Monday, 17 February 2020

Iran yasema haina nia ya kuendelea kulipa kisasi dhidi ya Marekani

...
Waziri wa mambo ya nje wa Iran Mohammed Javad Zarif ameikosoa Marekani na mapendekezo ya kufanya mazungumzo na mataifa jirani ya kiarabu, wakati alipokuwa akihudhuria mkutano wa kiusalama mjini Munich Ujerumani. 

Tangu mwanzo, Zarif aliishambulia vikali Marekani akisema rais Donald Trump amekuwa akipokea ushauri mbaya akimaanisha mshauri wa zamani wa rais wa masuala ya usalama John Bolton. 

Ameongezea kwamba Trump alishawishika kwamba Iran ilikuwa ikikaribia kuanguka hasa baada ya kujiondoa katika mkataba wa nyuklia. 

Waziri huyo wa mambo ya kigeni amekataa mazungumzo yoyote na Marekani ikiwa vikwazo havijaondolewa bado akisema utawala wa Trump umekuwa na shinikizo kubwa na kusababisha athari kubwa za kiuchumi.

 Akijibu swali juu ya kuuawa kwa kamanda Qassem Soleimani mapema mwezi Januari, Zarif ametangaza mwisho wa Iran kulipiza kisasi akisema nchi yake haina tena nia ya kuzidisha mvutano na Marekani.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger