Wednesday, 14 April 2021

Basata Watoa Onyo Kwa Wasani Kudhalilishana

...

 Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limeingilia kati sakata la kusambazwa kwa video zisizo na maadili kwa msanii Harmonize kwa kutoa taarifa inayosema imesikitishwa na kitendo hicho kinachoendelea kwenye mitandao ya kijamii.

Aidha BASATA wametoa onyo na kukemea  vikali vitendo hivyo na kuwataka wahusika kuacha tabia hiyo na hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa msanii atakayebainika kuendelea kutenda vitu hivyo.

"Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) limesikitishwa na matukio na mienendo ya wasanii wa Tanzania kwenye mitandao ya kijamii kwa kushamiri vitendo vya matumizi ya lugha zisizo na staha, malumbano, kukashifiana na usambazaji wa taarifa na video zenye mwelekezo wa kudhalilishana, vitendo hivi ni kinyume na kanuni ya Baraza"

Aidha ripoti ya taarifa hiyo imeendelea kueleza kuwa "Baraza linatoa onyo na kukemea vikali mienendo na vitendo hivi na kuwataka wahusika wote kuacha mara moja tabia hiyo, Baraza litachukua hatua kali kwa msanii yeyote atakayebainika kuendelea kutenda vitendo ambavyo ni kinyume na sheria na kanuni zinazosimamia sekta ya sanaa"




Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger