Thursday, 13 February 2020

BENKI YA STANDARD CHARTERED YAIKOPESHA TANZANIA SH. TRILIONI 3.3 KUJENGA RELI YA KISASA

 
Waziri wa Fedha na Mipango,  Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto), na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chattered (Tanzania) Bw. Sanjay Rughani, wakionesha Hati za Mkataba wa makubaliano ya mkopo nafuu wa dola za Marekani bilioni 1.46, sawa na shilingi za Tanzania Tril. 3.3 ambazo Benki hiyo imetoa kwa ajili ya ujenzi wa Reli kwa Kiwango cha Kimataifa (SGR), kipande cha Morogogoro hadi Makutupora, mkoani Singida, hafla iliyofanyika Jijini Dar es Salaam 13 Februari, 2020. 
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto), na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chattered (Tanzania) Bw. Sanjay Rughani, wakibadilishana Hati za Mkataba wa makubaliano ya mkopo nafuu wa dola za Marekani bilioni 1.46, sawa na shilingi za Tanzania Tril. 3.3
ambazo Benki hiyo imetoa kwa ajili ya ujenzi wa Reli kwa Kiwango cha Kimataifa (SGR), kipande cha Morogogoro hadi Makutupora, mkoani Singida, hafla iliyofanyika Jijini Dar es Salaam 13 Februari, 2020.

Waziri wa Fedha na Mipango,Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto), na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chattered (Tanzania) Bw. Sanjay Rughani, wakitia saini makubaliano ya mkopo nafuu wa dola za Marekani bilioni 1.46, sawa na shilingi za Tanzania Tril. 3.3, zilizotolewa na Benki hiyo kwa ajili ya ujenzi wa Reli kwa Kiwango cha Kimataifa (SGR), kipande cha Morogogoro hadi Makutupora, mkoani Singida, hafla iliyofanyika Jijini Dar es Salaam 13 Februari, 2020. 
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa tatu kushoto)), na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chattered (Tanzania) Bw. Sanjay Rughani (wa tatu kulia), wakitia saini Hati za Mkataba wa makubaliano ya mkopo nafuu wa dola za Marekani bilioni 1.46, sawa na shilingi za Tanzania Tril. 3.3 ambazo Benki hiyo imetoa kwa ajili ya ujenzi wa Reli kwa Kiwango cha Kimataifa (SGR), kipande cha Morogogoro hadi Makutupora, mkoani Singida, hafla iliyofanyika Jijini Dar es Salaam 13 Februari, 2020. 
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa tatu kushoto), na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chattered (Tanzania) Bw. Sanjay Rughani (wa tatu kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali waliohusika na kutoa mkopo huo pamoja na utekelezaji wa Ujenzi wa Mradi wa Reli kwa kiwango cha Kimataifa (SGR), wakiwemo Balozi wa Denmark nchini Tanzania Mhe. Mette Norgaard Dissing-Spandet (wa pili kushoto) na Balozi wa Sweden nchini Tanzania Mhe. Anders Sjoberg (wa nne kushoto) baada ya kusainiwa kwa makubaliano ya mkopo nafuu wa dola za Marekani bilioni 1.46, sawa na shilingi za Tanzania Tril. 3.3 ambazo Benki hiyo imetoa kwa ajili ya ujenzi wa Reli hiyo.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa tatu kushoto) akimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango,Doto James mara baada ya kusaini Hati za Mkataba wa makubaliano ya mkopo nafuu wa dola za Marekani bilioni 1.46, sawa na shilingi za Tanzania Tril. 3.3 ambazo Benki hiyo imetoa kwa ajili ya ujenzi wa Reli kwa Kiwango cha Kimataifa (SGR), kipande cha Morogogoro hadi Makutupora, mkoani Singida
 Baadhi ya Mabalozi na Wadau wengine mbalimbali wa Maendeleo wakishuhudia utiaji saini wa Hati za Mkataba wa makubaliano ya mkopo nafuu wa dola za Marekani bilioni 1.46, sawa na shilingi za Tanzania Tril. 3.3 ambazo Benki hiyo imetoa kwa ajili ya ujenzi wa Reli kwa Kiwango cha Kimataifa (SGR), kipande cha Morogogoro hadi Makutupora, mkoani Singida.
 Sehemu ya Meza kuu ikifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye hafla hiyo fupi
 Meza kuu ikifurahia kwa pamoja huku wakibadilishana mawazo mara baada ya kusaini Hati za Mkataba wa makubaliano ya mkopo nafuu wa dola za Marekani bilioni 1.46, sawa na shilingi za Tanzania Tril. 3.3 ambazo Benki hiyo imetoa kwa ajili ya ujenzi wa Reli kwa Kiwango cha Kimataifa (SGR), kipande cha Morogogoro hadi Makutupora, mkoani Singida
 Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango akizungumza jambo na Wadau wa Maendeleo mara baada ya kusaini Hati za Mkataba wa makubaliano ya mkopo nafuu wa dola za Marekani bilioni 1.46, sawa na shilingi za Tanzania Tril. 3.3 ambazo Benki hiyo imetoa kwa ajili ya ujenzi wa Reli kwa Kiwango cha Kimataifa (SGR)

***
SERIKALI kupitia Wizara ya fedha imeweza kupata mkopo wa shilingi trilioni 3.3 kupitia waabia 17 wakishirikiana na benki ya Standard Chartered ili kuwezesha mradi wa reli ya kisasa kukamilika kwa wakati.

Akizungumza katika hafla ya usainishaji wa mikataba ya mkopo huo, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.Philip Mpango amesema kuwa kila mara wamekuwa wanaomba mabenki ya hapa nchini kuchangia katika miradi mikubwa ya vipaumbele vya taifa ili kuweza kufikia malengo yetu kama taifa.

“Mradi huu wa kujenga reli ya kisasa ni mradi ambao unakwenda kubadilisha maisha ya wananchi wakitanzania, hivi sasa unavyojengwa unawaajiri watanzania wengi, mradi huu unatumia baadhi ya vifaa ambavyo vinazalishwa hapa nchini hususani saruji, mchanga lakini nguvu kazi ni ya vijana wetu”. Amesema Dkt.Mpango.

Aidha Dkt.Mpango amesema kuwa deni la nchi yetu bado ni himilivu na ni lazima tukope kwasababu reli hii tunawekeza takribani miaka 200 ijayo. Hii reli iliyopo (ya zamani) imekuwepo takribani miaka 100, hii ya kisasa itakaa zaidi ya miaka 200.

“Kuna baadhi ya waabia wetu tena wa siku nyingi tuliwaomba waingie kwenye safari hii ya kuchangia mkopo wala si kama wanatupa bure lakini walinikatalia kwahiyo tunashukuru sana kupitia kwenu serikali ya Denmark  na serikali ya Sweden kuwa waabia wazuri na marafiki wa watanzania”. Ameongeza Dkt.Mpango.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Sanjay Rughani amesema kuwa zoezi la kuwekeana saini ya makubaliano ya mkopo kwaajili ya mradi wa reli ya kisasa ni hatua kubwa hasa katika suala la uchumi pamoja na upande wa uwekezaji.

“Afrika inabaki kuwa kipaumbele kwa biashara yetu na wateja kwa ujumla, tunajivunia kutumia utaalamu wetu kusaidia serikali ya Tanzania na fedha zinazohitajika kwenye mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa wa SGR”. Amesema Sanjay.

Pamoja na hayo Sanjay amesema kuwa upatikanaji wa wawekezaji 17 kusaidia mkopo huo ni juhudi kubwa imefanyika hivyo tutegemee kuwepo kwa maendeleo pamoja na ukuaji wa uchumi.

Nae Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa amesema kuwa mpaka kuwezesha upatikanaji wa mkopo kwaajili ya mradi huo, kutaongezeka kwa kasi ya ujenzi huo kwani mpaka sasa ujenzi kutoka Dar es Salaam mpaka mkoani Morogoro umefikia asilimia 73, hivyo mkopo huo utawezesha ujenzi wa reli hiyo kutoka mkoani Morogoro hadi Makutupora mkoani Singida.
Share:

Waziri Mkuu: Muundo Wa Halmashauri Ya Jiji La Dodoma Ukamilishwe

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameiagiza Ofisi ya Rais–TAMISEMI ishirikiane na mamlaka nyingine, zihakikishe zinakamilisha mchakato wa muundo wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma.

Pia, Waziri Mkuu ameitaka Halmashauri ya Jiji la Dodoma iongeze kasi ya upimaji wa viwanja pamoja na kusimamia kikamilifu udhibiti wa uendelezaji holela wa makazi. “Hatuhitaji kuona Jiji la Dodoma likiwa na makazi yasiyopimwa na holela.”

Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo leo (Alhamisi, Februari 13, 2020) wakati akizindua mpango kabambe wa jiji la Dodoma katika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma.

Waziri Mkuu amesema Serikali haitaki kuona jiji la Dodoma likiwa na makazi yasiyopimwa na holela kwani kasi ndogo ya upimaji wa viwanja kwa halmashauri ya jiji ndiyo itakayosababisha wananchi kujenga makazi holela yasiyopimwa.

Amesema wananchi hawawezi kuisubiri halmashauri bali halmashauri ndiyo inapaswa kuendana na kasi ya mahitaji ya wananchi. “Tayari katika baadhi ya maeneo wananchi wameanza na wanaendelea kujenga bila kufuata taratibu zinazotawala masuala ya ujenzi mijini.”

Waziri Mkuu ameongeza kuwa upimaji wa maeneo uende sambamba na uendelezaji wa miundombinu na huduma muhimu katika maeneo, ikiwemo maji na barabara. “Kasi ya uboreshaji barabara za mitaa iongezwe.”

Pia, Waziri Mkuu amesema halmashauri ya Jiji la Dodoma iweke utaratibu mzuri wa ufuatiliaji, utekelezaji na tathmini ya Mpango Kabambe ili kuhakikisha mpango huo unatekelezwa kikamilifu.

“Hili ni takwa la kisheria kwa mujibu wa kifungu namba 14(3) cha Sheria ya Mipango Miji ya Mwaka 2007 ambacho kinaitaka kila mamlaka ya upangaji kutoa taarifa ya utekelezaji wa Mpango Kabambe kila mwaka katika maeneo yao ya upangaji kwa Mkurugenzi wa Maendeleo ya Makazi.”

Hata hivyo, Waziri Mkuu ameiagiza halmashauri ya Jiji la Dodoma ianzishe mchakato wa kutambua nyumba zote zilizojengwa kwenye barabara kwa lengo la kujua idadi kamili, uhalali wao kuwepo au kama ni wavamizi na baadaye kuandaa utaratibu wa fidia kwa wananchi wanaostahili.

Kadharika, Waziri Mkuu ametoa wito kwa viongozi wa Mkoa wa Dodoma, Wizara, Halmashauri, Taasisi, sekta binafsi, Jumuiya za Kimataifa, wananchi na wadau wengine kuendelea kutoa ushirikiano katika utekelezaji wa Mpango Kabambe ili kufikia malengo ya kuwa na jiji bora, lenye mandhari ya kuvutia na litakalokidhi mahitaji ya kijamii na kiuchumi ya sasa na ya baadae.

Uamuzi wa kuhamishia shughuli za Serikali Dodoma ulifanyika mwaka 1973 ikiwa ni maelekezo ya Chama cha TANU kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa utawala wa awamu ya kwanza chini ya Uongozi wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

 (mwisho)
IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU


Share:

Benki ya CRDB Yatoa Udhamini Mnono Tamasha la Sauti za Busara!

Msimu wa 17 wa Sauti za Busara umeanza rasmi leo Alhamis ya Februari 13 hadi 17 utakaofanyika eneo la kihistoria Ngome Kongwe likiwa na wadhamini mbalimbali ikiwemo Benki ya CRDB. 


Akizungumza na waandishi wa habari katika hafla iliyofanyika katika Hoteli ya Marumaru, Stone Town, Zanzibar mwakilishi wa Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Zanzibar Ndugu Jerome Saraka ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Makusanyo ya VISA uwanya wa ndege amesema: "Leo tunapotambulisha rasmi udhamini huu wa milioni 20, tunadhamiria kulenga mambo makubwa matatu, moja kuongeza nguvu katika kutangaza vivutio vya utalii vya nchi yetu katika tamasha hili la Sauti za Busara, mbili kushiriki katika juhudi za kufungua milango ya uwezeshaji kiuchumi kupitia watalii ambao watakuwa wakihudhuria katika tamasha hili la Sauti za Busara na tatu kushiriki katika juhudi za kutambulisha vipaji vya muziki na uigizaji ambavyo ni sehemu kubwa ya ajira kwa vijana wa taifa hili.
Kupitia kampeni yetu ya malipo kwa kadi ya “Scan, Chanja, Lipa Sepa,’ benki itaendelea kuwahamasisha wahudhuriaji wa tamasha la sauti za Busara kutobeba pesa taslimu, kwani wanaweza kufanya manununzi na malipo yao , kupitia mashine zetu za kulipia fedha popote ndani ya Zanzibar. 

Aidha Benki ya CRDB pia itashiriki kikamilfu katika tamasha hili kwa kuweka gazebo la mauzo katika viwanja vya tamasha hilo. Gazebo hilo litatoa huduma ya kubadili fedha za kigeni na huduma za kuweka na kutoa fedha kupitia wakala. Benki ya CRDB pia imeandaa shindano maalumu litakalo wawezesha wateja wake kujishindia safari ya kuhudhuria tamasha hilo. Jumla ya nafasi nne zitatolewa. 

Ambapo kila mshindi atapata nafasi ya kumleta na mwenza wake. Washindi wanapatikana kupitia ushiriki wao kupitia akaunti za Benki za mitandao ya kijamii. 

Washindi wanne watalipiwa gharama zote kuanzia safari, malazi na chakula. Nawashauri wateja wetu kufuatilia taarifa za shindano hili kupitia kurasa zetu za mitandao ya kijamii ili kujua jinsi ya kushiriki na kushinda.


Share:

AMUUA MKEWE MJAMZITO KWA KUMTENGANISHA KICHWA NA KIWILIWILI

Mkazi wa Kijiji cha Mrere wilayani Rombo  mkoani Kilimanjaro Anthony Asenga (33), anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za mauaji ya mkewe, Happiness Sianga aliyekuwa na ujauzito unaokadiriwa kuwa wa miezi minane.

Asenga anatuhumiwa kumuua mwanamke huyo kwa kutenganisha kiwiliwili na kichwa chake usiku wa kuamkia jana na kisha akajisalimisha katika Kituo cha Polisi cha Mashati.

Tukio hilo limeacha simanzi katika kijiji hicho na Kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro, Salum Hamduni amesema wanamshikilia mtu huyo wakimuhusisha na mauaji hayo.

“Ni kweli kuna tukio la mume kumuua mke wake huko Rombo. Tunamshikilia mtuhumiwa,” alisema Kamanda Hamduni.

“Uchunguzi unaendelea na utakapokamilika hatua nyingine za kisheria zitafuata.”

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Sembalo, Kijiji cha Mrere, Faustina Urassa alisema wanandoa hao waliwahi kugombana na kutengana kwa muda mrefu, na kwamba siku ambayo tukio limetokea ndiyo waliyopatana na kuanza kuishi tena pamoja.
Via Mwananchi
Share:

Tanzia: Aliyewahi Kuwa Waziri Wa Viwanda Na Biashara, Idd Simba Afariki Dunia

Aliyewahi kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara katika Serikali ya Awamu ya 3, Iddi Simba amefariki dunia. 

Taarifa zilizothibitishwa na mtoto wake, Sauda Simba Kilumanga zinasema Iddi Simba amefariki katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) alipokuwa akipatiwa matibabu.

Mungu amlaze mahali pema peponi


Share:

Benki Ya Standard Chatered Yaikopesha Tanzania Sh. Trilioni 3.3 Kujenga Reli Ya Kisasa-GR

Serikali kupitia Wizara ya fedha imeweza kupata mkopo wa shilingi trilioni 3.3 kupitia waabia 17 wakishirikiana na benki ya Standard Chartered ili kuwezesha mradi wa reli ya kisasa kukamilika kwa wakati.

Akizungumza katika hafla ya usainishaji wa mikataba ya mkopo huo, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.Philip Mpango amesema kuwa kila mara wamekuwa wanaomba mabenki ya hapa nchini kuchangia katika miradi mikubwa ya vipaumbele vya taifa ili kuweza kufikia malengo yetu kama taifa.

“Mradi huu wa kujenga reli ya kisasa ni mradi ambao unakwenda kubadilisha maisha ya wananchi wakitanzania, hivi sasa unavyojengwa unawaajiri watanzania wengi, mradi huu unatumia baadhi ya vifaa ambavyo vinazalishwa hapa nchini hususani saruji, mchanga lakini nguvu kazi ni ya vijana wetu”. Amesema Dkt.Mpango.

Aidha Dkt.Mpango amesema kuwa deni la nchi yetu bado ni himilivu na ni lazima tukope kwasababu reli hii tunawekeza takribani miaka 200 ijayo. Hii reli iliyopo (Ya zamani) imekuwepo takribani miaka 100, hii ya kisasa itakaa zaidi ya miaka 200.

“Kuna baadhi ya waabia wetu tena wa siku nyingi tuliwaomba waingie kwenye safari hii ya kuchangia mkopo wala si kama wanatupa bure lakini walinikatalia kwahiyo tunashukuru sana kupitia kwenu serikali ya Denmark na serikali ya Sweden kuwa waabia wazuri na marafiki wa watanzania”. Ameongeza Dkt.Mpango.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Bw.Sanjay Rughani amesema kuwa zoezi la kuwekeana saini ya makubaliano ya mkopo kwaajili ya mradi wa reli ya kisasa ni hatua kubwa hasa katika suala la uchumi pamoja na upande wa uwekezaji.

“Afrika inabaki kuwa kipaumbele kwa biashara yetu na wateja kwa ujumla, tunajivunia kutumia utaalamu wetu kusaidia serikali ya Tanzania na fedha zinazohitajika kwenye mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa wa SGR”. Amesema Bw.Sanjay.

Pamoja na hayo Bw.Sanjay amesema kuwa upatikanaji wa wawekezaji 17 kusaidia mkopo huo ni juhudi kubwa imefanyika hivyo tutegemee kuwepo kwa maendeleo pamoja na ukuaji wa uchumi.

Nae Mkurugenzi wa Shirika la Reli hapa nchini Mhe.Masanja Kadogosa amesema kuwa mpaka kuwezesha upatikanaji wa mkopo kwaajili ya mradi huo, kutaongezeka kwa kasi ya ujenzi huo kwani mpaka sasa ujenzi kutoka Dar es Salaam mpaka mkoani Morogoro umefikia asilimia 73, hivyo mkopo huo utawezesha ujenzi wa reli hiyo kutoka mkoani Morogoro hadi Makutupora mkoani Singida.


Share:

Mawaziri wenye dhamana ya Manejimenti ya Maafa wa SADC kukutana Zanzibar

Na Daudi Manongi, MAELEZO
Mkutano wa kwanza wa kamati ya Mawaziri wanaohusika na Menejimenti ya Maafa kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) utafanyika tarehe 18-21 Februari visiwani Zanzibar, 2020 ukiwa na lengo la kuchochea juhudi zilizopo katika kupunguza madhara ya maafa ambapo mgeni rasmi atakuwa Rais wa Zanzibar, Mhe.Dkt. Ali Mohamed Shein.

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Ajira,Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma.

“Katika mkutano huu wa SADC tutajadiliana namna ya kuwekeza katika kupunguza madhara ya maafa kwa kuwa gharama za usimamizi wa maafa kama ya mafuriko huzilazimu nchi wanachama kuelekeze rasilimali zilizotengwa kwa ajili ya shughuli za maendeleo na badala yake huelekezwa katika shughuli za kurejesha hali”, aliongeza Waziri Mhagama

Ameongeza kuwa nchi wanachama ikiwemo Comoro, Malawi, Msumbiji na Zimbabwe kwa mwaka 2019 zilipata mafuriko yaliyosababishwa na vimbunga Idai na Keneth na gharama zake misaada na madhara zilikuwa kubwa sana zikikadiriwa kuwa dola bilioni 10.

Ili kwenda sambamba na juhudi za kikanda na kimataifa , Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Dkt John Pombe Magufuli itaendelea kuimarisha uwezo wake wa usimamizi wa maafa katika Nyanja zote, aliongeza Mhagama.

“Tayari Serikali ya Awamu ya Tano imetunga Sheria ya Usimamizi wa Maafa ya Kitaifa na.7 ya 2015 na kanuni zake, tunao wasifu wa janga la mafuriko na ukame wa kitaifa na mkakati wa Taifa kupunguza madhara ya maafa”, aliongeza Waziri Mhagama.

Itakumbukwa kuwa Tanzania ilichukua rasmi nafasi ya Mwenyekiti wa Jumuiya kuanzia mwezi Agosti, 2019 kwa kipindi cha mwaka mmoja hadi mwezi Agosti, 2020. Mkutano huo unafanyika kwa mara ya kwanza visiwani Zaznibar huku ukiwa na fursa kubwa kwa wananchi kwani utasaidia kukuza biashara na utalii na kujitangaza kimataifa.

Kauli mbiu ya Mkutano huu:Ushiriki wa kisekta kwenye kupunguza madhara ya maafa ni njia bora ya kuimraisha ustamilivu katika ukanda wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini wa Afrika (SADC).”



Kamati ya Mawaziri wenye dhamana ya Menejimenti ya Maafa imeanzishwa kwa lengo la kulishauri Baraza la Mawaziri wa nchi za SADC kuhusu masuala ya upunguzaji wa madhara ya maafa kikanda huku lengo mahususi likiwa ni kuwa na jukwaa la kubadilishana taarifa na uzoefu wa kiutendaji.


Share:

Urusi Yaituhumu Uturuki Kwa Kuvunja Makubaliano na Kuishambulia Syria

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Russia Bibi Maria Zakharova amesema Uturuki kutotekeleza makubaliano yaliyofikiliwa na viongozi wa Russia walipokutana mjini Sochi mwaka 2018, ni sababu kuu inayosababisha hali ya wasiwasi izidi kuwa mbaya kaskazini mwa Syria.

Bibi Zakharova amesema Uturuki imetuma jeshi kaskazini mwa Syria, kitendo ambacho kimeharibu Makubaliano ya Sochi na kusababisha hali ya wasiwasi mkoani Idlib izidi kuwa mbaya. Amesema Russia inapenda kuendelea kufanya mazungumzo na Uturuki juu ya kutuliza hali ya mkoa wa Idlib.

Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki amesema kama askari wa Uturuki walioko vituo vya uchunguzi huko Idlib watashambuliwa tena, Uturuki itafanya mashambulizi kutoka mahali popote dhidi ya jeshi la serikali ya Syria bila ya kujali Makubaliano ya Sochi.

Wakati huohuo, mjumbe maalumu wa Marekani nchini Syria Bw. James Jeffrey amekutana na naibu waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Bw. Sedat Onal na msemaji wa rais wa Uturuki Bw. Ibrahim Kalin, ambao wamejadili suala la maendeleo ya hali ya Syria pamoja na juhudi zinazofanywa kwa ajili ya kuhimiza utulivu na usalama nchini Syria.


Share:

KATIBU MWENEZI CHADEMA SHINYANGA MJINI CHARLES SHIGINO AFUKUZWA UANACHAMA CHADEMA

Katibu Mwenezi wa CHADEMA wilaya ya Shinyanga Mjini, Charles Shigino.

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)

MKOA WA SHINYANGA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NA UMMA.

YAH: KUFUKUZWA UANACHAMA NDUGU CHARLES SHIGINO.

Baraza la Uongozi Mkoa Shinyanga, katika kikao chake cha dharula kilichoketi Tarehe 11.02.2020, kimeamua kumfukuza uanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo  (CHADEMA) Ndugu Charles Shigino, aliekuwa Katibu Mwenezi  wa Jimbo la Shinyanga Mjini.

Kwa Mujibu wa Katiba ya CHADEMA ya Mwaka 2006, Toleo la 2016. Ibara ya 5.4. Inaeleza  juu ya “Kukoma kwa Uanachama.” Kwamba, Ibara 5.4. (1 , 2, na 3) inaeleza kuwa; Mwanachama atakoma uanachama wake kwa kujiuzulu , kufariki , kuachishwa ama kufukuzwa.

Kwa mantiki hiyo, Ndugu Charles Shigino, amefukuzwa Uanachama wa CHADEMA, kutokana na kupatikana na makosa ya utovu wa nidhamu na usaliti kwa Chama pamoja na kwenda kinyume cha Katiba ya Chama, Kanuni na Maadili ya Viongozi wa Chama, na hivyo; anakosa sifa ya kuwa Mwanachama wa CHADEMA kwa mujibu wa Ibara ya 5.4.5 ya Katiba ya Chama.

Aidha, Chama kinatoa taarifa kwa Umma na Wanachama kuwa Ndugu Charles Shigino, kuanzia tarehe 11.02.2020, si Mwanachama wa CHADEMA tena.


Imetolewa na;

EMMANUEL NTOBI
MWENYEKITI (M)SHINYANGA
13.02.2020
Share:

CHELSEA YANASA KIUNGO MWAFRIKa

Share:

Ajali Yaua Wanafunzi Watano Ruvuma

Wanafunzi watano wa shule ya msingi Ndelenyuma,Ruvuma wamefariki Dunia na mmoja amejeruhiwa baada ya kugongwa na Land Cruiser jana  lililokuwa likitokea Songea kwenda Madaba.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Simon Maigwa amesema ajali hiyo ilihusisha gari ndogo iliyokua na watu wawili waliokuwa wanakwenda  kufanya ukarabati wa mnara.

“Wanafunzi sita waligongwa, watano walikufa palepale na mmoja alijeruhiwa. Wanafunzi hao walikuwa upande wa kushoto wa barabara na eneo hilo lina utelezi kutokana na mvua iliyokuwa inanyesha,” amesema Maigwa.

Amesema polisi wanaendelea kumsaka dereva wa gari hilo ambaye alikimbia baada ya kuwagonga wanafunzi hao, kisha gari kupinduka.


Share:

Rugemalira aomba kuondolewa kwenye kesi ya uhujumu uchumi

Mfanyabiashara James Rugemalira, ametoa notisi kwa taasisi tisa, ikiwemo Usalama wa Taifa, TAKUKURU, Gavana wa Benki Kuu, DCI, TRA, Wakili Mkuu wa Serikali, Kamishna wa Magereza pamoja na kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini akiomba amtoe kwenye kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili.

Rugemalira ameyabainisha hayo leo February 13, 2020 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi wakati kesi hiyo ilipofikishwa kwa ajili ya kutajwa na kusema kuwa asipofanya hivyo atawasilisha hoja rasmi za kuondolewa katika kesi hiyo Mahakamani ambapo upande wa mashtaka kupitia kwa Wakili wa Serikali Wankyo Simon alisema kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Baada ya Wakili Wankyo kusema hivyo Rugemalira alinyoosha mkono akiomba kuzungumza na aliporuhusiwa alidai kuwa notisi alizoziandika na kuzituma zote zimepokelewa sehemu husika na hivyo alitarajiwa leo kuachiwa na kuondolewa katika shauri hilo.

“Nilitegemea leo Jamhuri waje na ufafanuzi juu ya barua niliyoandika kuhusu Benki ya Standard Chartered kukwepa kodi, sheria haitekelezwi, jana nimetoa notisi na kuisambaza na imepokelewa kote,”  Rugemarila.

Rugemalira pamoja na mmiliki mwenza wa zamani wa kampuni ya IPTL, Harbinder Sethi, wanakabiliwa na mashtaka 12 ikiwemo utakatishaji wa fedha, kujihusisha na mtandao wa uhalifu, utakatishaji wa fedha na kusababisha hasara ya Dola za Marekani 22,198,544.60 na Sh 309,461,300,158.27 za Tanzania, makosa ambayo wanadaiwa kuyatenda jijini Dar es Salaam na nchi za Afrika Kusini, Kenya na India.


Share:

CCM yavuna madiwani watano wa ACT Wazalendo

Madiwani  watano wa chama cha ACT Wazalendo mkoani Kigoma wametangaza kujivua uanachama wa chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Walitangaza uamuzi huo jana katika ofisi ndogo za Makao Makuu ya CCM Lumumba, Dar es Salaam.

Walisema wamechukua uamuzi huo kwa kujiuzulu nafasi zao za udiwani na nafasi zote za uongozi ndani ya ACT Wazalendo na kujinga na CCM kuanzia jana.

Madiwani hao ni Hamis Rashid (Kata ya Gungu), Amduni Nassor (Kata ya Kasingirima), Fuad Sefu (Kata ya Kasimbu), Ismail Hussein (Kata ya Kagera) na Mussa Ngogolwa (Kata ya Kipampa), wote kutoka Manispaa ya Kigoma Ujiji.

Akiwapokea madiwani hao, Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Bashiru Ally alisema anafurahi kwa kuwa kila wanapopata mwanachama mpya uwezo wa chama katika kupambana na kuendelea kuongoza nchi na Serikali zake mbili unaongezeka.


Share:

WAZIRI WA ZAMANI IDDI SIMBA AFARIKI DUNIA

Waziri wa zamani wa Viwanda na Biashara, Iddi Simba amefariki dunia leo saa Alhamisi Februari 13, 2020 saa 5 asubuhi.

Mtoto wa marehemu, Ahmad Simba amesema baba yake amefariki wakati akipatiwa matibabu katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) alikokuwa akipatiwa matibabu.

 “ni mshtuko kwetu kwa kweli, amefariki wakati akiendelea na matibabu.”
Share:

TMA yatabiri mvua kubwa mikoa 12

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetangaza hali mbaya ya hewa kwa siku tano kuanzia jana Jumatano Februari 12, 2020.

Taarifa ya TMA imeitaja mikoa inayotarajia kunyesha mvua kubwa kwa baadhi ya maeneo ni mikoa ya Lindi, Mtwara, Mbeya, Songwe, Njombe, Iringa, Ruvuma, Pwani, Dar es Salaam, Tanga, Morogoro Kusini pamoja na visiwa vya Unguja, Pemba na Mafia.

Leo Alhamisi Februari 13, 2020 mvua kubwa itanyesha kwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Lindi, Mtwara, Rukwa, Mbeya, Songwe, Njombe, Iringa, Ruvuma pamoja na kusini mwa mkoa wa Morogoro.

Ijumaa ya Februari 14, 2020 angalizo la la mvua kubwa limetolewa kwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Kagera, Mwanza, Geita, Shinyanga, Kigoma, Tabora, Rukwa, Mbeya, Songwe, Iringa, Njombe, Ruvuma pamoja na Kusini mwa mkoa wa Morogoro.

TMA imesema Jumamosi ya Februari 15, 2020 angalizo la mvua kubwa limetolewa kwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Kagera, Mwanza, Geita, Shinyanga, Kigoma, Tabora, Rukwa, Mbeya, Songwe, Iringa, Njombe, Ruvuma pamoja na Kusini mwa mkoa wa Morogoro


Share:

Lukuvi Kutekeleza Agizo La Rais Jumatatu Ijayo

Na Munir Shemweta, WANMM DODOMA
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi Jumatatu tarehe 17 Februari 2020 atakwenda katika halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni kwa ajili ya kurudisha umiliki wa ekari 750 kwa manispaa hiyo kama ilivyoelekezwa na Rais Magufuli.

Rais John Pombe Magufuli alitoa siku saba kuanzia jumanne iliyopita kwa Wizara ya Ardhi kurejesha miliki ya eneo hilo kwa Halmashauri ya wilaya ya Kigamboni kufuatia kufuta miliki ya eneo hilo ili kuwa chini ya Serikali.

Uamuzi wa Lukuvi ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli alilolitoa jumanne wiki hii baada ya kuzindua jengo la Manispaa ya Kigamboni na lile la Mkuu wa Wilaya hiyo yaliyoko eneo la Gezaulole jijini Dar es Salaam.

Akizungumza kwa njia ya Mtandao leo tarehe 13 Februari 2020 akiwa Abu Dhabi, Falme za Kiarabu anakohudhuria  Kikao cha Mawaziri wa Afrika Kuhusu Masuala ya Nyumba na Maendeleo ya Miji Lukuvi alisema, jumatatu atakuwa ofisi za Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni kwa ajili ya kutekeleza agizo la Rais kuhusiana na urejeshaji miliki ya ardhi kwa halmashauri hiyo.

‘’Jumatatu tarehe 17 Februari 2020 saa tano asubuhi nitakuwa ofisi za Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni kwa ajili ya kutekeleza agizo la mhe Rais la kukabidhi ardhi ambayo iko katika eneo la Kigamboni’’ alisema Lukuvi

Kwa mujibu wa Rais Magufuli, pamoja na kufuta umiliki wa eneo hilo ili kuwa chini ya Serikali  lakini umiliki wake haujarerejeshwa katika Manispaa ya Kigamboni na kutaka miliki hiyo kurejeshwa ndani ya wiki moja ili wananchi wapange wanavyotaka.

Hata hivyo, Magufuli alitahadharisha ardhi hiyo isije ikatumika vibaya kwani si ya viongozi bali ni kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wa kigamboni.



Share:

Wadau wa Michezo Kilimanjaro waipongeza Tigo Kili half marathon kwa kuibua vipaji vipya.

Na TIGO TEAM, MOSHI.
WADAU mbalimbali wa michezo mkoani Kilimanjaro hususani wapenzi wa mchezo wa Riadha (Mbio) mkoani hapa wamepongeza mchango mkubwa unaofanywa na Mbio maarufu Afrika mashariki na duniani kwa ujumla za Tigo Kili Half Marathon katika kuibua vipaji mbalimbali vya Wanariadha wanaoiwakilisha vyema nchi ya Tanzania katika Medani mbalimbali za Mashindano ya Mbio kitaifa na kimataifa.
 
Wakizungumzia namna mbio hizo zimesaidia kuinua vipaji vya wanariadha waliofanya vyema katika Mashindano ya Mbio kitaifa na Kimataifa kama vile Emmanuel Giniki na Alphonce Simbu; wadau hao wanafafanua kuwa, Tigo Kili Half Marathon imewaibua wanariadaha wengi mmashuhuri na ina mchango mkubwa sana katika kukuza mchezo wa ridaha nchini.
 
Mbio za tigo Kili Half Marathon zimezinduliwa hivi karibuni mjini Moshi ambapo wadau mbalimbali kutoka katika mataifa mbalimbali duniani wanatarajiwa kumiminika mkoani Kilimanjaro zinatarajiwa kuleta neema kubwa ya kiuchumi mkoani hapa.
 
Mbio hizo zilizozinduliwa rasmi katika viwanja vya kibo Palace Homes, mjini Moshi kwa kuwashirikisha viongozi mbalimbali, wadhamini, Chama Cha riadaha mkoani Kilimanjaro (KAAA), waandaaaji wa mbio hizo na wadau mbalimbali zinatarajiwa kufanyika siku ya jumapili ya Machi 1, 2020 katika viwanja vya Chuo Kikuu Cha ushirika mjini Moshi (MoCU).
 
Akizungumzia namna mbio hizo zimesaidia kuinua vipaji vipya ikiwemo Wanariadha wapya waliofanya vizuri katika mashindano ya kitaifa na kimataifa, Mwenyekiti wa Chama Riadha Maniaspaa ya Moshi (MMAAA), Abdi Massawe anafafanua kuwa kwa kutambua mchango mkubwa unaofanywa na Tigo Kili Half Marathon, chama cahake kimepeleka wakimbiaji mahiri 17 kushiriki mashindano hayo ya kilometa 21 kwa mwaka huu wa 2020.

“Pia tutapeleka wakimbiaji mbalimbali zaia ya 60 kutoka katika makundi mbalimbali ikiwemo wakimbiaji binafsi na Jogging klabu mbalimbali zilizoko mkoani Kilimanjaro kushiriki mashindano ya Tigo Kili Half Marathon…” anafafanua Abdi Massawe.
 
Massawe amewataka wananchi mbalimbali mkonai hapa kujitokeza kwa wingi kushiriki mashindano ya Tigo Kili Half Marathon kwani mbali na kuibua vipaji mbalimbali vya wanariadaha wapya, pia yatawasaidia kuboresha afya zao kupitia michezo.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini, Aidan Komba alisema: “Tigo tunajivunia kuwa wadhamini wakuu wa mbio maarufu za Tigo Kili Half Marathon kwa mwaka wa nne mfululizo. Tukiongoza sokoni kwenye mageuzi ya maisha ya kidijiti yakiwamo masuala ya fedha, tunafurahi kwa mara nyingine tena kuwezesha usajili na malipo kwa washiriki kwenye mashindano hayo yajayo kupitia kwa huduma zetu kamilifu za fedha - Tigo Pesa.

Alisema kwamba kwa miaka kadhaa sasa, Tigo Pesa imethibitishwa kuwa bora zaidi na mfumo wa kuaminika wa malipo kwa wanariadha wote wenye nia kutoka sehemu yoyote nchini. “Zaidi ya hapo, tunakaribisha kila mmoja kwa ajili ya kupata kumbukumbu za mashindano hayo na kutumia wengine kupitia mtandao wenye kasi zaidi Tanzania wa 4G+,” akasema.

“Washiriki waendelee kujisajili kupitia mtandao na kufanya malipo kwa kutumia credit card kupitia https://ift.tt/1n0Lfq7 au kupitia TIGO Pesa - Pigal *149*20# kisha fuata maelekezo,” alisema na kuongeza kwamba washiriki wajisajili mapema ili kuepuka usumbufu kwani usajiliutafungwa Februari 16,2019 au nafasi zitakapojaa.

Mwisho.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger