Monday, 17 February 2020

RC Tabora Awataka TRA Kutumia Tehama Kujenga Mazingira Rafiki Na Mlipa Kodi

...
NA TIGANYA VINCENT
WATUMISHI wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wametakiwa kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kujenga mazingira rafiki kwa mlipa kodi ili aweze kutumia mifumo hiyo katika ulipaji kodi na hivyo kuongeza mapato ya Serikali.

Kauli hiyo imetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati akifunga mafunzo ya siku sita ya matumizi ya mifumo ya TEHAMA katika utendaji kazi kwa  Watendaji wa TRA wa Mikoa ya Katavi, Kigoma na Tabora wanaohusika na ukusanyaji wa mapato.

Alisema ni vema wakatumia elimu waliyopata kuboresha utoaji wa huduma ambap watamfanya  Mlipa kodi aweze kutumia muda mfupi na gharama nafuu katika ulipaji kodi jambo ambalo litasaidia kuongeza mapato ya Serikali.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka Wafanyakazi hao wa TRA kuendelea kutoa elimu kwa wananchi ili wajue wajibu wao katika kulipa kodi kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.

Naye Meneja wa Mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Lazaro Swai alisema lengo la mafunzo hayo ilikuwa ni  kuwaongezea ujuzi watumishi ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi na hivyo kuongeza mapato ya Serikali.

Alisema kuwa elimu waliyopata itawasaidia kuwawezesha walipa kodi kuweza kulipa Kodi katika mazingira jirani ikiwemo Ofisi kwao au kwa Wakala badala ya kusafiri hadi TRA na kutumia muda na gharama za usafiri.

Swai alisema Mifumo ikitumika vizuri itasaidia kuongeza ukusanyaji wa mapato ya Serikali na hivyo kuwa na fedha nyingi za kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ya wananchi.

Kwa upande wa Meneja wa TRA Mkoa wa Tabora Thoams Masese alisema mafunzo yaliyotolewa yatawasaidia watumishi wa TRA katika kuwasaidia walipa kodi ili waweze kulipa katika mazingira ambayo wataona ni rahisi kwao na kuwapunguzia usumbufu na hivyo kuwezesha kuongeza makusanyo ya Serikali.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger