Wanafunzi watano wa shule ya msingi Ndelenyuma,Ruvuma wamefariki Dunia na mmoja amejeruhiwa baada ya kugongwa na Land Cruiser jana lililokuwa likitokea Songea kwenda Madaba.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Simon Maigwa amesema ajali hiyo ilihusisha gari ndogo iliyokua na watu wawili waliokuwa wanakwenda kufanya ukarabati wa mnara.
“Wanafunzi sita waligongwa, watano walikufa palepale na mmoja alijeruhiwa. Wanafunzi hao walikuwa upande wa kushoto wa barabara na eneo hilo lina utelezi kutokana na mvua iliyokuwa inanyesha,” amesema Maigwa.
Amesema polisi wanaendelea kumsaka dereva wa gari hilo ambaye alikimbia baada ya kuwagonga wanafunzi hao, kisha gari kupinduka.

0 comments:
Post a Comment