Friday 30 April 2021

Breaking : LAZARO NYALANDU AIKACHA CHADEMA NA KUREJEA CCM

...

Lazaro Nyalandu akitangaza kurejea CCM leo
**
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Kati, Lazaro Nyalandu ametangaza kurejea Chama Cha Mapinduzi akisema ameamua kurejea nyumbani.

Nyalandu ametangaza kurejea CCM leo Ijumaa Aprili 30,2021 wakati wa Mkutano Mkuu Maalum wa Chama Cha Mapinduzi Dodoma.

Mara baada ya kutangazwa na Rais wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama hicho Samia Suluhu Hassan kurejea CCM Nyalandu ametoa shukrani zake kwa Mwenyekiti wa Chama hicho,kumpokea ,kumsamehe na kumruhusu kumrejesha katika chama hicho.

“Watanzania wameona nyota yako wamejaa na furaha,Mungu akakuongoze uwepo wangu mbele yako na mkutano huu ni kielezo tosha wewe kuungwa mkono na watanzania wote,”amesema Nyalandu
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger