Tuesday, 5 May 2020

DIWANI AISHUKURU KAMPUNI YA GP KWA KUWASAIDIA VIFAA VYA KUJIKINGA NA CORONA

  Mmiliki wa Kampuni ya SSMC Limited Saidi Mohamed kushoto akimkabidhi vyakula vya futari na vifaa vya kujikinga na Ugonjwa wa Corona Diwani wa Kata ya Makorora Omari Mzee vyenye thamani ya milioni 16 vilivyotolewa na Kampuni ya Mafuta ya GP mapema leo kushoto ni Afisa Mtendaji wa Kata ya Makorora Ramadhani Badi
 Diwani wa Kata ya Makorora Omari Mzee kushoto akibidhi mmoja wa wananchi wa Kata ya Makorora Futari yenye thamani ya milioni 16 vilivyotolewa na Kampuni ya Mafuta ya GP mapema leo ikiwemo vifaa vya kujikinga na Virusi vya Corona
 Diwani wa Kata ya Makorora Omari Mzee kulia akikabidhiwa vitakasa mikono (Sanitize ) na vyakula kutoka kwa  Mmiliki wa Kampuni ya SSMC Limited Saidi Mohamed vyenye thamani ya milioni 16 vilivyotolewa na Kampuni ya Mafuta ya GP mapema leo
 Diwani wa Kata ya Makorora Omari Mzee kulia akigawa msaada huo kwa wananchi wa mitaa mbalimbali kwenye Kata hiyo kulia ni  Mmiliki wa Kampuni ya SSMC Limited Saidi Mohamed

 Mmiliki wa Kampuni ya SSMC Limited Saidi Mohamed akiwaaonyesha waandishi wa habari vitakasa mikono ambavyo vimetolewa


DIWANI wa Kata ya Makorora Jijini Tanga (CCM) Omari Mzee ameishukuru Kampuni ya Mafuta ya GP kwa kutoa msaada futari kwa kaya 150 kwenye kata yake ikiwemo vifaa vya kujikinga na ugonjwa wa Virusi vya Corona.


Huku akiwataka wazazi na walezi kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele kuwaelimisha watoto wao ili kuona ile mikusanyiko isiyokuwa ya lazima waweze kuepukana nayo ikiwa ni mkakati wa kukabiliana na Ugonjwa wa Virusi vya Corona ambayo kwa sasa vinaitikisha dunia.

Omari aliyasema hayo leo wakati akipokea msaada huo wenye thamani ya Milioni 16 vilivyotolewa na kampuni ya Mafuta ya GP vilikabidhiwa na Mmiliki wa Kampuni ya SSMC Limited Saidi Mohamed kufuatia ombi la kumtaka ashirikiana nao kwenye kukabidhi vyakula na vifaa hivyo..

Alisema vifaa hivyo vitawasaidia wakati huu wa mwezi wa ramadhani ikiwemo katika kukabiliana dhidi ya Ugonjwa huo wa Corona huku akiwataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari ambazo zimekuwa zikitolewa na wataalamu wa Afya hapa nchini.

Aidha alisema kwa sasa shule zimefungwa na watoto wamekuwa wakizagaa mitaani hivyo wanapaswa kuchukua tahahdari kwa kuwaelimisha ili kuona ile mikusunyiko ilisyokuwa ya lazima waweze kuepukana nayo kwa lengo la kuwaepusha na maambukizi ambayo wanaweza kukumbana nayo.

“Nishukuru sana kwa furari hii kwa zile kaya ambazo hawajiwezi zitawasaidia kupunguzia makali ya maisha lakini wazazi tutambue ugonjwa huu wa Virusi vya Corona upo hivyo niwasihi wazazi na jamii nzima kwa ujumla tuweza kuchukua tahadhari kukabiliana nao “Alisema Diwani huyo.

Awali akizungumza kabla ya makabidhiano hayo Mkurugenzi wa Kampuni ya SSMC Limited Saidi Mohamed alisema kwamba wamekabidhi vyakula hivyo kwenye kaya masikini 150 ambavyo vimetolewa na kampuni.


Ambapo alisema kutokana na ukongwe wangu wa kampuni za Oili Mkoa wa Tanga wamemuomba washirkiane nami kukabidhi vyakula hivyo kwa waliofunga mwezi mtufuku na vifaa vya kujikinga dhidi ya Corona vyenye thamani ya milioni 16.

Vifaa hivyo alivikabidhi kwa diwani wa Kata hiyo Omari Mzee ili aweze kuvikabidhi kwa wananchi kwenye mitaa ili kuweza kuwapunguzia makali ya maisha waliokuwa nao baadhi ya jamii maeneo hayo kutokana na kushindwa ukata ambao wamekuwa wakikumbana nao.
Share:

Kenya Yarekodi Idadi Kubwa Zaidi Ya Maambuzi ya Corona Ndani Ya Saa 24....Maambukizi Sasa Yamefika 535

Waziri wa Afya  nchini Kenya Mutahi Kagwe almetangaza kwamba visa vya maambukizi ya corona  nchini humo  vimefika 535 baada ya watu 45 zaidi kupatikana na maradhi hayo. 

Kwenye hotuba yake kwa vyombo vya habari leo Jumanne, Mei 5, Kagwe amesema hii ni idadi kubwa zaidi kuwahi kurekodiwa tangu kisa cha kwanza cha COVID-19 kuripotiwa Machi 13, 2020. 
 
Kati ya visa hivyo 45, 30 ni wanaume na 15 ni wanawake. Mutahi amesema kwamba watu 29 ni wakaazi wa Nairobi, 11 kutoka Mombasa na watano kutoka Wajir.


Share:

Ndege iliyobeba vifaa vya kupambana na corona yaanguka na kuua 6 Somalia

Watu sita wameaga dunia katika ajali ya ndege ya mizigo iliyokuwa imebeba misaada na vifaa vya kupambana na janga la corona katika mji wa Bardale, kusini mwa eneo la Bay nchini Somalia.

Shirika la Habari la Somalia limetangaza kuwa, ndege hiyo ni ya shirika la African Express Airways yenye makao makuu yake katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi na kwamba ilianguka jana katika mji huo, ikiwa njiani kuelekea Baidoa ikitokea mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.

Mohamed Salad, Waziri wa Uchukuzi wa Somalia ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa, sita waliopoteza maisha katika ajali hiyo ni rubani na msaidizi wake, rubani mwanagenzi, mhandisi wa ndege pamoja na wahudumu wawili.

Msemaji wa serikali ya Somalia, Ismael Mukhtar Omar amethibitisha kuwa, ndege hiyo ndogo ya Kenya iliyokuwa imebeba watu sita ilianguka jana kusini magharibi mwa Somalia wakati wa kutua. Vyombo vya usalama vya Somalia vinachunguza chanzo cha ajali hiyo.

Duru za habari zimearifu kuwa, ingawaje kuna uwepo wa kundi la kigaidi la al-Shabaab katika mji huo wa Bardale, lakini eneo palipotea ajali hiyo hususan uwanja wa ndege wa  Bardale unalindwa vikali na askari wa Somalia wakishirikiana na wanajeshi wa Ethiopia.

Baadhi ya ripoti zinadai kuwa, ndege hiyo iliyokuwa imebeba misaada ya kibinadamu ilitunguliwa kimakosa na askari wa jeshi la Ethiopia wanaofanya chini ya mwavuli wa Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Afrika AMISOM.


Share:

Video: Baba Levo Ft. Zitto Kabwe – Corona

Video: Baba Levo Ft. Zitto Kabwe – Corona


Share:

Shirikisho la soka nchini (TFF) Wafunguka Kuhusu Kurejea Kwa Michuano ya Ligi Kuu

Shirikisho la soka nchini (TFF), limeweka wazi kuwa linashirikiana na Bodi ya Ligi (TPLB), kuhakikisha ligi kuu inarejea, lakini bado mchakato huo ni wa ndani kwani unategemea tamko la serikali juu ya mwenendo wa janga la Corona.

Taarifa ya TFF leo Mei 5, 2020 imeeleza kuwa mchakato wa ndani kati ya shirikisho na Bodi pamoja na wadau ikiwemo vilabu unaendelea


Share:

Visa Vya Corona Uganda Vyafikia 97...... Rais Museveni Alegeza Baadhi Ya Masharti

Rais Yoweri Museveni ametangaza kuwa kuvaa barakoa ni jambo la lazima nchini humo kuanzia leo katika kipindi hiki ambacho marufuku ya kutotoka nje imelegezwa kidogo.

Hatua hiyo ilitangazwa jana Jumatatu usiku ambapo rais Museveni alihutubia taifa baada ya kumaliza siku 35 za marufuku ya kutotoka nje ama 'lockdown'.

Museveni amesema watu wanaweza kuvaa barakoa ambazo zimeshonwa kienyeji na vitambaa.

Katika hatua nyingine, Museveni amesema kuwa kuruhusu shughuli kuendelea kama awali inabidi kufanyike kwa umakini na mpangilio ili kuzuia virusi kusambaa kwa kasi.

Kwa kuanzia, ameruhusu maduka ya jumla, karakana za kukarabati magari, maghala kufunguliwa. Pia ameruhusu wafanyakazi wa bima na idadi ndogo ya wanasheria kurejea kazini.

Masharti mengine yaliyosalia ya marufuku ya awali bado yanaendelea mathalani kufungwa kwa mipaka ya nchi, kutoruhusu usafiri binafsi na wa umma, mikusanyiko ya watu na marufuku ya kutotoka nje usiku bado yangalipo kwa kipindi kingine cha siku 14.

Museveni amesema hatua hizo mpaka sasa zimetoa mafanikio ambayo ni kuzuia kusambaa kwa kasi kwa virusi hivyo.
 
Idadi mpya ya maambukizi kufikia leo asubuhi nchini humo imeongezeka kutoka 89 mpaka 97.

Kati ya wagonjwa hao, Waganda ni 57. Mpaka kufikia Jumatatu, madereva 30 wa malori walikuwa wamekutwa na corona nchini humo, kati yao Wakenya 13 na Watanzania 12.


Share:

WHO: Ushahidi Tulionao Unaonesha Virusi Vya Corona Vilitoka Kwa Wanyama

Msemaji wa Shirika la afya duniani (WHO) Bibi Fadela Chaib jana kwenye mkutano na waandishi wa habari amesema, kwa mujibu wa ushahidi uliopo sasa, WHO inaamini kuwa virusi vya Corona vinatoka kwa wanyama.

“Ushahidi wote tulionao unaonesha kuwa virusi vya Corona vinatoka kwa wanyama, na havitokani na uingiliaji wa binadamu au kutengenezwa kwenye maabara.”

Vilevile amesema WHO inapambana na maambikizi ya virusi pamoja na uvumi. 
 
“WHO inapambana na kuenea kwa virusi vya Corona duniani, wakati huo huo inapambana na kuenea kwa habari feki duniani. Wakati virusi vipya kama virusi vya Corona vinapotokea, habari nyingine feki huenea kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.”- Alisema


Share:

Viongozi Rukwa waendelea kuhamasisha matumizi ya Nyungu( Kujifukiza)

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ametoa wito kwa wananchi na wadau wote mkoani humo kuhakikisha wananchukua hatua za tahadhari ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona (Covid-19) kwa kufuata maelekezo ya wataalamu wa Afya pamoja na kushauri matumizi ya Nyungu kwaajili ya kujifukiza.

Amehamasisha hayo ikiwa ni katika kuunga mkono kauli ya Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) pamoja na viongozi wengine wa juu nchini katika kupambana na Covid – 19 ambao huenezwa kwa kuingiwa na majimaji yatokayo kwa njia ya hewa wakati mgonjwa anapokohoa au kupiga chafya au kugusa majimaji yanayotoka puani mwa mtu aliyeathirika.

“Nitoe wito kwa wadau wote ikiwa ni pamoja na nyini waheshimiwa madiwani kuchukua hatua za tahadhari ya ugonjwa huu kwa kufuata maelekezo ya wataalamu wetu wa afya. Tukumbuke kuwa virusi vya Corona ni janga la kidunia na linaua, Aidha matumizi ya Nyungu kwaajili ya kujifukizia yanashauriwa na Mh. Jafo waziri wa OR-TAMISEMI pamoja na viongozi wengine wa juu tuyazingatie, watu wapige Nyungu,” Alisisitiza.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Nkasi ambaye pia anakaimu Wilaya ya Sumbawanga Mh. Said Mtanda akifafanua michanganyiko ya aina tatu inayoshauriwa na wataalamu wa tiba ya asili yaliyofanyiwa majaribio na kituo cha Tiba asili kinachotambulika na serikali amesema moja ya mchanganyiko ni kutumia mti wa mwarobaini, tangawizi iliyopondwa, majani ya mpera, limao zilizokatwa  unachemsha pamoja na kisha kujifunika na kuvuta moshi kwa pua na mdomo ili moshi huo uingie mwilini na hatimae kwenda kuua virusi vya Corona.

“Sisi kule Namanyere (Wilayani Nkasi) tumeweka utaratibu wa kuhamasishana kujifukiza, kwasababu ukiona aibu matatizo kweli utayapata, kwahiyo kiongozi ukiwa unajifukiza unakapiga kapicha kidogo unawatumia wengine ili waseme hee hata Diwani kajifukiza, kwahiyo wale unaowaongoza watahamasiska kujifukiza kwasababu wataona kumbe sasa hili sio suala la aibu,” Alisema.

Viongozi hao wamesema hayo wakati wa vikao vya madiwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo na Wilaya ya Sumbawanga katika vikao vya Mabaraza ya Madiwani ya Halmashauri hizo kuhusu utekelezaji wa hoja za ukaguzi na mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali nchini.




Share:

HII NDIYO MADAGASCAR NCHI ILIYOTANGAZA KUWA NA DAWA YA CORONA...WANANCHI WAKE WANAAMINI KATIKA NGUVU ZA MABABU NA MIZIMU


Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
MADAGASCAR imekua nchi ya kwanza barani Afrika kutangaza dawa ya asili inayotibu virusi vya Corona ambapo Rais wa nchi hiyo Andry Rajoelina aliwataarifu wananchi juu ya uimara wa dawa hiyo na Mei 03, 2020 Rais wa Tanzania Dkt. John Joseph Magufuli aliuhakikishia umma juu ya Serikali ambayo hailali kwa Kuhakikisha wananchi wote wanakua salama na kueleza kuwa yupo tayari kutuma ndege nchini Madagascar ili kuleta dawa ambayo itawasaidia watanzania waliopatwa na homa hiyo ya mapafu (Covid -19) inayosababishwa na virusi vya Corona.

Mambo yanayovutia kuhusu Madagascar ni haya;
Inajulikana rasmi kama Jamhuri ya Madagascar, ikiwa nchi ya kisiwa (katika bahari ya Hindi kwa Pwani ya Afrika Mashariki) na ni kisiwa cha nne kwa ukubwa duniani.

Kuanzia mwaka 1895 ilitawaliwa na Ufaransa na ikawa nchi huru 1960 na kuitwa Jamhuri ya Malagasy na baadaye 1975 ikawa Jamhuri ya Demokrasia ya Madagascar na mwaka1993 ikawa Jamhuri ya Madagascar huku Mji mkuu wa Madagascar ni Antananarivo ukiwa na watu wapatao milioni 2.

Lugha rasmi nchini humo Malagasy na Kifaransa, na inakadiriwa kuwa na wakazi zaidi ya milioni 25.

Wananchi wengi wa Madagascar wanaamini katika mizimu na miiko hata katika wakati huu wa sayansi na teknolojia na imeelezwa kuwa wakazi wengi nchini humo ni wakristo (dini ililetwa na wamisionari) lakini bado wanaamini katika nguvu za mababu, uchawi, mizimu na miiko; wengi wao huwazika wapendwa wao katika mapango wakiwa katika majeneza na baadaye kufanya sherehe na masalia ya mifupa hiyo na hata kupiga nayo picha.
Pia imeelezwa kuwa nchi hiyo ina zaidi ya aina 10,000 ya mimea ya dawa asili huku asilimia 90 ikiwa zimefanyiwa utafiti na zinapatikana katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo.

Mlima mkubwa zaidi nchini humo ni Maromokotro wenye mita 2876 na kubwa zaidi ni kwamba viumbe 250,000 vinavyopatikana nchini humo havipatikani sehemu nyingine duniani na hii ni pamoja na mimea ya asili 14,000 inayopatikana Madagascar ambayo haipatikani sehemu nyingine duniani. 
Tafiti zinaonesha kuwa asilimia 50 za idadi ya vinyonga duniani wanapatikana Madagascar ikiwa ni pamoja na vinyonga wakubwa zaidi, huku aina 156 za vinyonga wanaopatikana ulimwenguni nusu yake wanapatikana Madagascar.


Pia Madagascar imepambwa na miti ya mibuyu, miti yenye umbo la chupa, miti iliyoelekeza mizizi angani na vivutio vingi vya kiasili.
SOMA ZAIDI <HAPA>
Via Michuzi blog
Share:

Wafanyabiashara Wanaouza Sukari Kwa Bei Ya Juu Jijini Dar Es Salaam Kuanza Kukamatwa Kuanzia Leo

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amesema kuanzia leo mkoa wake utawakamata wafanyabiashara wanaouza sukari kinyume cha bei elekezi isiyozidi Sh. 2,600 kwa kilo.

Amesema katika ukaguzi wao huo, sukari itakayokamatwa inauzwa kinyume cha maelekezo ya serikali, itataifishwa huku wahusika wakikamatwa.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Makonda alisema amebaini baadhi ya wafanyabiashara wanauza kilo moja ya sukari kwa Sh. 3,500 badala ya Sh. 2,600 iliyoelekezwa na Wizara ya Kilimo.

Kutokana na hilo, amewaagiza wakuu wa wilaya zote tano mkoa huo kuhakikisha wanafanya ukaguzi wa kuwabaini wafanyabiashara hao ili wakamatwe na sukari hiyo itaifishwe.

Makonda alisema hakuna sababu ya kutumia mwezi wa Ramadhani kuwakandamiza watu.
 
Makonda alisema uongozi wa mkoa huo utaichukua sukari hiyo na kuiuza kwa bei elekezi na fedha itakayopatikana ikatumika kununua vifaa vya kuwakinga madaktari wa Mkoa wa Dar es Salaam.


Share:

MWANAMKE MWENYE LIPS KUBWA DUNIANI ACHOMA SINDANO 20 ASIDI AONGEZE UKUBWA ZAIDI


Andrea Ivanova aliyeongeza lips

Mwanamke Andrea Ivanova mwenye miaka 22 kutokea nchini Bulgaria, amesema ameongeza lips za mdomo wake ambapo siku ya Aprili 28, amechomwa sindano 20 za Asidi ya Hyaluronic ili kuongeza lips hizo.

Mwanamke huyo ambaye ni mwanafunzi wa falsafa "Philosophy" amekuwa ni mmoja kati ya watu wenye lips kubwa duniani, amesema ataendelea kuongeza lips zake mpaka pale atakapo ridhika.

Akizungumzia suala hilo la kuongeza lips zake amesema "Nazipenda sana lips zangu, nilipata ugumu kwenye kula kwa siku mbili hadi tatu baada ya kuchomwa sindano ila sasa hivi sipati ikwazo vyovyote, madaktari wamesema inatosha ila mimi nataka kubwa zaidi ila itabidi nisubiri angalau kwa miezi miwili".

Andrea Ivanova amesema alianza kufanya mabadiliko ya lips za mdomo wake mwaka 2018, na anatumia Tsh 386,258 kwa kila matibabu, hadi hakumbuki jumla ya gharama zote alizotumia kwenye lips zake.


Chanzo : Daily Mail
Share:

WABUNGE WA CHADEMA WAKIUKA MAAGIZO YA MWENYEKITI WAO FREEMAN MBOWE YA KUTOHUDHURIA BUNGENI


Wabunge wanane wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), jana walikaidi maagizo ya Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, kuwataka kutohudhuria vikao vya bunge na kujitenga kwa siku 14.

Wabunge hao na majimbo yao kwenye mabano ni Joseph Selasini (Rombo), Peter Lijualikali (Kilombero), David Silinde (Momba), Antony Komu (Moshi Vijijini), Susan Masele (Viti Maalum), Jaffary Michael (Moshi Mjini), Latifa Chande na Subrina Sungura (Viti Maalum).

Wabunge hao walihudhuria mkutano wa 18 wa kikao cha 21 cha Bunge la 11, kilichojadili na kupitisha makadirio ya bajeti ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na walikuwa katika ukumbi wa Msekwa na ukumbi mkuu wa Bunge.

Mbunge Selasini wiki iliyopita alilalamika bungeni kwa kuondolewa kwenye kundi songezi la wabunge wa Chadema na kushindwa kuchangia mjadala wowote tangu kuanza kwa bunge, hadi alipopitia kwa Spika, Job Ndugai.

Aidha, siku iliyofuata Selasini alitangaza kuendelea kuwa mbunge, lakini hana mpango wa kugombea kupitia Chadema, bali NCCR- Mageuzi, Oktoba mwaka huu.

Februari mwaka huu, Komu alitangaza kuwa atagombea ubunge jimbo hilo, na kwamba wakati ukifika atagombea kupitia NCCR- Mageuzi.


Share:

MSHUMAA WAUNGUZA NYUMBA NA KUUA WATOTO


Watoto wawili wamefariki Dunia kufuatia kuungua moto kwa nyumba waliyokuwa wakiishi, katika mtaa wa Makuburi Ubungo jijini Dar es salaam. 

Akizungumza na EA Radio Mwenyekiti wa Mtaa Makuburi, Moshi Kaftany amesema chanzo cha moto inadaiwa ni mshumaa.

Kaftany amesema kuwa "moto umetokea usiku wa kuamkia leo na wajukuu zangu wawili wamefariki, bahati mbaya zaidi, hakuna hata mpangaji aliyefanikiwa kuokoa chochote"

Share:

TANZIA: Mwanasheria na Mwanasiasa mkongwe Dk. Masumbuko Lamwai Afariki Dunia

Mwanasiasa na mwanasheria mkongwe, Dkt. Masumbuko Lamwai amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Mei 5, 2020.

Dkt. Lamwai aliwahi kuwa mbunge wa Ubungo (NCCR-Mageuzi) kabla ya kuhamia CCM na kisha  kuwa mbunge wa kuteuliwa na Rais Benjamin Mkapa.

‪Kabla ya kifo chake, Dkt. Lamwai alikuwa Mhadhiri Mwandamizi (Senior Lecture) katika Chuo Kikuu cha Tumaini akifundisha masomo ya Sheria.

Dkt. Lamwai atakumbukwa kama Mwanasiasa machachari, mwanasheria nguli na mkufunzi mwandamizi (senior lecturer) wa Tumaini University.

Akiwa NCCR-Mageuzi, alikuwa na wanasiasa wengine wakongwe kama Mabere Marando, Marehemu Dk Sengondo Mvungi(RIP), Augustine Mrema, Makongoro Nyerere, Prince Bagenda, Ndimara Tegambwage, Stephen Wassira na wengine wengi.

Katika uchaguzi mkuu wa vyama vingi wa 1995, NCCR-Mageuzi walitetemesha na kutingisha .Baadae alijivua uanachama wa NCCR na kuhamia CCM.


Share:

Algeria yafunga tena biashara kwa hofu ya Corona Baada ya taratibu kukiukwa

Biashara nyingi nchini Algeria zilizokuwa zimefunguliwa wiki iliyopita, zimefungwa tena, katika maeneo kadhaa ya nchi hiyo, kwa sababu ya kutofuata kanuni za usafi na hatua ya kutokaribiana kwa umbali wa mita moja.

Tangu kuanza kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani zaidi ya wakuu 15 wa majimbo kati ya 48 wamejikuta hatua walizochukua kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona hazitekelezwi na wafanyabiasha pamoja na raia katika majimbo yao, na hivyo kuagiza kufungwa kwa biashara zote.

Maeneo yaliyohusishwa zaidi na uamuzi huo ni maduka ya nguo, maduka ya viatu, migahawa na maduka ya mikate, yanayotembelewa sana wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, pamoja na maduka ya manukato.

Picha za milolongo ya watu wakiwa mbele ya maduka zimewakasirisha sana viongozi na maafisa wa afya nchini Algeria ambao wamesikitishwa na hatua ya wananchi ya kutoheshimu kanuni na taratibu za kuzuia maambukizo ya virusi vya Corona.

Ijumaa iliyopita, Rais Abdelmadjid Tebboune wa nchi hiyo alitishia kuongeza masharti ya raia kutotembea ikiwa hatua za kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona zitapuuziwa na kutotekelezwa ipasavyo.

Vifo 463 vimerekodiwa nchini Algeria tangu kuripotiwa kisa cha kwanza cha maambukizi ya virusi vya Corona, Februari 25, kulingana na kamati ya kisayansi inayofuatilia jinsi ugonjwa huo unavyoendelea nchini.

Algeria inashika nafasi ya nne kwa idadi kubwa ya maambukizi ya virusi vya Corona barani ya Afrika baada ya kuthitisha kesi 4,474 hadi sasa.


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne May 05





















Share:

Monday, 4 May 2020

Wenye Virusi Vya Corona Nchini Kenya Wafika 490 Baada ya Wengine 25 Kuongezeka

Kenya imethibitisha maambukizi mapya 25 ya virusi vya Corona na kufikisha 490 waliothibitishwa kuwa na virusi hivyo kufikia sasa.

Wizara ya afya inasema kuwa visa 15 vinatoka jijini Nairobi na 10 kutoka kaunti ya Mombasa.

Wote wakiwa ni wakenya ambao hawana historia ya kusafiri nje ya nchi.

Naibu waziri wa afya Dkt Mercy Mwangangi anasema kuwa sampuli 1012 zilifanyiwa vipimo katika muda was aa 24 zilizopita.

Aidha watu 6 zaidi wamepona na kuruhusiwa kuondoka hospitalini na kufikisha 173 waliopona kufikia sasa.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger