Wednesday, 4 November 2020

JUMUIYA YA MARIDHIANO YAMSHUKURU MUNGU UCHAGUZI KUFANYIKA KWA AMANI NA UTULIVU


Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano Tanzania, Sheikh Alhad Mussa akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dodoma, kumshukuru Mungu kwa Uchaguzi Mkuu wa Tanzania kufanyika kwa amani na utulivu. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Jumuia hiyo, Askofu Oswald Mlay na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Mkoa wa Dodoma, Askofu Evance Chande. PICHA NA RICHARD MWAIKENDA

Na Richard Mwaikenda, CCM Blog, Dodoma.

MWENYEKITI wa Tume ya Maridhiano Tanzania, Sheikh Alhad Mussa Salumu amewasihi watanzania kuendelea kumshukuru Mungu kwa wema aliowatendea baada ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania kufanyika kwa salama na amani.

Ameyazungumza hayo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dodoma leo, akiwa pamoja na wajumbe wa tume ya kitaifa ya maridhiano na wa mkoa wa Dodoma.

 Aidha, Sheikh Alhad Mussa amesema kuwa inatakiwa sasa baada ya uchaguzi kumalizika salama ni kuungana kuendelea kuiombea kwa Mungu serikali iliyoshinda iongoze vema.

"Tunashukuru Mungu Uchaguzi umeisha kwa amani na salama, kilicho mbele yetu ni kuungana kuendelea  kuiombea Mungu Serikali iliyopo madarakani ituongoze salama.

Katika chaguzi zote kuna kushinda na kushindwa, huwezi kukubalika na kila mmoja  haiwezekani, manabii wa Mwenyezi Mungu na hata Wacha Mungu hawakukubalika nao walipingwa, hii ni desturi ni jambo la kawaida,"amesema Sheikh Alhad. 

Ameshauri upande ambao haujaridhika usisababishe vurugu, bali ufuate taratibu zilizopo ikiwemo ya kisheria na hata jumuiya hiyo inaweza kuweka mambo sawa.

"Kubwa tunawaomba Watanzania Nchi yetu iendelee kuwa salama na utulivu, tunahitaji nchi yenye amani ili tuweze kufanya shughuli zetu kwa ukamilifu bila bughudha yoyote, tusijaribu kuchezea amani iliyopo, tutajuta, tuna mifano mingi ya nchi mbalimbali zilizochezea amani, kuirejesha ni ngumu sana."

Amesema viongozi wa Dini walimlilia sana Mungu ili Uchaguzi uvuke kwa salama na amani, hivyo inabidi kumshukuru Mungu  kwa wema wake  aliotutendea. na kwamba wakifanya hivyo Mungu atatuzidishia. 

Alimalizia kwa kutoa shukrani kwa viongozi wote walioiombea kwa Mungu  nchi wakati wa mlipuko wa ugonjwa wa corona na Uchaguzi Mkuu  na sasa iko salama hivyo tuendelee kumshukuru Mungu naye ataendelea kutusikiliza.
Share:

Picha : BARAZA LA WAFANYAKAZI LA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA SHINYANGA LAZINDULIWA RASMI


Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Timoth Sosoma akizungumza wakati akizindua Baraza la Wafanyakazi la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
 
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Timoth Sosoma amezindua rasmi Baraza la Wafanyakazi la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga ambalo litakuwa na jukumu la kujadili mikakati mbalimbali ya kuimarisha na kuboresha utendaji na uwajibikaji ndani ya hospitali utakaowezesha hospitali kutoa huduma kwa wananchi kwa haraka,uwazi,urahisi,gharama nafuu wakati wowote.

Uzinduzi huo umefanyika leo Jumatano Novemba 4,2020 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga na kuhudhuriwa na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga pamoja na viongozi wa Chama Cha Wafanyakazi (TUGHE) mkoa wa Shinyanga.

Akizindua Baraza hilo la Wafanyakazi, Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Timoth Sosoma amesema baraza hilo litakuwa chachu ya kuboresha huduma za afya katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga huku akiwasisitiza wajumbe kuwa waadilifu na kuzingatia maadili ya utumishi wa umma.

“Hiki ni kikao cha kwanza cha Baraza la Wafanyakazi tangu mabadiliko ya kuwa chini ya Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto. Mkiwa sehemu ya historia hii ni matumaini yangu kuwa nafasi mliyopewa mtaitumia vizuri kwa ajili ya kushauri namna bora ya kuboresha utendaji kazi na kujenga mahusiano baina ya Mwajiri na Mwajiriwa”,amesema Sosoma.

“Madhumuni ya kuundwa kwa mabaraza ya wafanyakazi ni kuishauri serikali kuhusu usimamizi wa kazi na rasilimali,utekelezaji wa majukumu,kulinda haki na wajibu wa Waajiri na Wafanyakazi,kutoa ushauri kuhusu kujenga hali bora za kazi na maslahi na kusimamia haki na ustawi katika sehemu za kazi”,ameongeza Sosoma.

Amesema Baraza la Wafanyakazi kama vyombo vya ushauri na usimamizi yana wajibu wa kuhakikisha kuwa waajiri na watumishi wanatambua wajibu na haki zao na wanazingatia maadili ya utumishi wao kuleta mabadiliko ya utendaji kazi yenye tija, staha na upendo.

“Maadili ni kitu muhimu cha kuzingatia katika utendaji kazi. Ni lazima kila mtumishi wa umma kujiepusha na vitendo vinavyoashiria ukosefu wa maadili kama vile rushwa,utovu wa nidhamu,utoaji wa siri za serikali na huduma mbaya kwa wagonjwa”,amesisitiza Sosoma.

Aidha amewataka wajumbe wa Baraza hilo kufanya vikao walau mara mbili kwa mwaka kwa mujibu wa sheria ili kuepusha fursa kwa wafanyakazi kukuza majungu mahala pa kazi na kwamba vikao hivyo havipaswi kupuuzwa hivyo viandaliwe katika viwango vinavyokidhi malengo na makusudio ya sheria.

Naye Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi la Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga, Dk. Rose Malisa amewaomba wajumbe wa baraza hilo kuzingatia majukumu yao ambayo ni pamoja na kuwashirikisha wafanyakazi wa serikali katika utekelezaji wa shughuli za hospitali kwa ushirikiano na uongozi wa hospitali na kuishauri Menejimenti juu ya ufanisi wa kazi na hatua zinazofaa kuchukuliwa kuboresha huduma za afya na maslahi ya wafanyakazi.

Aidha Dk. Malisa ambaye ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Shinyanga amewataka wajumbe wa baraza hilo kuwa chachu ya mabadiliko katika kuboresha huduma za afya katika hospitali na kuendelea kutoa elimu ya afya kwa jamii.

Kwa upande wake, Katibu wa Chama Cha Wafanyakazi (TUGHE) mkoa wa Shinyanga, Gaudensi Kadyango amewataka wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga kufanya kazi kwa bidii,kujipenda na kuwa mfano bora kwa watumishi wengine wa umma.

Aidha amewakumbusha watumishi wa umma kuzingatia maadili ya kazi yao ikiwa ni pamoja na kuepuka kutumia lugha mbaya kwa wateja na kuendekeza matumizi ya simu za mkononi wakati wa kazi.

 Uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi la Hospitali ya Rufaa mkoa wa Shinyanga umekwenda sanjari na uchaguzi wa  viongozi  Baraza hilo ambapo Clementina Salutari amechaguliwa kuwa Katibu na Allan Luvanda kuwa Katibu Msaidizi.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Timoth Sosoma akizungumza wakati akizindua Baraza la Wafanyakazi la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Novemba 4,2020 katika ukumbi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Timoth Sosoma akizungumza wakati akizindua Baraza la Wafanyakazi la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi la Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga, Dk. Rose Malisa ambaye ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Shinyanga akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga. Wa kwanza kushoto ni Katibu wa Chama Cha Wafanyakazi (TUGHE) mkoa wa Shinyanga, Gaudensi Kadyango akifuatiwa na Kaimu Mwenyekiti wa TUGHE mkoa wa Shinyanga, Rajabu Masanche akifuatiwa na Mwakilishi wa Mganga Mkuu mkoa wa Shinyanga, Timoth Sosoma.
Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi la Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga, Dk. Rose Malisa ambaye ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Shinyanga akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi la Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga, Dk. Rose Malisa ambaye ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Shinyanga akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Katibu wa Chama Cha Wafanyakazi (TUGHE) mkoa wa Shinyanga, Gaudensi Kadyango akitoa mada ya wajibu na majukumu ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga na umuhimu wa Chama cha Wafanyakazi.
Katibu wa Chama Cha Wafanyakazi (TUGHE) mkoa wa Shinyanga, Gaudensi Kadyango akiwasititiza watumishi wa umma kuzingatia maadili ya kazi wakati wa Uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Katibu wa Baraza la Wafanyakazi la Hospitali ya Rufaa mkoa wa Shinyanga, Clementina Salutari akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Afisa Utumishi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Beatrice Cheyo akitoa taarifa fupi ya Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga wakati wa Uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi la Hospitali ya Rufaa mkoa wa Shinyanga.
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini wakati wa Uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi la Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga, Dk. Rose Malisa, Wa kwanza kushoto ni Katibu wa Chama Cha Wafanyakazi (TUGHE) mkoa wa Shinyanga, Gaudensi Kadyango akifuatiwa na Kaimu Mwenyekiti wa TUGHE mkoa wa Shinyanga, Rajabu Masanche akifuatiwa na Kaimu Mganga Mkuu mkoa wa Shinyanga, Timoth Sosoma wakiwa kwenye uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Kulia ni Katibu Msaidizi wa Baraza la Wafanyakazi la Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga Allan Luvanda akifuatiwa na Katibu wa Baraza hilo, Clementina Salutari na Mwenyekiti wa Baraza hilo Dk. Rose Malisa. Wa kwanza kushoto ni Kaimu Mwenyekiti wa TUGHE mkoa wa Shinyanga, Rajabu Masanche. 
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini wakati wa Uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini wakati wa Uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.

Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini wakati wa Uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini wakati wa Uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini wakati wa Uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga wakiimba wimbo wa Mshikamano Daima ' Solidarity Forever' wakati wa Uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.

Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga wakipiga picha ya pamoja baada ya Uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.

Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga wakipiga picha ya pamoja baada ya Uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


Share:

Majaliwa Akagua Maandalizi Ya Uwanja Wa Jamhuri Dodoma utakaotumika kwa ajili ya uapisho wa Rais wa Tanzania

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, wakati akiwasili kwenye viwanja vya Jamhuri jijini Dodoma leo Novemba 4, 2020, kukagua maandalizi ya uwanja huo utakaotumika kwa ajili ya uapisho wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania utakaofanyika kesho Novemba 5, 2020.




Share:

Lukuvi Apokea Taarifa Ya Awali Ya Uhakiki Eneo La Mgogoro Mtakuja Dodoma


Na Munir Shemweta, WANMM DODOMA
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amepokea taarifa ya awali ya uhakiki wa eneo lenye Mgogoro la Mtakuja lilipo Kata ya Chang’ombe mkoani Dodoma.

Taarifa ya uhakiki wa eneo hilo lenye ukubwa hekta kumi uliwasilishwa leo tarehe 4 Oktoba 2020 katika ofisi za Wizara eneo la Mtumba jijini Dodoma na Kamishna Msaidizi wa Ardhi Uratibu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Wilson Luge kwa niaba ya timu inayofanya uhakiki kwa wakazi wanaoishi eneo hilo.

Uwasilishaji taarifa hiyo unafuatia kukwama kwa mara kadhaa mazoezi yaliyofanyika huko nyuma na kusababisha Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi kuelekeza kufanyika uhakiki mwingine ili kutafuta suluhu ya kudumu ya mgogoro wa muda mrefu kwenye eneo hilo.

Kwa mujibu wa Kmaishna Msaidizi wa Ardhi Uratibu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Wilson Luge, tayari timu ya uhakiki mgogoro huo imeshawapitia wananchi 750 kati ya 1,025 watakaofanyiwa uhakiki.

Luge alisema, kazi kubwa inayofanywa na timu ya uhakiki ni kupitia taarifa ya kila mwananchi na kuangalia hali ya maendelezo yaliyofanyika katika kila eneo la mwananchi analomiliki.

Mazoezi ya uhakiki eneo la Mtakuja Kata ya Chang’ombe mkoa wa Dodoma yamefanyika mara kadhaa katika miaka ya 2005, 2008 na 2015 ambapo zoezi linaloendelea sasa linatarajiwa kuleta suluhu ya mgogoro huo.

Uwasilishwaji taarifa ya uhakiki wa mgogoro wa eneo la Mtakuja Dodoma, ulihudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde, Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mary Makondo, Naibu wake Nocolaus Mkapa, Kamishna wa Ardhi Nathaniel Nhonge na Watendaji wa Wizara, Jiji la Dodoma pamoja na wa Kata ya Chang’ombe.


Share:

Donald Trump Alalamika Kuibiwa Kura....Kasema Ataenda mahakamani kuzuia kuendelea kuhesabiwa kwa kura


Rais Donald Trump amedai kushinda uchaguzi wa Marekani licha ya kwamba matokeo ya mwisho bado hayajatangazwa, na amesema atakwenda Mahakama ya Juu kupinga kuendelea kuhesabiwa kwa kura. 

Trump amedai ushindi huo katika hotuba isiyo ya kawaida akiwa ikulu ya White House, na kuongeza kuwa kuendelea kuhesabiwa kwa kura ni njama ya kufanya udanganyifu. 

Mrepublican huyo ambaye matokeo ya awali yanamuonesha akiwa katika mchuano mkali na Mdemocrat Joe Biden, amesema atakwenda mahakamani na anataka upigaji kura wote kusimama - akionekana kumaanisha kusitisha kuhesabiwa kwa kura za posta, ambako kunaweza kuruhusiwa kisheria na bodi za uchaguzi za majimbo baada ya uchaguzi wa Jumanne iwapo zilikuja kwa wakati.

 Suala hilo linaweza kugeuka nyeti katika majimbo ambayo yanaendelea kuhesabu kura katika kinyang'anyiro hicho kikali. 

Timu ya kampeni ya Joe Biden imekosoa matamshi hayo ya Trump na kuyataja kuwa kashfa, na baadhi ya wanachama wa chama chake cha Repulican pia wameikosoa hatua hiyo.



Share:

DC Kiswaga: Baada ya uchaguzi tugeukie kilimo


Samirah Yusuph,
Bariadi. Baada ya kukamilika kwa mchakato wa uchaguzi mkuu na hatmaye kupatikana kwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, wabunge pamoja na madiwani, wananchi wameshauriwa kugeukia shughuli zao za kiuchumi.
 
Ushauri huo umetolewa na mkuu wa wilaya ya Bariadi Festo Kiswaga, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake.

Ambapo wananchi wametakiwa kujikita katika shughuli zao za kila siku ili kujiongezea kipato kwani sasa ni msimu wa kilimo na wakati wa maisha baada ya uchaguzi hivyo ni muda kuendelea na shughuli za kilimo.

Huku akiwataka wananchi kuendana na mabadiliko ya hali ya hewa kwa kulima zao la Pamba kwa wingi kutokana na taarifa za mamlaka ya hali ya hewa kutoa taarifa ya uwepo wa mvua chache kwa mwaka huu.

Kiswaga alisema msimu wa mvua chache ni msimu mzuri kwa wakulima wa zao la Pamba kwani uzalishaji wake unakuwa ni mkubwa kutokana na zao hilo kutokuhitaji mvua nyingi hivyo wananchi watumie nafasi hiyo katika kuongeza uzalishaji na kuongeza kuwa:

"Tayari pembejeo za kilimo cha pamba zimefika katika ofisi za ushirika hivyo wananchi wafike kwa ajili ya kuchukua mbegu ili kazi iendelee kama kawaida".
 
Mwisho.


Share:

Uchaguzi wa Marekani 2020: Mchuano bado mkali kati ya Trump-Biden


Matokeo ya awali ya urais nchini Marekani kati ya Donald Trump na hasimu wake wa Democrat Joe Biden yanaonesha mchuano kuwa mkali katika majimbo kadhaa.

Donald Trump anaongoza katika jimbo la Florida kwa karibu kura zote zilizohesabiwa.

Lakini majimbo mengine ya Georgia, Pennsylvania, Wisconsin, Michigan, Arizona, Ohio, Texas, na North Carolina chochote kinatarajiwa.

Zaidi ya watu milioni 100 walikwisha piga kura zao za mapema.

Udhibiti wa Congress pia uko hatarini. Pamoja na Ikulu ya White House, Republican wanawania kupata idadi kubwa ya viti vya Seneti.

Bunge la wawakilishi linatarajiwa kuwa katika mikono ya Democratic.


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano November 04



Share:

Tuesday, 3 November 2020

Country Manager at Adexen

Country Manager Adexen Dar es Salaam, Tanzania Adexen was mandated by a leading international Group to recruit a Country Manager for its operations. The position is based in Tanzania. Only applications through Adexen website will be considered for this job vacancy. Responsibilities Responsible for overall direction, development and growth of the Company in the Country […]

The post Country Manager at Adexen appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

PLANNING AND CONSTRUCTION ENGINEER II at SHUWASA

POST PLANNING AND CONSTRUCTION ENGINEER II – 1 POST POST CATEGORY(S) ENGINEERING AND CONSTRUCTION EMPLOYER Shinyanga Urban Water Supply and Sewerage Authority, (SHUWASA) APPLICATION TIMELINE: 2020-11-02 2020-11-16 JOB SUMMARY Responsible for planning, designing and Construction of water and sewer Networks. DUTIES AND RESPONSIBILITIES i. Data collection. Analysis, system design and preparation of procedures for urban […]

The post PLANNING AND CONSTRUCTION ENGINEER II at SHUWASA appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

WATER SUPPLY ENGINEER II at SHUWASA November, 2020

POST WATER SUPPLY ENGINEER II – 1 POST POST CATEGORY(S) ENGINEERING AND CONSTRUCTION EMPLOYER Shinyanga Urban Water Supply and Sewerage Authority, (SHUWASA) APPLICATION TIMELINE: 2020-11-02 2020-11-16 JOB SUMMARY RESPONSIBLE FOR WATER DISTRIBUTION WORKS DUTIES AND RESPONSIBILITIES i. To supervise all water network maintenance and development plans activities in accordance with systems procedures agreed with the […]

The post WATER SUPPLY ENGINEER II at SHUWASA November, 2020 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

WATER QUALITY TECHNICIAN II at SHUWASA

POST WATER QUALITY TECHNICIAN II – 1 POST POST CATEGORY(S) WATER, MINING AND NATURAL RESOURCES EMPLOYER Shinyanga Urban Water Supply and Sewerage Authority, (SHUWASA) APPLICATION TIMELINE: 2020-11-02 2020-11-16 JOB SUMMARY NA DUTIES AND RESPONSIBILITIES i. To interpret, build upon, and comply with company quality assurance standards; ii. To carefully maintain complaint and nonconformance processing through […]

The post WATER QUALITY TECHNICIAN II at SHUWASA appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

MECHANICAL TECHNICIAN (MECHATRONICS) II at SHUWASA

POST MECHANICAL TECHNICIAN (MECHATRONICS) II – 1 POST POST CATEGORY(S) ENGINEERING AND CONSTRUCTION EMPLOYER Shinyanga Urban Water Supply and Sewerage Authority, (SHUWASA) APPLICATION TIMELINE: 2020-11-02 2020-11-16 JOB SUMMARY NA DUTIES AND RESPONSIBILITIES i. To carryout inspection of plant, machines and equipment in accordance with laid down procedures; ii. To participate in repair and maintenance of […]

The post MECHANICAL TECHNICIAN (MECHATRONICS) II at SHUWASA appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

HEAD OF PROCUREMENT MANAGEMENT UNIT at SHUWASA

POST HEAD OF PROCUREMENT MANAGEMENT UNIT – 1 POST POST CATEGORY(S) PROCUREMENT & LOGISTIC MANAGEMENT EMPLOYER Shinyanga Urban Water Supply and Sewerage Authority, (SHUWASA) APPLICATION TIMELINE: 2020-11-02 2020-11-16 JOB SUMMARY OTHER COMPETENCIES Must have Strong negotiation and analytical presentation skills. DUTIES AND RESPONSIBILITIES i. To manage all procurement and disposal by tender activities of the […]

The post HEAD OF PROCUREMENT MANAGEMENT UNIT at SHUWASA appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Sales Representative at Raha Beverages ltd

Sales representatives are responsible for selling a company’s products. Sales representatives are responsible for selling a company’s products by identifying leads, educating prospects on products through calls, trainings, and presentations, and providing existing customers with exceptional support. Qualification & Experience Holder of diploma or equivalent in sales management from a recognize institution. Must have valid […]

The post Sales Representative at Raha Beverages ltd appeared first on Udahiliportal.com.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger