Tuesday, 5 May 2020

Wafanyabiashara Wanaouza Sukari Kwa Bei Ya Juu Jijini Dar Es Salaam Kuanza Kukamatwa Kuanzia Leo

...
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amesema kuanzia leo mkoa wake utawakamata wafanyabiashara wanaouza sukari kinyume cha bei elekezi isiyozidi Sh. 2,600 kwa kilo.

Amesema katika ukaguzi wao huo, sukari itakayokamatwa inauzwa kinyume cha maelekezo ya serikali, itataifishwa huku wahusika wakikamatwa.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Makonda alisema amebaini baadhi ya wafanyabiashara wanauza kilo moja ya sukari kwa Sh. 3,500 badala ya Sh. 2,600 iliyoelekezwa na Wizara ya Kilimo.

Kutokana na hilo, amewaagiza wakuu wa wilaya zote tano mkoa huo kuhakikisha wanafanya ukaguzi wa kuwabaini wafanyabiashara hao ili wakamatwe na sukari hiyo itaifishwe.

Makonda alisema hakuna sababu ya kutumia mwezi wa Ramadhani kuwakandamiza watu.
 
Makonda alisema uongozi wa mkoa huo utaichukua sukari hiyo na kuiuza kwa bei elekezi na fedha itakayopatikana ikatumika kununua vifaa vya kuwakinga madaktari wa Mkoa wa Dar es Salaam.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger