Tuesday, 5 May 2020

Wafanyabiashara Wanaouza Sukari Kwa Bei Ya Juu Jijini Dar Es Salaam Kuanza Kukamatwa Kuanzia Leo

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amesema kuanzia leo mkoa wake utawakamata wafanyabiashara wanaouza sukari kinyume cha bei elekezi isiyozidi Sh. 2,600 kwa kilo.

Amesema katika ukaguzi wao huo, sukari itakayokamatwa inauzwa kinyume cha maelekezo ya serikali, itataifishwa huku wahusika wakikamatwa.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Makonda alisema amebaini baadhi ya wafanyabiashara wanauza kilo moja ya sukari kwa Sh. 3,500 badala ya Sh. 2,600 iliyoelekezwa na Wizara ya Kilimo.

Kutokana na hilo, amewaagiza wakuu wa wilaya zote tano mkoa huo kuhakikisha wanafanya ukaguzi wa kuwabaini wafanyabiashara hao ili wakamatwe na sukari hiyo itaifishwe.

Makonda alisema hakuna sababu ya kutumia mwezi wa Ramadhani kuwakandamiza watu.
 
Makonda alisema uongozi wa mkoa huo utaichukua sukari hiyo na kuiuza kwa bei elekezi na fedha itakayopatikana ikatumika kununua vifaa vya kuwakinga madaktari wa Mkoa wa Dar es Salaam.


Share:

MWANAMKE MWENYE LIPS KUBWA DUNIANI ACHOMA SINDANO 20 ASIDI AONGEZE UKUBWA ZAIDI


Andrea Ivanova aliyeongeza lips

Mwanamke Andrea Ivanova mwenye miaka 22 kutokea nchini Bulgaria, amesema ameongeza lips za mdomo wake ambapo siku ya Aprili 28, amechomwa sindano 20 za Asidi ya Hyaluronic ili kuongeza lips hizo.

Mwanamke huyo ambaye ni mwanafunzi wa falsafa "Philosophy" amekuwa ni mmoja kati ya watu wenye lips kubwa duniani, amesema ataendelea kuongeza lips zake mpaka pale atakapo ridhika.

Akizungumzia suala hilo la kuongeza lips zake amesema "Nazipenda sana lips zangu, nilipata ugumu kwenye kula kwa siku mbili hadi tatu baada ya kuchomwa sindano ila sasa hivi sipati ikwazo vyovyote, madaktari wamesema inatosha ila mimi nataka kubwa zaidi ila itabidi nisubiri angalau kwa miezi miwili".

Andrea Ivanova amesema alianza kufanya mabadiliko ya lips za mdomo wake mwaka 2018, na anatumia Tsh 386,258 kwa kila matibabu, hadi hakumbuki jumla ya gharama zote alizotumia kwenye lips zake.


Chanzo : Daily Mail
Share:

WABUNGE WA CHADEMA WAKIUKA MAAGIZO YA MWENYEKITI WAO FREEMAN MBOWE YA KUTOHUDHURIA BUNGENI


Wabunge wanane wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), jana walikaidi maagizo ya Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, kuwataka kutohudhuria vikao vya bunge na kujitenga kwa siku 14.

Wabunge hao na majimbo yao kwenye mabano ni Joseph Selasini (Rombo), Peter Lijualikali (Kilombero), David Silinde (Momba), Antony Komu (Moshi Vijijini), Susan Masele (Viti Maalum), Jaffary Michael (Moshi Mjini), Latifa Chande na Subrina Sungura (Viti Maalum).

Wabunge hao walihudhuria mkutano wa 18 wa kikao cha 21 cha Bunge la 11, kilichojadili na kupitisha makadirio ya bajeti ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na walikuwa katika ukumbi wa Msekwa na ukumbi mkuu wa Bunge.

Mbunge Selasini wiki iliyopita alilalamika bungeni kwa kuondolewa kwenye kundi songezi la wabunge wa Chadema na kushindwa kuchangia mjadala wowote tangu kuanza kwa bunge, hadi alipopitia kwa Spika, Job Ndugai.

Aidha, siku iliyofuata Selasini alitangaza kuendelea kuwa mbunge, lakini hana mpango wa kugombea kupitia Chadema, bali NCCR- Mageuzi, Oktoba mwaka huu.

Februari mwaka huu, Komu alitangaza kuwa atagombea ubunge jimbo hilo, na kwamba wakati ukifika atagombea kupitia NCCR- Mageuzi.


Share:

MSHUMAA WAUNGUZA NYUMBA NA KUUA WATOTO


Watoto wawili wamefariki Dunia kufuatia kuungua moto kwa nyumba waliyokuwa wakiishi, katika mtaa wa Makuburi Ubungo jijini Dar es salaam. 

Akizungumza na EA Radio Mwenyekiti wa Mtaa Makuburi, Moshi Kaftany amesema chanzo cha moto inadaiwa ni mshumaa.

Kaftany amesema kuwa "moto umetokea usiku wa kuamkia leo na wajukuu zangu wawili wamefariki, bahati mbaya zaidi, hakuna hata mpangaji aliyefanikiwa kuokoa chochote"

Share:

TANZIA: Mwanasheria na Mwanasiasa mkongwe Dk. Masumbuko Lamwai Afariki Dunia

Mwanasiasa na mwanasheria mkongwe, Dkt. Masumbuko Lamwai amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Mei 5, 2020.

Dkt. Lamwai aliwahi kuwa mbunge wa Ubungo (NCCR-Mageuzi) kabla ya kuhamia CCM na kisha  kuwa mbunge wa kuteuliwa na Rais Benjamin Mkapa.

‪Kabla ya kifo chake, Dkt. Lamwai alikuwa Mhadhiri Mwandamizi (Senior Lecture) katika Chuo Kikuu cha Tumaini akifundisha masomo ya Sheria.

Dkt. Lamwai atakumbukwa kama Mwanasiasa machachari, mwanasheria nguli na mkufunzi mwandamizi (senior lecturer) wa Tumaini University.

Akiwa NCCR-Mageuzi, alikuwa na wanasiasa wengine wakongwe kama Mabere Marando, Marehemu Dk Sengondo Mvungi(RIP), Augustine Mrema, Makongoro Nyerere, Prince Bagenda, Ndimara Tegambwage, Stephen Wassira na wengine wengi.

Katika uchaguzi mkuu wa vyama vingi wa 1995, NCCR-Mageuzi walitetemesha na kutingisha .Baadae alijivua uanachama wa NCCR na kuhamia CCM.


Share:

Algeria yafunga tena biashara kwa hofu ya Corona Baada ya taratibu kukiukwa

Biashara nyingi nchini Algeria zilizokuwa zimefunguliwa wiki iliyopita, zimefungwa tena, katika maeneo kadhaa ya nchi hiyo, kwa sababu ya kutofuata kanuni za usafi na hatua ya kutokaribiana kwa umbali wa mita moja.

Tangu kuanza kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani zaidi ya wakuu 15 wa majimbo kati ya 48 wamejikuta hatua walizochukua kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona hazitekelezwi na wafanyabiasha pamoja na raia katika majimbo yao, na hivyo kuagiza kufungwa kwa biashara zote.

Maeneo yaliyohusishwa zaidi na uamuzi huo ni maduka ya nguo, maduka ya viatu, migahawa na maduka ya mikate, yanayotembelewa sana wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, pamoja na maduka ya manukato.

Picha za milolongo ya watu wakiwa mbele ya maduka zimewakasirisha sana viongozi na maafisa wa afya nchini Algeria ambao wamesikitishwa na hatua ya wananchi ya kutoheshimu kanuni na taratibu za kuzuia maambukizo ya virusi vya Corona.

Ijumaa iliyopita, Rais Abdelmadjid Tebboune wa nchi hiyo alitishia kuongeza masharti ya raia kutotembea ikiwa hatua za kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona zitapuuziwa na kutotekelezwa ipasavyo.

Vifo 463 vimerekodiwa nchini Algeria tangu kuripotiwa kisa cha kwanza cha maambukizi ya virusi vya Corona, Februari 25, kulingana na kamati ya kisayansi inayofuatilia jinsi ugonjwa huo unavyoendelea nchini.

Algeria inashika nafasi ya nne kwa idadi kubwa ya maambukizi ya virusi vya Corona barani ya Afrika baada ya kuthitisha kesi 4,474 hadi sasa.


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne May 05





















Share:

Monday, 4 May 2020

Wenye Virusi Vya Corona Nchini Kenya Wafika 490 Baada ya Wengine 25 Kuongezeka

Kenya imethibitisha maambukizi mapya 25 ya virusi vya Corona na kufikisha 490 waliothibitishwa kuwa na virusi hivyo kufikia sasa.

Wizara ya afya inasema kuwa visa 15 vinatoka jijini Nairobi na 10 kutoka kaunti ya Mombasa.

Wote wakiwa ni wakenya ambao hawana historia ya kusafiri nje ya nchi.

Naibu waziri wa afya Dkt Mercy Mwangangi anasema kuwa sampuli 1012 zilifanyiwa vipimo katika muda was aa 24 zilizopita.

Aidha watu 6 zaidi wamepona na kuruhusiwa kuondoka hospitalini na kufikisha 173 waliopona kufikia sasa.


Share:

WATOA HUDUMA ZA AFYA SHINYANGA WAPEWA MAFUNZO NAMNA YA KUHUDUMIA WASHUKIWA NA WAGONJWA WA CORONA

Jumla ya watoa huduma za afya 56 kutoka kwenye vituo vya afya vya umma na watu binafsi wilaya ya Shinyanga na Kishapu wamepatiwa mafunzo ya namna ya kutoa matibabu kwa washukiwa na wagonjwa watakaobainika kuwa na Maambukizi ya Virusi vya Corona (COVID 19).

Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kwa ufadhili wa Shirika la Lifewater International yamefanyika leo Jumatatu Mei 4,2020 katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga.

Afisa Afya Mkoa wa Shinyanga Neema Simba amesema mafunzo hayo yatakayofanyika kwa muda wa siku mbili yanalenga kuwajengea uwezo watoa huduma za afya wawe tayari kuhudumia washukiwa wa ugonjwa wa Corona.

“Tunawashukuru Lifewater International kwa ufadhili wa mafunzo haya ambayo yamekutanisha watoa huduma za afya kutoka kwenye vituo vya afya vya umma na binafsi katika Halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Shinyanga na Manispaa ya Shinyanga”,ameongeza Bi. Neema.

Naye Meneja wa Shirika la Lifewater International mkoa wa Shinyanga, Benety Malima amesema watoa huduma za afya ni kundi ambalo linatakiwa kuangaliwa kwa jicho la pekee kwani wapo hatarini kupata maambukizi ya COVID 19 hivyo ni vyema wakajengewa uelewa wa kutosha kuhusu ugonjwa wa Corona.

“Lifewater International tumeamua kufadhili mafunzo haya kwani tunaamini sekta ya afya ni sekta ambayo ipo mstari wa mbele zaidi katika mapambano dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Corona. Watoa huduma za afya ndiyo wapo mstari wa mbele katika kuhudumia washukiwa na wagonjwa wa Covid 19”,amesema Malima.

Kwa upande wake, Mratibu wa Huduma za Matibabu Mkoa wa Shinyanga Dkt. Daniel Mzee amesema miongoni mwa mada zitakazofundishwa katika mafunzo hayo ni pamoja na Utambuzi wa washukiwa na wagonjwa wa Corona na namna ya kuchukua tahadhari kwenye maeneo yao ya kazi ili wasipate maambukizi.

Amesema pia watoa huduma wa afya watafundishwa namna ya kufanya matumizi sahihi ya vifaa vya kujikinga na maambukizi (Personal Protective Equipment - PPE) pamoja na namna ya kuvaa nguo/vazi maalumu linalotumika kuhudumia mshukiwa/mgonjwa wa Corona.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Afisa Afya Mkoa wa Shinyanga Neema Simba akizungumza leo Jumatatu Mei 4,2020 wakati  wa mafunzo kwa watoa huduma za afya kutoka kwenye vituo vya afya vya umma na watu binafsi wilaya ya Shinyanga na Kishapu yenye lengo la kuwajengea uwezo watoa huduma za afya namna ya kutoa matibabu kwa washukiwa na wagonjwa watakaobainika kuwa na Maambukizi ya Virusi vya Corona (COVID 19). Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mratibu wa Huduma za Matibabu Mkoa wa Shinyanga Dkt. Daniel Mzee akizungumza wakati wa mafunzo  kwa watoa huduma za afya wilaya ya Shinyanga na Kishapu ambapo amesema miongoni mwa mada zitakazofundishwa katika mafunzo hayo ni pamoja na Utambuzi wa washukiwa na wagonjwa wa Corona,namna ya kuchukua tahadhari kwenye maeneo yao ya kazi ili wasipate maambukizi,matumizi sahihi ya vifaa vya kujikinga na maambukizi (PPE) pamoja na namna ya kuvaa nguo/vazi maalumu linalotumika kuhudumia mshukiwa/mgonjwa wa Corona.
Meneja wa Shirika la Lifewater International mkoa wa Shinyanga, Benety Malima akizungumza wakati wa mafunzo kwa watoa huduma za afya ambapo amesema watoa huduma za afya ni kundi ambalo linatakiwa kuangaliwa kwa jicho la pekee kwani wapo hatarini kupata maambukizi ya COVID 19 hivyo ni vyema wakajengewa uelewa wa kutosha kuhusu ugonjwa wa Corona.
Watoa huduma za afya wakiwa ukumbini.
Watoa huduma za afya wakiwa ukumbini.
Katibu wa Afya Mkoa wa Shinyanga William Mambo akizungumza wakati wa mafunzo hayo.
Katibu wa Afya Mkoa wa Shinyanga William Mambo akizungumza wakati wa mafunzo hayo.
Watoa huduma za afya wakiwa ukumbini.
Mwezeshaji katika mafunzo hayo Dkt. Geofrey Mboye akitoa mada kuhusu COVID 19.
Mwezeshaji katika mafunzo hayo Dkt. Geofrey Mboye akitoa mada kuhusu COVID 19.
Watoa huduma za afya wakiwa ukumbini.
Afisa Afya Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Musa Makungu akitoa mada kuhusu COVID 19
Mafunzo yanaendelea.
Mafunzo yanaendelea.
Mafunzo yanaendelea.
Watoa huduma za afya wakiwa ukumbini.
Mafunzo yanaendelea.
 Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Share:

Wadau Wachangia Sh. Milioni 150 Kukabiliana Na Corona

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama amepokea msaada wa hundi tatu zenye thamani ya sh. milioni 150 zilizotolewa na kampuni tatu zinazozalisha nguzo za umeme nchini kwa ajili ya kusaidia mapambano dhidi ya homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona (COVID- 19).

Waziri amepokea michango hiyo kwa niaba ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa leo tarehe 4 Mei, 2020 katika Ofisi ya Waziri Mkuu Mlimwa, Jijini Dodoma. Michango hiyo imetolewa na kampuni Mufindi Woodpoles Plant and Timber Ltd, Qwihaya General Enterprises Co Ltd na Poles (T) Ltd ambapo kila kampuni imetoa sh. milioni 50.

Akizungumza wakati wa kupokea michango hiyo Waziri Mhagama aliwapongeza viongozi wa kampuni hizo kwa kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuhakikisha inapambana na janga la ugonjwa wa COVID-19.

“Nawashukuru sana kwa niaba ya Serikali na hii inaonesha uzalendo, utayari na kuhakikisha kila Mtanzania anakuwa ni sehemu ya mapambano hayo kwa vitendo,”alieleza Waziri Mhagama.

Pia, Waziri Mhagama alitumia fursa hiyo kuwasihi wakandarasi wengine pamoja na Watanzania kuendelea kushirikiana na Serikali kwa kujitolea kwa hali na mali ili kuwezesha katika kukabiliana na janga hilo.

“Tunatoa wito kwa Watanzania wote kuona umuhimu na kuguswa na janga hili kwa kuchangia kwa kadiri inavyofaa ili kuendeleza uzalendo kwa hali ya kujali na kuonesha utayari ili kudumisha hali ya utamaduni uliopo tangu awali wa umoja na mshikamano ,”alisema Waziri Mhagama. 

Aliwahakikishia wadau hao kuwa, michango hiyo itatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na kuwaeleza kuwa imefika katika eneo salama.

Awali, Waziri wa Nishati Dkt. Medadi Kalemani aliwapongeza viongozi wa kampuni hizo kwa michanga waliyoitoa kwa Serikali ambayo inakwenda kuongeza nguvu katika kukabiliana na ugonjwa wa COVID-19.

“Niwapongeze wakandarasi hawa kwa kuonesha nia ya kushiriki katika mapambano haya na wito wangu kila anayeguswa na janga hili ni faraja kubwa mnayoitoa kwa Serikalini katika kuhudumia na kusaidia katika kipindi hiki. Pia nawaomba wakandarasi wengine waige, ”alisema Dkt. Kalemani.  

IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
OFISI YA WAZIRI MKUU



Share:

Serikali Yasema Demokrasia itaendelea kuheshimiwa nchini

Na Eleuteri Mangi, WHUSM, Dodoma
Serikali inaendelea na zoezi la Kidemokrasia la wananchi kuboresha taarifa za wananchi kwenye Daftari la Kudumu la Mpiga Kura ambazo zitatumika kwenye Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Mdiwani unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2020.

Msemaji Mkuu wa Serikali na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi ameongoza zoezi hilo kwa Makatibu Wakuu leo Mei 04, 2020 hapa jijini Dodoma kuhakiki na kuhuisha taarifa zao katika ikizingatiwa leo ni siku ya mwisho kwa zoezi hilo nchini kote.

“Serikali inaendelea kukamilisha kuboresha Daftari la Kudumu la Mpiga Kura, Serikali zoezi hili ni muhimu sana kwa nchi yetu ikizingatiwa ni la kidemokrasia licha ya kwamba nchi yetu na dunia nzima inapitia kwenye changamoto tuliyonayo ya COVID-19” alisema Dkt. Abbasi.

Ameongeza kuwa Demokrasia itaendelea kuheshimiwa nchini kwa sababu ni kitu muhimu sana na viongozi hao pamoja na wananchi waliojiandikisha kutumia haki yao ya Kikatiba kuchagua viongozi wao.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome amesema kuwa Wizara yake inajukumu la kuhamasisha mambo mbalimbali ikiwemo elimu ya haki ya Mpiga kura.

“Nchi yetu imepiga hatua kubwa sana katika demokrasia kiasi kwamba tunajivunia hatua tuliyofika ni nzuri na demokrasia imekuwa ni ya kweli hakuna mwaka ambao tumevuka miaka mitano hatujafanya uchaguzi na wanannchi wamekuwa wakijitokeza kwa wingi kuwachagua viongozi wao” alisema Prof. Mchome.

Lengo la elimu ya mpiga kura ni kuwahamasisha wananchi kutumia haki yao ya kikatiba katika kujitokeza na kushiriki kuchagua viongozi wao watakao waongoza ili kujenga Demokrasia na Utawala Bora nchini hatua inaanza kwa wananachi kijiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Mpiga Kura ambalo linaratibiwa na kusimamiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).


Share:

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo Ataka Mbinu Mbadala Ya Karantini Kwa Wageni Kutoka Nje Ya Mkoa Kuinua Sekta Ya Utalii

Na Ahmed Mahmoud,,Arusha
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema ataishauri serikali kuangalia uwezekano wa kuondoa utaratibu wa sasa wa kuwaweka kwenye karantini ya siku 14 wageni wote wanaoingia mkoani hapa kwa shughuli za utalii  ili kuepusha kuwakatisha tamaa.
 
Gambo amelazimika kutoa kauli hiyo mapema leo wakati akipokea msaada wa Lita 500 za vitakasa mikono kutoka kampuni ya bia nchini, TBL na kueleza kwamba njia sahihi ya kuendelea kuchapa kazi ni pamoja na kuruhusu watalii walioonyesha nia kuingia nchini kama njia moja wapo ya kuvutia utalii .
 
Alisema wapo wageni wengi walioonyesha nia ya kutembelea vivutio mbalimbali mkoani hapa ila wanakumbwa na kikwazo cha Karantini jambo linalowakatisha tamaa na hivyo ameonelea ipo haja ya kuishauri serikali kubadilisha kipengere hicho ili kuangalia namna nzuri zaidi itakayowapendeza watalii bila kueneza maambukizo ya Korona.
 
Amesema sekta ya utalii ni muhimu sana kwa ustawi wa mkoa wa Arusha hivyo ameonelea ipo haja kwa watalii walioonyesha nia yakuingia nchini kuanzia mwezi juni mwaka huu kupewa utaratibu mpya wa maambukizi ya ugonjwa wa Korona badala ya kuwekwa kwenye Karantini ambayo huwapotezea muda na kuwaongezea gharama zaidi.
 
“Tunafikiria mkoa wa Arusha kuishauri  serikali ili kile kipengere cha Karantini iweze kukiondoa ili kuepuka kuwakatisha tamaa watalii walioonyesha nia ya kuja mkoani hapa kuanzia mwezi juni mwaka huu”Amesema Gambo
 
Katika hatua nyingine Gambo alisema kuwa mkoa wa Arusha utaendelea kutoa elimu kwa wananchi sanjari na kuwaondoa hofu ikiwemo kuondoa misongamano isiyo ya lazima kwa kuweka utaratibu wa mazishi kwa watu wasiozidi 10  na kuwa sio kila anayefariki basi amefariki wa Ugonjwa wa Covid 19.
 
Awali Meneja Uzalishaji wa kiwanda Cha bia cha TBL ,Joseph Mwaikasu alisema kampuni imeona uhitaji wa jamii na kuunga Juhudi za Serikali za kukabiliana na Ugonjwa wa homa Kali ya mapafu Covid 19 kwani hata wafanyakazi wao idadi kubwa ni wakazi wa mkoa wa Arusha.
 
Alisema kuwa wataendelea kuunga mkono juhudi za Serikali kwa kuhakikisha waendelea kusaidia katikamapambano dhidi ya janga hili hatari
 
Kwa upande wake Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha Richard Kwitega alizipongeza baadhi ya Taasisi na mashirika mbalimbali ambayo yamekuwa yakitoa vifaa kwa ajili ya kupambana na Ugonjwa huo na kutaka wengine kuendelea kujitokeza kusaidia.


Share:

Serikali Yawataka Wafanya Kazi Wa Saluni Wachukue Tahadhari Dhidi Ya Maambukizi Ya Corona

Na WAMJW – DSM
Serikali kupitia Wizara ya Afya imetoa wito kwa Wafanya kazi katika maeneo ya saluni kuchukua tahadhari ili kujikinga dhidi ya maambukizi ya homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona katika maeneo yao.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kitengo cha maji na usafi wa mazingira, Wizara ya Afya, Ndg. Anyitike Mwakitalima wakati akitoa elimu kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kuhusu kuchukua tahadhari za kujikinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona.

“Kwa wale ambao wanasafisha nywele, kucha, wanafanya masaji, wanaosuka nywele, mchukue tahadhari kwasababu mpo katika hatari kubwa sana ya kuambukizwa lakini vile vile kuambukiza watu wengine maambukizi ya virusi vya Corona” alisema

Aliendelea kusema kuwa, Serikali inaendelea kuwakumbusha wafanya kazi wote katika maeneo ya saluni kuhakikisha wanaepuka msongamano pindi wanapokuwa katika majukumu yao, huku akisisitiza ni muhimu kwa kinyozi kuvaa Barakoa pindi ananyoa.

“Tunawakumbusha tena, kwa upendo kabisa, Tunawakumbusha muepuke msongamano ndani, awepo mtu anaenyoa na anaenyolewa na yule ambae ananyoa ahakikishe muda wote amevaa Barakoa, tunawaambia hivi kwasababu tunawapenda” alisema.

Kwa upande wake, Sfaff sergeant (S/Sgt ) Valentine Ngowi, amewataka madereva wote wa vyombo vya moto hususan bodaboda na bajaj kuhakikisha wanavitakasa vyombo vyao vya usafiri kwa sabuni mara kwa mara ili kuua maambukizi ya virusi vya Corona endapo vitakuwepo.

Nae, Balozi wa kampeni ya Mikoni safi, Tanzania salama, Msanii Mrisho Mpoto (Mjomba) amesisitiza kuwa ili kupambana na ugonjwa huu watu wasichoke kunawa mikono kwa sabuni na maji safi yanayotiririka ili kuepuka kupata maambukizi ya virusi vya Corona.

Uhamasishaji huu unafanywa kupitia kampeni hii ya “Mikono safi, Tanzania salama” inaratibiwa na Wizara ya Afya, kwa kushirikiana na Shirika lisilo la kiserikali la Project CLEAR kwa kushirikiana na Msanii Mrisho Mpoto (Mjomba) kutoka Mjomba Theatre Gallery unaendelea katika Jiji la Dar es Salaam.


Share:

Je? Umeachwa na mke/ mume/mchumba na bado unampenda ?

Je? Umeachwa na mke/ mume/mchumba na bado unampenda ? Kuna mtu unamtaka unashindwa kumwambia? 

Ipo dawa ya kumvuta  mume, mke ,mchumba na mtu yoyote unaye muhitaji katika mahusiano na kumfanya atimize unachokiitaji kutoka kwakwe na kumfunga asiwe na mtu mwingine zaidi yako hata kama yupo mbali ndani ya masaa .(2) tu na kukutafufuta yeye mwenyewe  .

Unamatatizo ya kushika mimba ? Na ukishishika zinaharibika?dawa zipo . 

PIA.TUNAYO DAWA YA ASILI YA NGUVU ZA KIUME YENYE KUTIBU MATATIZO MATATU KWA WAKATI MMOJA (1)nguvu za kiume ,(2) Kuongeza maumbile (3)kuchelewa kufika  kilelen.

Yajue .matatizo yanayosababisha upungufu wa nguvu za kiume .
(1)ngiri ya kupanda na kushuka 
(2)korodani moja kuvimba 
(3)tumbo kuunguruma,kujaa ges.
(4)kisukari 
(5)presha
(6)kiuno kuuma 
(7)kutopata choo 

 Tunatibu kisukari Suki (14)vidonda vya tumbo siku(30) mmiguu kufa ngazi,kuwaka moto .anapandikiza nyota ya kushinda bahati  na sibu ,kusafisha nyota kukupa mvuto wa ajabu ,kutoa nuksi na mifungo mbalimbali zindiko za nyumba na biashara  Peter za bahati .huzuia chuma ulete kwenye biashara .hurudisha Mali zilizopotea anao uwezo wa kumurudisha alie mbali au alie chukuliwa msukule :humaliza kesi ya aina yoyote ndan ya siku .(4)PIA TUNATIBU.BUSHA BILA OPRESHEN. 

Kwa mawasiliano tupigie No.0747100745( Namba hii pia iko Whatsapp)

Share:

Mkurugenzi wa Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii asimamishwa kazi......Waziri Ummy Aunda Tume Ya Uchunguzi Wa Mwenendo Wa Maabara Ya Taifa




Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger