Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mh. Angela Kairuki akitoa hotuba ya ufunguzi wa Kongamano la Uwekezaji mkoa wa Songwe lililoenda sambamba na uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji wa mkoa huo ulioandaliwa na ESRF kwa ufadhili wa UNDP lililofanyika kwenye viwanja vya CCM katika halmashauri ya wilaya ya Mbozi mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Brig.Jen (MST), Nicodemas Mwangela akitoa salamu za mkoa wake kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua Kongamano la Uwekezaji mkoa wa Songwe lililoenda sambamba na uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji wa mkoa huo ulioandaliwa na ESRF kwa ufadhili wa UNDP lililofanyika kwenye viwanja vya CCM katika halmashauri ya wilaya ya Mbozi mkoani humo.
Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila akitoa salamu na kuitambulisha meza kuu wakati wa uzinduzi wa Kongamano la Uwekezaji mkoa wa Songwe lililoenda sambamba na uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji wa mkoa huo ulioandaliwa na ESRF kwa ufadhili wa UNDP lililofanyika kwenye viwanja vya CCM katika halmashauri ya wilaya ya Mbozi mkoani humo.
Mtafiti Mkuu Mshiriki wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Hoseana Lunogelo akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF wakati wa uzinduzi wa Kongamano la Uwekezaji mkoa wa Songwe lililoenda sambamba na uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji wa mkoa huo ulioandaliwa na ESRF kwa ufadhili wa UNDP lililofanyika kwenye viwanja vya CCM katika halmashauri ya wilaya ya Mbozi mkoani humo.
Waziri wa Kilimo ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Vwawa, Mh. Japhet Hasunga akitoa salamu wakati wa uzinduzi wa Kongamano la Uwekezaji mkoa wa Songwe lililoenda sambamba na uzinduzi wa Mwongozo wa Uwekezaji wa mkoa huo ulioandaliwa na ESRF kwa ufadhili wa UNDP lililofanyika kwenye viwanja vya CCM katika halmashauri ya wilaya ya Mbozi mkoani humo.
Ofisa Mwandamizi Uhamasishaji na Uwekezaji wa Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji (EPZA), Nakadongo Fares akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kongamano la Uwekezaji mkoa wa Songwe lililoenda sambamba na uzinduzi wa Mwongozo wa Uwekezaji wa mkoa huo ulioandaliwa na ESRF kwa ufadhili wa UNDP lililofanyika kwenye viwanja vya CCM katika halmashauri ya wilaya ya Mbozi mkoani humo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya uchimbaji dhahabu ya Shanta Gold Mine, Romani Urasa akitoa ushuhuda kuhusu uwekezaji waliofanya mkoani Songwe wakati wa halfa ya uzinduzi wa Kongamano la Uwekezaji mkoa wa Songwe lililoenda sambamba na uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji wa mkoa huo ulioandaliwa na ESRF kwa ufadhili wa UNDP lililofanyika kwenye viwanja vya CCM katika halmashauri ya wilaya ya Mbozi mkoani humo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mh. Angela Kairuki (wa pili kushoto) akizindua Mwongozo wa Uwekezaji wa mkoa wa Songwe ulioandaliwa na ESRF kwa ufadhili wa UNDP wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kongamano la Uwekezaji mkoa wa Songwe lililoenda sambamba na uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji wa mkoa huo lililofanyika kwenye viwanja vya CCM katika halmashauri ya wilaya ya Mbozi mkoani humo. Wanaoshuhudia tukio hilo ni kutoka kushoto ni Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila, Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Brig.Jen (MST), Nicodemas Mwangela, Waziri wa Kilimo ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Vwawa, Mh. Japhet Hasunga, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Songwe, Ndg. Elynico Mkola.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mh. Angela Kairuki (wa tatu kushoto) akionyesha nakala ya Mwongozo wa Uwekezaji wa mkoa wa Songwe ulioandaliwa na ESRF kwa ufadhili wa UNDP mara baada ya kuzindua wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kongamano la Uwekezaji mkoa wa Songwe lililoenda sambamba na uzinduzi wa mwongozo huo lililofanyika kwenye viwanja vya CCM katika halmashauri ya wilaya ya Mbozi mkoani humo. Wanaoshuhudia tukio hilo ni kutoka kushoto ni Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila, Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Brig.Jen (MST), Nicodemas Mwangela, Waziri wa Kilimo ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Vwawa, Mh. Japhet Hasunga, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Songwe, Ndg. Elynico Mkola.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mh. Angela Kairuki akimkabidhi Waziri wa Kilimo ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Vwawa, Mh. Japhet Hasunga nakala ya Mwongozo wa Uwekezaji wa mkoa wa Songwe ulioandaliwa na ESRF kwa ufadhili wa UNDP mara baada ya kuzindua wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kongamano la Uwekezaji mkoa wa Songwe lililoenda sambamba na uzinduzi wa mwongozo huo lililofanyika kwenye viwanja vya CCM katika halmashauri ya wilaya ya Mbozi mkoani humo. Wanaoshuhudia tukio hilo ni ni Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Brig.Jen (MST), Nicodemas Mwangela
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mh. Angela Kairuki akimkabidhi Mkurugenzi wa Taasisi Binafsi Nchini Tanzania (TPSF), Godfrey Simbeye nakala ya Mwongozo wa Uwekezaji wa mkoa wa Songwe ulioandaliwa na ESRF kwa ufadhili wa UNDP mara baada ya kuzindua wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kongamano la Uwekezaji mkoa wa Songwe lililoenda sambamba na uzinduzi wa mwongozo huo lililofanyika kwenye viwanja vya CCM katika halmashauri ya wilaya ya Mbozi mkoani humo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mh. Angela Kairuki akiwa kwenye picha ya pamoja na Mtafiti Mkuu Mshiriki wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Hoseana Lunogelo aliyepokea cheti kwa niaba ya wadau wa maendeleo UNDP wakati wa halfa ya uzinduzi wa Kongamano la Uwekezaji mkoa wa Songwe lililoenda sambamba na uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji wa mkoa huo ulioandaliwa na ESRF kwa ufadhili wa UNDP lililofanyika kwenye viwanja vya CCM katika halmashauri ya wilaya ya Mbozi mkoani humo. Wengine katika picha ni Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Brig.Jen (MST), Nicodemas Mwangela.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mh. Angela Kairuki akisalimiana na Mtafiti Mkuu Mshiriki wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Hoseana Lunogelo wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya maonesho kwenye uzinduzi wa Kongamano la Uwekezaji mkoa wa Songwe lililoenda sambamba na uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji wa mkoa huo ulioandaliwa na ESRF kwa ufadhili wa UNDP lililofanyika kwenye viwanja vya CCM katika halmashauri ya wilaya ya Mbozi mkoani humo. Katikati Mkurugenzi wa Taasisi Binafsi Nchini Tanzania (TPSF), Godfrey Simbeye
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mh. Angela Kairuki akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Taasisi Binafsi Nchini Tanzania (TPSF), Godfrey Simbeye (katikati) wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya maonesho kwenye uzinduzi wa Kongamano la Uwekezaji mkoa wa Songwe lililoenda sambamba na uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji wa mkoa huo ulioandaliwa na ESRF kwa ufadhili wa UNDP lililofanyika kwenye viwanja vya CCM katika halmashauri ya wilaya ya Mbozi mkoani humo. Kulia ni Mtafiti Mkuu Mshiriki wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Hoseana Lunogelo
Baadhi ya washiriki kutoka taasisi mbalimbali za sekta binafsi, serikali pamoja na wananchi wa mkoa wa Songwe walioshiriki uzinduzi wa Kongamano la Uwekezaji mkoa wa Songwe lililoenda sambamba na uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji wa mkoa huo ulioandaliwa na ESRF kwa ufadhili wa UNDP lililofanyika kwenye viwanja vya CCM katika halmashauri ya wilaya ya Mbozi mkoani humo.
Mkoa wa Songwe wazindua Mwongozo wa Uwekezaji
MKOA wa Songwe umezindua Mwongozo wa Uwekezaji na kuhamasisha wawekezaji kuchangamkia fursa lukuki zilizopo mkoani humo.
Uzinduzi huo ulifanywa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Angellah Kairuki akimwakilisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
“Uzinduzi wa Mwongozo huu unaonyesha dhamira ya kweli na utayari wa Mkoa wa Songwe kuvutia wawekezaji katika mkoa huu. Bado ninatoa rai kwa Mikoa ambayo bado haijakamilisha Miongozo wa Uwekezaji kufanya hivyo,” alisema.
Akizungumza Kairuki alisema Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, mbali na kuwapongeza wana-Songwe kwa juhudi walizofanya za kuandaa Mwongozo, aliagiza majumuisho na taarifa ya Kongamano apelekewe kwa ufuatiliaji zaidi.
“Mkoa wa Songwe una fursa nyingi sana za kiuwekezaji na hasa eneo la kilimo pamoja na kuwepo fursa nyingine kama madini, ufugaji, utalii nk. Mna mtaji mkubwa wa watu na hivyo hamna budi mkazitumia fursa hizo kubadilisha maisha,” alisema.
Kairuki aliipongeza Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa kusaidiana na Mkoa kuandaa Mwongozo wa Uwekezaji na kuhimiza uandaliwe utaratibu wa kufanya tathimini ya utekelezeji wa Miongozo pamoja na Makongamano ya Uwekezaji yanayofanyika nchini. Aidha, Kairuki alilishukuru Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kwa kuendelea kushirikiana na Serikali kufadhili uandaaji wa Miongozo pamoja na miradi mingine ya maendeleo.
Kairuki aliipongeza pia Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), kwa kufanya kazi bega kwa bega na uongozi wa Mkoa wa Songwe, kuhakikisha kuwa fursa za kibiashara na uwekezaji, zinatangazwa na pia kongamano la uwekezaji linaleta mafanikio yaliyokusudiwa.
“Nitakuwa mstari wa mbele kutangaza fursa zilizopo katika mkoa huu na pia naomba msichoke kujifunza kutoka katika mikoa mingine. Jitahidini pia kuwekeza katika miundombinu muhimu ili kuvutia wawekezaji zaidi,” alisema.
Alisema tangu alipowasili mkoani Songwe, hajasikia malalamiko yoyote kutoka kwa wawekezaji wala wananchi na hivyo aliuomba uongozi wa mkoa kuendelea kufanya kazi karibu na wawekezaji ili kuongeza mapato na makusanyo ya serikali.
Awali akimkaribisha mgeni rasmi katika kongamano hilo, Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Brig. Gen. Nicodemas Mwangela alisema Mkoa wa Songwe umeandaa Kongamano lenye lengo la kutangaza fursa na vivutio vya uwekezaji vilivyopo katika halmashauri zote za Mkoa wa Songwe ili kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.
Brig. Gen. Mwangela alibainisha baadhi ya fursa akianza na fursa kubwa ya kilimo biashara hasa kilimo cha umwagiliaji ambapo hekta 18,464 zimetengwa kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji wa matunda na mbogamboga, uzalishaji wa mbegu ambapo kwasasa asilimia 70 ya mbegu inaagizwa nje ya nchi, usambazaji wa mbolea na pembejeo za kilimo, na vifaa vya kukaushia mazao ili kuondoa sumukuvu.
Brig. Gen. Mwangela aliongeza Mkoa wa Songwe una fursa ya kuwekeza kwenya Ranchi ambapo hekta 96,434 zimetengwa wilayani Songwe na Momba. Pia aliwakaribisha Wawekezaji kuzalisha chakula cha mifugo, kuwekeza kwenye uvuvi na ufugaji samaki, kufuga mifugo, mashamba ya miti, vitalu vya uwindaji, makampuni ya usafiri na kuongoza watalii, hoteli za kitalii, kambi za watalii nk.
Aidha katibu Tawala wa Songwe David Kafulila alisema kwamba mkoa huo umejiandaa vyema kuwa lango kuu la mataifa ya SADC.
Alisema asilimia 70 za bidhaa za zinatoka bandari ya Dar es salaam zinapita Tunduma katika Mkoa wa Songwe hivyo ni vyema wawekezaji wakafika eneo hilo ambalo tayari linahitaji kuwa na Bandari Kavu.
Alisema atakayewekeza Songwe atakuwa hazungumzii soko la watu milioni 60 bali anazungumzia soko la SADC la watu milioni 400.
Akiongea kwa niaba ya Dkt Tausi Kida - Mkurugenzi wa ESRF, Dkt Hoseana Lunogelo - Matafiti Mkuu Mshiriki wa ESRF alisema ESRF imesaidia uandaaji wa Miongozo ya Uwekezaji katika Mikoa 25 ambapo Mikoa 15 imekamilisha uandaaji wa Miongozo hiyo na Mikoa mingine 10 iko katika katika hatua mbalimbali.
Miongozo hiyo imechambua na kuainisha fursa za uwekezaji zilizopo katika mikoa husika ili kuwavutia wawekezaji. Dkt Lunogelo kwa niaba yake Dkt Tausi Kida alisema kuwa Miongozo ya Uwekezaji ngazi ya Mikoa itachangia katika Mwongozo wa Uwekezaji wa Taifa. Pia aliongeza kwamba kama Mwongozo huo unatumika ipasavyo, utasaidia kwa kiasi kikubwa kuleta matokeo yaliyo kusudiwa na hasa kuboresha maisha ya wananchi.
"ESRF tutaendelea kushirikiana na Mikoa katika utekelezaji wa Miongozo hii, hasa kwa kufanya Upembuzi Yakinifu (feasibilty studies), na kuandaa Miongozo ya Biashara (Business Plans) kwa baadhi ya fursa ambazo Mikoa itapenda kuwekeza". alisema Dkt Tausi Kida katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Dk. Lunogelo.
Kwa mujibu wa Dk Kida Mwongozo huo wa uwekezaji una vipengele vikuu vitano (5). i) Sababu za Kuwekeza Mkoa wa Songwe, ii) Maelezo ya Mkoa kwa Ujumla, iii) Fursa za Uwekezaji za Kipaumbele, iv) Mazingira wezeshi, na hatua za kufuata ukitaka kuwekeza, na v) Mawasiliano Muhimu ya Mkoa.
Aidha Mwongozo utakuwa unapatikana kwenye mitandao ikiwemo tovuti ya Mkoa na ESRF (www.esrf.or.tz/invest.php).
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye aliipongeza Serikali ya Awamu Tano chini ya Rais John Magufuli kwa kufanikiwa kubadilisha fikra miongoni mwa watumishi wa umma.
“Naomba niwe mkweli Mheshimiwa Rais Magufuli amebadilisha kabisa fikra za watendaji na watumishi wa umma dhidi za dhana uwekezaji na biashara. Waziri Kairuki amekuwa msaada mkubwa sana katika eneo la uwekezaji na biashara,” alisema Simbeye.
Alisema Sekta Binafsi ina imani kubwa na Rais Magufuli kupitia waziri wake Kairuki, ambaye kwa muda mfupi tangu ateuliwe, ametembelea maeneo mbalimbali hapa nchini na kuzungumza na wawekezaji.
“Ameweza kukutana na wawekezaji na wafanyabiashara kuwasikiliza changamoto mbalimbali zinazowakabili na kuzitafutia ufumbuzi wa haraka. Kama Sekta Binafsi tutaendelea kufanyakazi kwa karibu ili kufikia azma ya Serikali ya kujenga uchumi wa kati wa viwanda ifikapo mwaka 2025,” aliongeza.
Aidha, mmoja wa wadhamini wa kongamano hilo Benki ya NMB kupitia Ofisa Mkuu wa Wateja Binafsi, Biashara Ndogo na za Kati, Filbert Mponzi alisema benki hiyo imetoa jumla ya Sh bilioni 22 katika Mkoa wa Songwe kwenye sekta ya kilimo hasa katika mazao ya kahawa, mahindi na mengine yanayolimwa mkoani humo.
Alisema kwa mwaka huu benki hiyo imeanza kufungua akaunti kwa ajili ya wakulima kufuatia wito wa Serikali kupitia Wizara ya Kilimo kwamba wakulima wote lazima walipwe kupitia akaunti zao za benki. Aliongeza kuwa akaunti hizo zitafunguliwa bure ili wakulima wote waingie katika mfumo ambao uko rasmi.
Bw. Mponzi alisema Benki ya NMB imeanza kutoa mikopo kwa wajasiriamali yenye riba nafuu lakini hata yenye dhamana ambazo siyo rasmi ikiwa na lengo la kuwawezesha wajasiriamali wadogo wote wanufaike na mikopo yao.
Alisema kutokana na mikopo hiyo wana imani watatokea wawekezaji wa kati hata wadogo Songwe watakaoenda kupata mkopo katika benki hiyo katika uwekezaji wake ambao imetoa mikopo ya Sh bilioni 400 kwa wajasiriamali wadogo na wa kati.
Wafadhili wengine waliopata fursa ya kutoa neno wakati wa uzinduzi wa Mwongozo ni pamoja na Benki ya CRDB pamoja na Shanta Mining.
Uzinduzi wa Mwongozo wa Uwekezaji Mkoa wa Songwe ulienda sambamba na Kongamano la Uwekezaji ambalo lilianza tarehe 15 Februari 2020 na kuhitimishwa tarehe 17 Februari 2020 na Mhe. Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda. Baada ya Mhe. Pinda kufunga rasmi Kongamano hilo, washiriki walipata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ya uwekejazi mkoani humo pamoja na vivutio vya utalii.