Polisi nchini Rwanda imetangaza kwamba msanii maarufu wa nyimbo za injili, Kizito Mihigo amejinyonga.
Kwa mujibu wa tangazo la polisi maiti ya msanii huyo imepatikana katika chumba alicho kuwemo, anazuiliwa kwenye kituo cha polisi mtaa wa Remera, mjini Kigali.
Polisi imesema kwamba amejinyonga siku tatu baada ya kukamatwa karibu na mpaka baina ya Rwanda na Burundi katika kile ambacho jeshi hilo inasema alikuwa na nia ya kutoroka nchi na kujiunga na makundi ya waasi dhidi ya Rwanda.
Alikuwa ameanza kufanyiwa uchunguzi kuhusu madai hayo pamoja na kutaka kuwahonga wananchi waliomkataa.
Mwaka uliopita aliachiwa huru kwa msamaha wa rais baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka 10 jela kwa hatia ya kutaka kumuua rais na kuhamasisha raia kupinga serikali.
0 comments:
Post a Comment