.

 Dr. Kiwanga aliniambia kuwa kabla hajatoa matibabu anauliza baadhi ya maswali hivyo niliulizwa maswali kidogo na kisha Dr akaniambia kuwa nisubiri kwa muda wa dakika 35 nitapata ujumbe wake.

Baada ya dakika 35 nilipokea ujumbe wa Dr kwenye WhatsApp, ujumbe ambao ulikuwa umeambatana na maelezo juu ya ndoto ambazo nilikuwa naota pamoja na chanzo cha hizo ndoto ni nini.

Kipindi nasoma maelezo ya Dr. Kiwanga aliyonitumia niliishiwa na nguvu kabisa maana ndoto niliyokuwa naota,ni ndoto ambazo zilikuwa zinanichukua katika ulimwengu mwingine nyakati za usiku na kunifanya niwe tofauti sana na watu wengine.

 Nilisoma vizuri na kumuuliza Dr. Kiwanga kuwa mimi nahitaji usaidizi wake ndipo Dr. Kiwanga akaniambia kulingana na shida yangu ni lazima kufika ofisini kwake Nakuru-Kenya.

Ukweli nilikuwa sijawai fika nchi jirani ya Kenya hivyo nilikuwa na uoga wa hapa na pale ila baada ya mwezi mmoja shida iliongezeka zaidi nipo nilimtafuta tena Dr ili niweze fika kwa ofisi yake kwa ajili ya usaidizi.

Nilijiandaa na kuanza safari ya kutoka hapa Tanzania na kuelekea Kenya. Kiwangadoctors walinipokea vizuri hadi kufika kwa ofisi japo nilikutana na watu wengi kutoka sehemu mbalimbali,ila nilivumilia na hatimaye nikaonana na Dr mhusika wa kazi yangu.

Nilipewa dawa za kutumia kwa ajili ya kuoga kwa siku tatu na tangu hapo sijawai pata tena ndoto zile ambazo zilininyima raha.

Katika mawasiliano yangu na Dr. mhusika ndipo niliweza fahamu kuwa kiwangadoctors wanatatua shida nyingi sana kwa ofisi yao kama kupata mpenzi,kurudisha mpenzi,kuleta furaha na amani katika familia,kusafirisha nyota na kupata dawa ya mvuto kwa mwanaume au mwanamke.

 Dr alizidi kuniambia kuwa wanatibu pia magonjwa sugu kama Sukari,Pressure kwa kutumia miti shamba.Wasiliana na Kiwanga doctors kwa namba +254 769404965 kwa ajili ya kupata ufumbuzi wa shida yako. Asante Kiwanga doctors.



Share:

SIMBA SC YAIKANDAMIZA MTIBWA SUGAR 5G


Mabingwa watetezi, Simba SC wamerejea na moto wao kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara na leo wameichapa Mtibwa Sugar 5-0 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Mabao ya Simba SC leo yamefungwa na nyota wa kigeni watupu, Wazambia Clatous Chama dakika ya tisa, Rally Bwalya dakika ya 19, Mnyarwanda Meddie Kagere dakika ya 43 na 52 na kiungo wa kimataifa wa Msumbiji, Luis Miquissone dakika ya 69.

Ushindi huo unaifanya Simba SC inayofundishwa na Mfaransa, Didier Gomes Da Rosa ifikishe pointi 49 baada ya kucheza mechi 21 na kurejea nafasi ya pili, ikizidiwa pointi mbili na vinara, Yanga SC ambao hata hivyo wamecheza mechi tatu zaidi.
Share:

WACHIMBAJI WANNE WAFARIKI KWA KUFUKIA NA KIFUSI MGODINI SIMIYU

Wachimbaji wanne katika mgodi wa dhahabu wa Namba Mbili uliopo kijiji cha Ilujamate Wilaya ya Busega Mkoa wa Simiyu wamefariki dunia baada ya kufukiwa na vifusi baada ya kuta za duara kuporomoka kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

Tukio hilo limetokea Aprili 12,2021 saa 4:25 usiku katika duara namba 18 na 17 AB na kusababisha vifo vya wachimbaji wanne na mwingine mmoja kujeruhiwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Richard Abwao amesema aliyejeruhiwa ni Mangu Ngumba (33) mkazi wa Matongo Wilaya ya Bariadi na waliopoteza maisha ni Limbu Kisabo (28) mkazi wa Mwakibuga Wilaya ya Bariadi na Tembo Male (42) mkazi wa Isanga Bariadi.

Wengine ni Benjamini Masaka (51) mkazi wa Katoro Geita na Musa Washa (37) mkazi wa Dutwa Bariadi.

Via Mwananchi
Share:

DKT. SUBI : TANZANIA TUPO VIZURI LAKINI TUSIBWETEKE TUENDELEE KUJIKINGA NA CORONA


 Mkurugenzi wa Huduma za Kinga Wizara ya Afya, Maendeleo ya Watoto, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.  Leonard Subi,akizungumza na washiriki wanaofanya tathmini ya mafanikio na changamoto katika utekelezaji wa kanuni za Afya za Kimataifa (International Health Regulations) katika kukabiliana na magonjwa ya mlipuko.

**

Mkurugenzi wa Huduma za Kinga kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Wazee na Watoto Dk. Leonard Subi amesema kuwa Tanzania ni mojawapo kati ya nchi zinazochukua tahadhari kubwa sana ya kupambana na magonjwa ya milipuko kama Corona.

Aliyasema hayo wakati akifungua kikao cha siku tatu kinachofanyika Jijini Arusha kilichoshirikisha wataalam mbalimbali, mashirika binafsi na wadau wa Afya  nchini.

"Tanzania tuko salama na wananchi wetu waendelee na maisha kama kawaida" alisema Dkt. Subi.

Vile vile Dkt. Subi ameendelea kusisitiza wananchi kuendelea kuchukua tahadhari zote za ugonjwa wa Corona ikiwemo utamaduni wa kunawa mikono kwa maji safi tiririka na sabuni, kuvaa barakoa kwa usahihi na kuepuka misongamano isiyo ya lazima. 

Aidha Dkt. Subi ametoa wito wa kuendelea kuyalinda makundi ya watu walio katika hatari ya kuathiriwa zaidi na ugonjwa wa Corona ikiwa ni makundi ya wazee pamoja na watu wenye magonjwa sugu kama Kisukari na presha.

Pia ameweka msisitizo kwa watanzania kuzingatia mtindo bora wa maisha ikiwa ni pamoja na kuzingatia mazoezi ya mwili na viungo na kuzingatia lishe bora ili kuongeza kinga za mwili katika kupambana maradhi ya kuambukiza pamoja na yale yasiyoambukiza.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger